Zanzibar: Watalii wanne kutoka Israeli watimuliwa Hotelini kwa kulalamika kuhusu gari kuandikwa "Free Palestine"

Zanzibar: Watalii wanne kutoka Israeli watimuliwa Hotelini kwa kulalamika kuhusu gari kuandikwa "Free Palestine"

Zanzibar watalii wanne wa Ki Israel wametimuliwa baada ya kuleta fujo ndani ya hotel baada ya kuona gari la manager wa Hotel Hiyo Ina stika za Free Palestine

๐Ÿšจ๐Ÿ‡ฎ๐Ÿ‡ฑ๐Ÿ‡ต๐Ÿ‡ธ FOUR ISRAELIS were KICKED OUT OF A HOTEL in Tanzania for complaining about the "FREE PALESTINE" badge on the manager's car.
View attachment 2968844

Four Israelis were kicked out of a hotel in Tanzania for complaining about the free Palestine badge on the manager's car.

The Canary Nungwi Hotel in Zanzibar kicked out four Israelis who interrogated a receptionist about a vehicle parked outside the premise with stickers that read "Free Palestine." The Israelis were told the vehicle belonged to the manager of the hotel, and they were eventually kicked out after complaining that the vehicle was causing them "concern."
Wathenge hao
 
Watu wengi hawajui tofauti kati ya MENEJA wa biashara na MFANYABIASHARA. Wengi wanadhani meneja ni mfanyabiashara! Kumbe meneja yeye ni MSIMAMIZI wa biashara na wala sio MFANYABIASHARA, maana yeye hajawekeza chochote kwenye hiyo biashara. Ndio maana kwa meneja anaweza kuona kama kumpoteza mteja au kumfukuza ni sawa tu manake yeye mshahara wake uko pale pale. Ila nna uhakika kama mwenye hoteli angekuwepo eneo la tukio, hii kesi wala isingefika kwenye vyombo vya habari.
mara nyingi nimegombana na mameneja wapuuzi wasiojua customer care hufanywaje ili wateja waendelee kuja kwa wingi. Huo wingi ndio hela zenyewe. Ukifukuza mteja mmoja ataondoka na hela nyingi na kuwafanya wengine wasije hapo, biashara itadoda na mapato yatapungua
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Ukitaka kujua demokrasia ni mfumo usiowezekana kutekelezeka ni pale ambapo wanaojiita wafuasi wa demokrasia na wanachama wa vyama vya kidemokrasia hugeuka madikteta pale tu ambapo jambo fulani hali furahishi fikra na matamanio yao.

Ukisoma michango mingi humu ya wafuasi wa demokrasia ndipo utajua ni wafuasi wa udikteta waliokosa tu madaraka ya kutekeleza udikteta wao.
 
Liliitwaje?
Ilitokea nini taifa likafa?
Na taifa lilivyokufa walienda wapi na je waliondoka wote au wengine walibaki?
Linaitwa Israeli na halikuwahi kufa.Lilikufa kifo fake mioyoni mwa watu kadhaa ukiwemo wewe.
 
Shida sio Stika, bali reaction ya Waisraeli yaani kwa sababu huipendi Yanga basi hadi mwenye hotel asiweke stika yake kwa kuipenda Team?
Wewe kama shabiki wa simba, siku ya mechi refa kaja na gari limeandikwa daima mbele na picha ya guede na kapaki sehemu ambayo unaliona hutahoji?
Wao walitakiwa tu kuona Bango halijawafurahisha na pengine hata kubadili Hotel nyingine.....ila kitendo cha kumtafuta kumjua ni nani kinatia mashaka sana.
Huenda haikuhitaji kumtafuta, huyo ameweka stika ili ionekane na yeye ndo mtoa huduma, huenda walimuona wakapuuza kuja kushtuka ndiye mhudumu wao na passport zao zinaonyesha ni waisraeli na wanahudumiwa na mtu anayewaona ni maadui.
Kidiplomasia ni kosa kutaka kuingilia Hisia za Watu wengine tena nyumbani kwao.
Hisia zako zisiondoe comfort ya wageni. Wageni wanapaswa kujisikia wapo salama nyumbani kwako. Yaani wewe umeenda nchi ya watu, Tanzania ina vita na nchi X sababu ya mpaka halafu aliyekupokea na kukuhudumia kavaa tshirt imeadikwa "Tanzania ishindwe dhidi ya X" utajisikia upo salama?
 
Hiyo sasa ni Ant Semitism! Na inaonekana huenda kwa kujua ni Waisraeli,meneja amebandika stika hiyo ili kuwaudhi.Lakini hata kama walichukia wasingetimuliwa ndani ya Hotel.
Tuwe makini tusije kuharibu soko letu la Watalii.
Ukiigusa Israel umeigusa US,UK,umegusa nchi za jumuia ya Ulaya,EU!
Zinaweza kuzuia Watalii wasije.
Umeandika ujinga wa viwango wa SGR. Eti ukiigusa Israel umeigusa Ulaya na kwahiyo wanaweza kuzuia Watalii kuja TZ! Wewe lazima utakuwa Msabato manake mawazo ya kitumwa kama hayo nayasikia sana kwa ndugu zangu wengine ambao na wenyewe ni Wasabato!

Sheria za kimataifa zinatambua uwepo wa Taifa la Palestine. Aidha, non-brainwashed individuals wote duniani, including Wayahudi wenyewe na sio nyie Wayahudi Weusi, wote hao wanazungumzia Uhuru wa Palestine. Sasa leo atokee mtu ameweka tag ya Free Palestine kwenye gari yake halafu atokee mwingine aseme anakosea; na akisema kama nimekosea nenda ambako hawajakosea, mnakuaj wengine eti hiyo ni antisementism?
 
Kama hawakufanya fujo na walilalamika pekee jamaa wangewapuuza (kuwafukuza ni over the top) Na wao hawana busara huwezi kunipangia cha kufanya kwenye property yangu...
 
Linaitwa Israeli na halikuwahi kufa.Lilikufa kifo fake mioyoni mwa watu kadhaa ukiwemo wewe.
Unaleta hoja mfu jibu kama msomi.
Labda nikutolee mfano Persia(Iran) himaya yake iliwahi kufa na ikamezwa na waturuki.
Sasa na Israel taifa lao liliangukaje?
Basi sawa tuseme halijai kufa,je huko Ulaya walifikaje??
 
IMG-20240420-WA0034.jpg
 
Hata kama ni gari binafsi la meneja naona atakuwa kakosea.Yeye ni meneja/individual. Sawa.Lakini,akumbuke amefika eneo la kazi ambalo anatakiwa ahudumie watu wenye imani,misimamo,itikadi na maono tofautitofauti. Kwa mfano,mteja Muizraeli akipatwa na dharula kiafya(au chochote)itakayohitaji apate usafiri,atakabali kutumia hilo gari kweli?Na tunajua watalii wengi Zanzibar siyo Wapalestina.Ni haohao "wazungu na waizraeli" anaowakwaza.
Imani ya dini gani inayokataza au kupinga uhuru wa taifa lingine? Tangu lini itikadi za nchi moja kukandimiza nchi nyingine zikawa ni itikadi za kuwa entertained?
 
Unaleta hoja mfu jibu kama msomi.
Labda nikutolee mfano Persia(Iran) himaya yake iliwahi kufa na ikamezwa na waturuki.
Sasa na Israel taifa lao liliangukaje?
Basi sawa tuseme halijai kufa,je huko Ulaya walifikaje??
Kumbe unajua kama walifika Uropa?Wakitokea wapi?
 
Imani ya dini gani inayokataza au kupinga uhuru wa taifa lingine? Tangu lini itikadi za nchi moja kukandimiza nchi nyingine zikawa ni itikadi za kuwa entertained?
Kwa hiyo ile ni hoteli au kituo cha wapigania "uhuru"?
 
Zanzibar uchumi wake ni WA kihistoria unachangiwa pakubwa na mapato ya utalii

Raia wawe makini Sana kutumia biashara zao kama nyenzo za kueneza au kuonyesha itikadi zao. Hii ikienda viral itatuharibia. Wakati wa mwezi wao wajue Kuna wageni wasiofungamana na Imani hiyo hivyo hoteli za Umma zisifungwe na Wala wasijihusishe kabisa na watu wanaokula hadharani. Suala la Mavazi waachane kabisa na kujishughulisha na watu wamevaa nini, hata ukiona mtu mweusi usidhani ni Mtanzania wengi ni wageni waliotuletea fedha zao walizo save siku nyingi
 
Back
Top Bottom