Zanzibar 2020 Zanzibar: Watendaji wa ZEC na Polisi kupiga kura Oktoba 27 badala ya Oktoba 28

Zanzibar 2020 Zanzibar: Watendaji wa ZEC na Polisi kupiga kura Oktoba 27 badala ya Oktoba 28

Mwenyekiti wa ZEC jaji mstaafu Mahmoud ametangaza uchaguzi wa Zanzibar wa Rais, wawakilishi na madiwani kufanyika tarehe 27 na 28 Oktoba,2020.

Tarehe 27 Oktoba ni maalumu kwa watendaji wa tume, wajumbe wa tume na Polisi ambao watakuwa zamu siku ya tarehe ya uchaguzi.

Tarehe 28 itakuwa uchaguzi wa jumla

My take. Sasa ni rasmi kwamba demokrasia imechukuliwa. Tusubiri vurumai ya matokeo.
Wanachokitaka ni kufanya "divide and rule" tu, na kuanza kusikilizia mapigo kutoka kambi ya Maalim Seif. Hapo sasa inahitajika kauli thabiti yenye kutoa hadhari juu ya hila hii yenye kupelekea dhuluma juu ya hitaji la kiuongozi kwa Wanzabari
 
Mara hii wameshaambiwa hakuna kugoma.
Tusubiri wayfoward ya wapinzani wa kweli.
Tayari Kuna mamluki wa vyama vinavyoitwa vya upinzani na visivyo na ushawishi wowote kupitia umoja wao watasubiri kauli ya ACT na vyama makini, ili wao wake wapinge tu.

CCM wanawakilishwa na vyama hivyo wao wenyewe wakiwa wanaenjoy haya makarama ya kupangwa.
 
Shida ni kwamba CCM hawataki mabadiliko na hawako tayari kutoa madaraka.
 
Namuona Maalim Seif akifurahia kukamata dola........
 
Mkuu sasa hapa sanduku la kura halifunguliwi mpaka uchaguzi umalizike tar 28 so haitaweza kujua idadi ya kura za askari au wafanyakazi wa tume
ili kuondoa utopolo huo, inabidi kura wa askari zisichanganywe na za wananchi, zihesabiwe pembeni na ijulikane idadi zao...
 
Yeah! Mkapa too and that’s why he wanted a free Electoral commission different from the current FAKE ONE.

Your brain is characterised by negative attitudes
 
Chama kilicho jenga mizizi ya kidola hakiondoki bila ya nguvu za wananchi au msaada wa nchi za nje. Lakini kwa kupitia sanduku la kura sahau

Ndukiiiii [emoji2089][emoji2089][emoji2089]
Tatizo ni kumtwanga mpiga kura tu mwenzako ambaye hana hatia yoyote!!
Wezi wa kura wanaenda zao kula bata huku wapiga kura wakitwangana!!
Tena wezi wa kura wengine wanaahidiwa vyeo na kuishi maisha bora kabisa!!
Hakuna haja ya kutwangana.
Watu waishi tu kwa amani kama wezi wa kura wanavyoishi kwa amani.

Haki huinua Taifa bali dhambi ni aibu kwa watu wote.
 
Wanachokitaka ni kufanya "divide and rule" tu, na kuanza kusikilizia mapigo kutoka kambi ya Maalim Seif. Hapo sasa inahitajika kauli thabiti yenye kutoa hadhari juu ya hila hii yenye kupelekea dhuluma juu ya hitaji la kiuongozi kwa Wanzabari
Usimuamshe alie lala.
Zanzibar sio kulinda mapinduzi Bali ni kulinda Nafasi zao na watoto wao.
Anayeona anaonewa apambane na hali yake.
Tuliwaambia 2015 kuwa Wajumbe wa Baraza waende Mahakamani mana walikua na shahada za ushindi mkononi wakasusia ushindi wao matokeo yake CCM ikatawala yenyewe na kuweka watu wao kila idara badala ya serikali ya umoja wa kitaifa huku Mbowe akifurahia kifo cha CUF kwa matumaini hewa kuwa atawateka wanachama wa CUF Zanzibar. Ukweli ni kwamba Mbowe na Chama chake hakuwa na mipango ya Kimungu zaidi ya ulevi tu wa uenyekiti na pombe.

Waacheni wazanzibar wapige kura hata wiki nzima kwani matokeo wanayo tayari. Wanajua nani atashinda na nani atatagazwa .
Papara ya wapinzani na mikakati feki haitawasaidia kitu zaidi ya kubaki wakilalamika miaka 25 sasa ,yaani Robo karne.
 
Mwenyekiti wa ZEC jaji mstaafu Mahmoud ametangaza uchaguzi wa Zanzibar wa Rais, wawakilishi na madiwani kufanyika tarehe 27 na 28 Oktoba,2020.

Tarehe 27 Oktoba ni maalumu kwa watendaji wa tume, wajumbe wa tume na Polisi ambao watakuwa zamu siku ya tarehe ya uchaguzi.

Tarehe 28 itakuwa uchaguzi wa jumla

My take. Sasa ni rasmi kwamba demokrasia imechukuliwa. Tusubiri vurumai ya matokeo.
Utaratibu mzuri sana, safi
 
TUME ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imetangaza kuwa watendaji wake na askari Polisi watakaokuwa kazini siku ya uchaguzi mkuu Oktoba 28 mwaka huu, watapiga kura siku moja kabla ya siku hiyo ya uchaguzi.

Watendaji hao watapiga kura Oktoba 27 mwaka huu ili Oktoba 28 wakasimamie uchaguzi huo. Mwenyekiti wa ZEC, Jaji Mkuu mstaafu, Hamid Mahmoud Hamid alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari wakati anatangaza rasmi tarehe ya uchaguzi mkuu.

Alisema sheria ya tume hiyo imetoa nafasi kwa baadhi ya watendaji kupiga kura mapema kabla ya wengine ambayo itawahusisha watendaji waliokabidhiwa majukumu ya ulinzi ikiwemo Polisi watakaokuwa kazini siku ya uchaguzi.

Alisema kazi ya kuhesabu kura na kutangaza matokeo itakuwa Oktoba 28 -31 mwaka huu. Alisema tume imetangaza tarehe hiyo kutokana na kutamkwa kwa tarehe rasmi ya kuvunjwa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Agosti 20.

“Nimearifiwa kuvunjwa rasmi kwa Baraza la Wawakilishi Agosti 20, mwaka huu. Kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa chini ya kifungu cha 34 (3) na (4) cha sheria ya uchaguzi kwa namba 4 ya mwaka 2018 natangaza rasmi tarehe ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar itakuwa Jumatano ya tarehe 28 Oktoba 2020,”alisema.

Aliitaja ratiba ya kuelekea uchaguzi mkuu ni uchukuaji na urejeshaji wa fomu za uteuzi wa wagombea wa urais wa Zanzibar pamoja na wawakilishi na udiwani ambao utafanyika kuanzia Agosti 26 hadi Septemba 9 mwaka huu.

Alisema Septemba 10 mwaka huu ZEC itateua wagombea hao, ambapo kampeni za uchaguzi mkuu zitafanyika Septemba 11 hadi Oktoba 26.

ZEC pia imewakumbusha wadau watakaoshiriki uchaguzi mkuu ikiwemo vyama vya siasa nchini kuzingatia makubaliano ya kanuni za uchaguzi ambayo yamefikiwa na kutiwa saini kati ya vyama na tume hiyo pamoja na Jeshi la Polisi.

Kuhusu vyombo vya habari, aliwakumbusha waandishi wa habari kuzingatia maadili yao na kuandika habari zilizofanyiwa utafiti, za kweli ambazo hazitoi taarifa ya upotoshaji wananchi kuhakikisha nchi inakuwa na amani na utulivu.

‘’Tume inatoa ujumbe wake kwa vyama vya siasa na asasi nyingine zitakazoshiriki uchaguzi mkuu ikiwemo vyombo vya habari kuzingatia maadili, kanuni za uchaguzi na sheria zake ili kuepuka uvunjifu wa amani unaoweza kuingiza nchi katika vurugu za kisiasa,”alisema.
 
Si tatizo,lakini pawepo na mawakala wa vyama kisha kura zao zihisabiwe kabla ya kupelekwa tume na kila chama kiondoke na hisabu yake .
 
Mwenyekiti wa ZEC jaji mstaafu Mahmoud ametangaza uchaguzi wa Zanzibar wa Rais, wawakilishi na madiwani kufanyika tarehe 27 na 28 Oktoba,2020.

Tarehe 27 Oktoba ni maalumu kwa watendaji wa tume, wajumbe wa tume na Polisi ambao watakuwa zamu siku ya tarehe ya uchaguzi.

Tarehe 28 itakuwa uchaguzi wa jumla

My take. Sasa ni rasmi kwamba demokrasia imechukuliwa. Tusubiri vurumai ya matokeo.

======

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imetangaza Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa urais na uwakilishi utafanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa ZEC, Jaji Mkuu mstaafu, Hamid Mahmoud wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi tarehe 30 Julai 2020 visiwani humo.

Jaji Mahmoud amesema, kura ya mapema kwa watendaji wanaosimamia majukumu ya uchaguzi huo, itafanyika siku moja kabla yaani Jumanne tarehe 27 Oktoba 2020.
“Natangaza rasmi tarehe ya uchaguzi itakuwa Jumatano tarehe 28 Oktoba mwaka huu, ndugu wananchi, sheria ya uchaguzi imetoa nafasi kufanyika kura ya mapema, napenda kuwajulisha, upigaji kura ya mapema itafanyika tarehe 27 oktoba 2020 siku moja kabla ya upigaji kura pamoja,” amesema Jaji Mahmoud.

Mwenyekiti huyo wa ZEC amesema, kura ya mapema itahusisha wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wa vituo vya uchaguzi na askari polisi watakaokuwa zamu siku ya uchaguzi. Wajumbe na watendaji wa tume.

“Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, upigaji kura mapema utahusisha watendaji wanaosimamia majukumu ya uchaguzi siku ya uchaguzi, watendaji hao ni wasimamizi wa uchaguzi, wasaidizi wasimamizi uchaguzi, wasimamizi wa vituo, askari polisi watakaokuwa kazini siku ya uchaguzi ,” amesema Jaji Mahmoud.
Siku hiyo ya uchaguzi mkuu, inafanana na ile iliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania kuwa, uchaguzi mkuu utafanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

NEC ilisema shughuli ya uchukuaji fomu kwa wagombea ambapo wagombea wa ubunge na udiwani watachukua fomu tarehe 12 hadi 25 Agosti 2020, katika ofisi za NEC za halmashauri na kata nchi nzima.

Uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 25 Agosti 2020, huku kampeni zitaanza tarehe 26 Agosti hadi 27 Oktoba 2020.
Tumeliwa
 
Mkuu sasa hapa sanduku la kura halifunguliwi mpaka uchaguzi umalizike tar 28 so haitaweza kujua idadi ya kura za askari au wafanyakazi wa tume
Kwani kungekuwa na kasoro gani kama wote tungepiga kura siku hiyohiyo lakini hawa wa tume na askari wakatangulia kwenye mstari, au hata wakawa wa mwisho kupiga kura? Kwani miaka yote tulipopiga kura pamoja na hao wajeda kwenye mistari ile ile na siku ileile, yalitokea matatizo gani?
 
Back
Top Bottom