Zanzibar 2020 Zanzibar: Watendaji wa ZEC na Polisi kupiga kura Oktoba 27 badala ya Oktoba 28

Zanzibar 2020 Zanzibar: Watendaji wa ZEC na Polisi kupiga kura Oktoba 27 badala ya Oktoba 28

Kura zihesabiwe siku hiyo hiyo na ijulikane nani kapata nini. Kesho yake maboksi yaonyeshwe yakiwa tupu kabla ya kuanza kupiga kura. Bila hiyo maboksi yatajazwa kura usiku na makada wa vyama wataambiwa hizo za jana.
 
Wawakilishi wa vyama wataruhusiwa kuwepo hiyo siku ya kwanza? Angalau wajue watu wangapi wamepiga kura kwenye kila kituo.
 
Mwenyekiti wa ZEC jaji mstaafu Mahmoud ametangaza uchaguzi wa Zanzibar wa Rais, wawakilishi na madiwani kufanyika tarehe 27 na 28 Oktoba,2020.

Tarehe 27 Oktoba ni maalumu kwa watendaji wa tume, wajumbe wa tume na Polisi ambao watakuwa zamu siku ya tarehe ya uchaguzi.

Tarehe 28 itakuwa uchaguzi wa jumla

My take. Sasa ni rasmi kwamba demokrasia imechukuliwa. Tusubiri vurumai ya matokeo.

======

TUME ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imetangaza Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa urais na uwakilishi utafanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa ZEC, Jaji Mkuu mstaafu, Hamid Mahmoud wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi tarehe 30 Julai 2020 visiwani humo.

Jaji Mahmoud amesema, kura ya mapema kwa watendaji wanaosimamia majukumu ya uchaguzi huo, itafanyika siku moja kabla yaani Jumanne tarehe 27 Oktoba 2020.
“Natangaza rasmi tarehe ya uchaguzi itakuwa Jumatano tarehe 28 Oktoba mwaka huu, ndugu wananchi, sheria ya uchaguzi imetoa nafasi kufanyika kura ya mapema, napenda kuwajulisha, upigaji kura ya mapema itafanyika tarehe 27 oktoba 2020 siku moja kabla ya upigaji kura pamoja,” amesema Jaji Mahmoud.

Mwenyekiti huyo wa ZEC amesema, kura ya mapema itahusisha wasimamizi wa uchaguzi, wasimamizi wa vituo vya uchaguzi na askari polisi watakaokuwa zamu siku ya uchaguzi. Wajumbe na watendaji wa tume.

“Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi, upigaji kura mapema utahusisha watendaji wanaosimamia majukumu ya uchaguzi siku ya uchaguzi, watendaji hao ni wasimamizi wa uchaguzi, wasaidizi wasimamizi uchaguzi, wasimamizi wa vituo, askari polisi watakaokuwa kazini siku ya uchaguzi ,” amesema Jaji Mahmoud.
Siku hiyo ya uchaguzi mkuu, inafanana na ile iliyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania kuwa, uchaguzi mkuu utafanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020.

NEC ilisema shughuli ya uchukuaji fomu kwa wagombea ambapo wagombea wa ubunge na udiwani watachukua fomu tarehe 12 hadi 25 Agosti 2020, katika ofisi za NEC za halmashauri na kata nchi nzima.

Uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 25 Agosti 2020, huku kampeni zitaanza tarehe 26 Agosti hadi 27 Oktoba 2020.
Goli la mkono lileee
 
Kura zisimamiwe na Tume na mawakala. Kisha zihesabiwe siku hiyo hiyo mbele ya mawakala. Masanduku yakibaki na Tume kusubiri siku ya uchaguzi - boxes hizo zitakutwa zimejaa kura za maruhani!!
 
Kwani kungekuwa na kasoro gani kama wote tungepiga kura siku hiyohiyo lakini hawa wa tume na askari wakatangulia kwenye mstari, au hata wakawa wa mwisho kupiga kura? Kwani miaka yote tulipopiga kura pamoja na hao wajeda kwenye mistari ile ile na siku ileile, yalitokea matatizo gani?
Huu ni mpango kabambe wa kumkwamisha maalim, watu wanaenda ktk uchaguzi wakiwa na kura 1million mkononi
 
kwahiyo wakiwa wanapiga watakuwa wanasimamiwa na nani?
na mawakala je wataruhusiwa kupiga sikuhiyo na pia wakiwa wanapiga hawa pia mawakala watakuwa wakina nani ?
 
Back
Top Bottom