Zanzibar 2020 Zanzibar: Watendaji wa ZEC na Polisi kupiga kura Oktoba 27 badala ya Oktoba 28

Kura zihesabiwe siku hiyo hiyo na ijulikane nani kapata nini. Kesho yake maboksi yaonyeshwe yakiwa tupu kabla ya kuanza kupiga kura. Bila hiyo maboksi yatajazwa kura usiku na makada wa vyama wataambiwa hizo za jana.
 
Wawakilishi wa vyama wataruhusiwa kuwepo hiyo siku ya kwanza? Angalau wajue watu wangapi wamepiga kura kwenye kila kituo.
 
Goli la mkono lileee
 
Kura zisimamiwe na Tume na mawakala. Kisha zihesabiwe siku hiyo hiyo mbele ya mawakala. Masanduku yakibaki na Tume kusubiri siku ya uchaguzi - boxes hizo zitakutwa zimejaa kura za maruhani!!
 
Huu ni mpango kabambe wa kumkwamisha maalim, watu wanaenda ktk uchaguzi wakiwa na kura 1million mkononi
 
kwahiyo wakiwa wanapiga watakuwa wanasimamiwa na nani?
na mawakala je wataruhusiwa kupiga sikuhiyo na pia wakiwa wanapiga hawa pia mawakala watakuwa wakina nani ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…