Zanzibar ya Rais Mwinyi na tuhuma za ufisadi unaoanzia juu kabisa

Zanzibar ya Rais Mwinyi na tuhuma za ufisadi unaoanzia juu kabisa

Ukiwa unatoka Round about ya Maringo unaelekea Mbezi beach eneo lipo kushoto linatazamana na maghorofa ya National Housing?
Ukiwa unatoka round about ya maringo mbele ya yale maghorofa ya National Housing ndio kuna hicho kiwanja upande wa kulia, baada tu ya kiwanja kuna nyumba ya Mwinyi.

Ukimaliza zile nyumba kuna mbuyu upande wa kulia, kiwanja kinachofuata baada ya huo mbuyu upande wa kulia ukiwa unatokea mjini unakuja mbezi beach.
 
Nakumbuka kulikua na inshu kama hii miaka 10 iliyopita.ilikua ijengwe mall pale ostabay , katikati ya ubalozi wa marekani na etel. Kilichosaidi kusitishwa, ubalozi wamegoma kutokana na usama wa ubalozi wao, lakini pia kazi kubwa kuhamisha kituo cha police na tanesco. Vikwazo hivyo ndio vilifanya project hiyo isitishwe. Hiki kilikua kipindi cha jk.

Kipindi cha mkapa kunaprojet ya aina hiyo pale nyuma ya rosegorden, kalibu na ttcl. Nayo jk alivyoingia aliisitisha kwaajili ya usalama wa madishi yao ya mawasiliani (satellite).

Hawa viongozi wa kiafrika wakishashika madalaka wakishaiba hela za kutosha, wanakulupuka kutamani kufanyavitu vyaajabu bila ya kujua faida na hasara.
Afrika jamii nzima ina matatizo kuanzia viongozi mpaka watu wa kawaida, yaani kila nafsi inayozaliwa na kukulia afrika ina matatizo fulani ya ndani kabisa.
 
Asubuhi ya leo nikikatiza maeneo ya mbuyuni huku Mbezi Beach wakati naelekea mjini tulipofika maeneo ya Kwa Mwinyi, pale ilipo nyumba yake ya miaka mingi rafiki yangu akanionyesha kiwanja kikubwa chenye heka kadhaa.

Akaniambia ni kwa sababu ya mvua tu lakini kuna michakato ya ujenzi wa Mall kubwa imezuiwa na hii hali ya eneo zima kujaa maji. Nilipomuuliza mmiliki wa eneo hilo nyeti ni nani akaniambia ni Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar.

Nikakumbuka kuna video moja inatembea huko instagram inayomuonyesha mzee mmoja wa kizanzibari akiueleza uongozi wa Rais Mwinyi kwamba Nyerere alisema kiongozi wa juu kabisa ni lazima achague moja kati ya mali na utumishi wa watu anaowaongoza.

Video kama zile mara nyingi zinatolewa hadharani baada ya anayeiandaa kuwa ameshajihakikishia kuhusu hilo analolisema mbele ya watu. Mali na utumishi wa watu siku zote ni vigumu sana kwenda pamoja.

Hiyo Mall japo sijaiona ramani yake naweza kuhisi ukubwa wake utakuwa vipi kwa kutazama tu eneo lote ambalo litatumika kuijenga, namna lilivyoanzia huku barabarani likaenda mpaka kule karibu na barabara ya mzunguko inayotokea karibu na Maringo ikazunguka kule usawa wa Beach ya Kawe.

Ni eneo kubwa ambalo mpaka uwezo wa ujenzi umeweza kupatikana maana yake gharama ya ujenzi sio ndogo. Ndio hapa hizi kelele kwamba Mwinyi ni rais mwenye harufu nzuri ya utafutaji wa mali, zinaanza kuwa na mashiko, kama ni kweli hilo eneo linamilikiwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar.

Inawezekana zikawa ni tuhuma tu, zinazotokana na hulka yetu ya kitanzania. Hata Mama Sitti ambaye ni mzazi wa Rais Mwinyi aliwahi kuzushiwa eti analimiki lile jengo linalotizamana na mahakama ya Kisutu pale kwenye kona ya kuelekea posta mpya, ni tuhuma zilizokuwa zikisikika miaka ile mumewe alipokuwa Rais wa Tanzania.

Hizi ni tuhuma tu lakini la maana sana ni kwa serikali anayoiongoza kuweza kutafuta njia ya kuzijibu. Kwani wenye kutuhumu hufanya hivyo wakiongozwa na roho za chuki kwa Mheshimiwa, Njaa zikituzidi tunaanzisha habari za kumnyooshea kidole kiongozi fulani ilimradi tu kujifariji sisi wenyewe.
Hilo eneo hilo nijuavyo, ni la Hational Housing, pengine kama wameliuza au wamenyang'anywa.
 
Ila najiuliza swali moja kwani mtu akiwa kiongozi mkubwa hana mshahara? Haruhusiwi kua na maendeleo binafsi? Asiwekeze? Sasa mshahara wa kiongozi ni kula tu? Au una mipaka? Mbona sisi tunamishahara? Wengine wana biashara zao na kupitia faida kidogo anajenga ka kibanda ka kupumzikia na watoto wake? Atafungua hata kioski sasa kwa nini kiongozi? Kwamba hana maono ama? Mbona huku mtaani namaanisha kwa wasio viongozi na wao wanapambana na maisha yao? Na wao wana maono yao jamani na wana mshahara yao pia ambayo wanaweza kuipangia chochote kama sisi tu nadhani tunachopishana ni uwezo tu lakini kila mmoja ana maono yake na malengo yake ambayo anatamani kuyafikia

Sitetei ufisadi lakini tukumbuke na wao ni wanadamu na wanahaki ya kufanya wanayopenda kufanya kupitia vipato vyao.
 
Hakatazwi kuwa na mali lakini kuna mahali linaingia suala zima la mchanganyiko wa maslahi. Kwamba inambidi apambane kulinda mali zake zinazokuwa sehemu ya zile zinajulikana kwenye jamii.

Hakuna mwenye kuupenda umaskini tatizo ni pale kiongozi anapoufikiria mwenendo mzima wa biashara zake unaoingiliana na biashara za wengine tena kwenye nchi ndogo kama Zanzibar.
 
Back
Top Bottom