Zanzibar ya Rais Mwinyi na tuhuma za ufisadi unaoanzia juu kabisa

Ukiwa unatoka Round about ya Maringo unaelekea Mbezi beach eneo lipo kushoto linatazamana na maghorofa ya National Housing?
Ukiwa unatoka round about ya maringo mbele ya yale maghorofa ya National Housing ndio kuna hicho kiwanja upande wa kulia, baada tu ya kiwanja kuna nyumba ya Mwinyi.

Ukimaliza zile nyumba kuna mbuyu upande wa kulia, kiwanja kinachofuata baada ya huo mbuyu upande wa kulia ukiwa unatokea mjini unakuja mbezi beach.
 
Afrika jamii nzima ina matatizo kuanzia viongozi mpaka watu wa kawaida, yaani kila nafsi inayozaliwa na kukulia afrika ina matatizo fulani ya ndani kabisa.
 
Hilo eneo hilo nijuavyo, ni la Hational Housing, pengine kama wameliuza au wamenyang'anywa.
 
Ila najiuliza swali moja kwani mtu akiwa kiongozi mkubwa hana mshahara? Haruhusiwi kua na maendeleo binafsi? Asiwekeze? Sasa mshahara wa kiongozi ni kula tu? Au una mipaka? Mbona sisi tunamishahara? Wengine wana biashara zao na kupitia faida kidogo anajenga ka kibanda ka kupumzikia na watoto wake? Atafungua hata kioski sasa kwa nini kiongozi? Kwamba hana maono ama? Mbona huku mtaani namaanisha kwa wasio viongozi na wao wanapambana na maisha yao? Na wao wana maono yao jamani na wana mshahara yao pia ambayo wanaweza kuipangia chochote kama sisi tu nadhani tunachopishana ni uwezo tu lakini kila mmoja ana maono yake na malengo yake ambayo anatamani kuyafikia

Sitetei ufisadi lakini tukumbuke na wao ni wanadamu na wanahaki ya kufanya wanayopenda kufanya kupitia vipato vyao.
 
Hakatazwi kuwa na mali lakini kuna mahali linaingia suala zima la mchanganyiko wa maslahi. Kwamba inambidi apambane kulinda mali zake zinazokuwa sehemu ya zile zinajulikana kwenye jamii.

Hakuna mwenye kuupenda umaskini tatizo ni pale kiongozi anapoufikiria mwenendo mzima wa biashara zake unaoingiliana na biashara za wengine tena kwenye nchi ndogo kama Zanzibar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…