Zanzibar: Yaliyojiri kwenye ziara ya Rais Magufuli kisiwani Pemba - Sept 2016: Ampongeza Jecha kusimamia uchaguzi vizuri

Katiba,katiba,katiba.Nina hakika kama huyu mtawala wa sasa angekuwa rais miaka 10 iliyopita hata hule mchakato wa Katiba usingekuwepo,hii style yake si ya kiongozi ni style ya watawala.
 
"Tanzania tumechezewa mno na kama kuibiwa tumeibiwa mno... Mimi nipo serikalini najua. Kila mahali ni dili! Kila mahali ni dili... Ukigeuka hivi unakuta kuna mahali palikuwa panapigwa dili... Ukigeuka hivi unakuta kuna mahali palikuwa panapigwa dili... Yaani ni dili ni dili tu... Ila naomba niseme kutoka moyoni Tanzania kugeuzwa shamba la bibi sasa basi... Ni lazima iwe mwisho na nasema imetosha!" Mhe Rais Dkt Magufuli.

Hii vita si nyepesi. Tunakuombea na kukuunga mkono Mhe Rais.

[HASHTAG]#ImetoshaKuibiwa[/HASHTAG]
 
Duuuuh hii nchi imeshakuwa ya kujaribiwa
 
.

"Kuna watu wanasema mzunguko wa pesa umepungua na hali imekuwa ngumu, hizo pesa zilizokuwa zinachezewa huko mtaani zilikuwa pesa za serikali. Mimi nataka pesa ziende kwenye miradi ya maendeleo na ndiyo maana bajeti ya maendeleo tumeiongeza kutoka 26% hadi 40% ".

-Mh Rais John Pombe Magufuli , 1st September 2016
 
Najua mmeshachoshwa na vtisho na ahadi hewa kwa watoto maskini,so nini kifanyike ili tuwe na uhuru kwa nchi yetu,coz hii ni nchi ya watu wote na s mmoja,hayo ni madaraka tu ya muda but watu wanashindwa kutumia utu,busara na hekima .hilo ndo tzo kubwa kwa africa,but kwa tz awamu hii imepitiliza bora juzi na hata jana lkn leo imekuwa too much
 
Acha uongo!!

Kura zote zilihesabiwa ila sema ZEC haikuverify kura zote kabla ya kufuta uchaguzi. Kura zinahesabiwa vituoni. Sasa kuna kituo kinahesabu kura zaidi ya siku tatu!?
 
Ndugu watanzania CCM, wapenda maendeleo na TBC kwa ujumla inakukaribisha/kukutaarifu kuwa leo jioni katika kipindi muddaartt kabisa cha "Tunatekeleza" atakuwepo Mh Harrison Mwakyembe waziri wa sheria na katiba kuelezea maendeleo na mipango/mikakati ya wizara yake katika kulipeleka taifa mbele kimaendeleo, kisheria na kuzongatia haki kwa wote.

Itakusaidia sana. Itakungua akili zaidi, hivyo usikose!!!
 
Rais wa JMT Mh Magufuli ametoa kongole zito kwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ZEC kuwa alifanya kazi kwa uadilifu na kwakweli anastahili sifa na tuzo ya heshima kwa kuiweka historia vyema na daima atakumbukwa.

Salim Jecha pokea pongezi kutoka kwa rais na kutoka kwa CCM Tanzania.
[HASHTAG]#hiindiccm[/HASHTAG]
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Magufuli amempa ujumbe mzito kwa Dr Shein kuwa aache upole na awe mkali kuwashughulikia kikamilifu wale wanaoleta mchezo kwa serikali.

Waonyeshe kuwa dola unaiongoza wewe, sio wanaleta chokochoko na waachwe hivyohivyo. Waonyeshe kazi.

[HASHTAG]#hiindioccmyahapakazi[/HASHTAG]
 
TBC hata Mkulu haangaliagi, kipindi hicho wangepeleka clouds
 
Serikali inayoongozwa na CCM chini ya Mh rais magufuli inetoa onyo kali kwa wale wanaodhania wataivuruga amani ya taifa. Jana rais alipokuza ziarani pemba alitoa dhamira nzito kuwa hatowavumilia vibyangarika watakao vuruga amani ya nchi
 
Katiba,katiba,katiba.Nina hakika kama huyu mtawala wa sasa angekuwa rais miaka 10 iliyopita hata hule mchakato wa Katiba usingekuwepo,hii style yake si ya kiongozi ni style ya watawala.
Pasingekuwa na mchakato wa katiba bali pangetokea ubadilishaji wa katiba hususani ibara inayoweka ukomo wa kuwa madarakani! Hata hivyo si kwamba hilo halitafanyika tena, it's a matter of time! Katu sitarajii kuuona ule ukali wa Mkapa pale baadhi ya watu kwa kujipendekeza tu; wakaanza kunong'ona nong'ona kwamba eti katiba ibadilishwe ili Mkapa aendelee! Mkapa akawajia juu mchana kweupe!
 
Ubabe haujawahi saidia chochote katika kuleta umoja, amani na maendeleo kwa wananchi. Hekima na Busara kwenye uongozi vinahitajika zaidi katika dhama hizi. Msije mkapandikiza vitu ambavyo mkizeeka mtakuja juta.
 
Ndugu Wanachadema Mkoa wa Arusha, sisi ni vijana wenye uchungu na chama chetu ndio maana tuko tayari kuipigania hata kuifia ili tupate ukombozi. Ni sisi tulikesha nje ya mahabusu alipowekwa ndani Kamanda Godbless Lema. Alivyoshinda siku tatu bila kula na sisi tulishinda naye bila kula.

Ndugu wanaChadema chama hiki kimejengwa kwa nguvu za umma yani sisi ndio maana CCM imefutika hapa Arusha. Hakipo.
Tuna uchungu sana. Hapa Arusha tumeshapigwa sana na Policcm tukitetea ukombozi. Wenzetu wameshatangulia mbele za haki. Mungu awarehemu. Yote ni kupigania ukombozi.

Ndugu zetu wanaChadema na Watanzania, hivi karibuni Kamati Kuu chini ya Kamanda Mbowe iliazimia tuandamane nchi nzima na mikutano kupinga Udikteta wa Serikali ya maCCM isiyotaka demolrasia, UKUTA ya Sept Mosi.

Vijana wa Arusha tulijiandaa vilivyo kupambana na Policcm endapo wangetuzuia hadi tone la mwisho la damu yetu. Tuko tayari kuifia haki na demokrasia. Dunia nzima ilijua ni siku ya ukombozi Tanzania.

Ndugu wanaChadema tumesikitishwa sana, tumeumizwa sana, tumefedheheshwa sana na kitendo cha Mbowe kwa hiari yake kusitisha maandamano hayo kwa madai eti ameombwa na viongozi wa dini na Lowassa naye ameombwa na familia ya Nyerere tuache kuandamana.

Ndugu wanaChadema, popote mlipo hata nje ya nchi tumechunguza hata kuongea na baadhi ya viongozi wa dini aliowataja Mbowe wamekataa hawakuongea naye hivyo Mbowe ni mwongo. Hata familia ya baba wa Taifa wamekataa hawakuongea chochote kuhusu Ukuta.

Tunatambua heshima ya Lowassa kwa chama. Lakini ni dhahiri Mbowe anamwogopa Lowassa. Lowassa bado ana maslahi binafsi na CCM ndio maana hapendi uharakati ambayo ndiyo asili ya Chadema na chama chochote cha upinzani. Tazameni Garbon.
Lowassa anatuletea siasa za Ccm. Anataka tufanane nao mafisadi. Arudi alikotoka.

Maandalizi ya UKUTA Sept 1 imegharimu chama mamilioni ya shilingi ilhali wilaya kibao hatuna ofisi, tumepanga na tunadaiwa kodi. Nani atarusisha fedha hizi?

Mbowe amelewa madaraka ya Uenyekiti wa Chadema. Sisi vijana kwa umoja wetu tunamtaka Mbowe na Lowassa wakae pembeni ili kamanda Lissu atuongoze. Hatuwezi kubembeleza haki yetu.
Tunamtaka aondoke na Lowassa wake atuachie chama. Kinyume cha hapo tumeamua kujichangisha fedha tutaenda kwa Msajili Dar es salaam atusajili kama CHADEMA-ASILI.

Akiondoka hata leo hatutafikia huko. Tulianza na Mungu tutamaliza na Mungu. Vijana wengine wa mikoa mingine mtuunge mkono kama Singida na Kagera ambao nao Wako mbioni kutoa matamko.

Ahsanteni
John Ole Kaparo
Mwenyekiti wa Muda
Kamati ya Kudai Chadema Asili (KAKUCHA)
 
Ujumbe murua kabisa huo!. Na hizi ndizo busara zilizotukuka za mkuu wetu wa nchi, Mhe. rais, Dr. John Pombe Joseph Magufuli!.
Mwenye masikio na asikie! .
Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…