Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Duuuuh hii nchi imeshakuwa ya kujaribiwaKwa bahati mbaya, jana sikupata fursa ya kufuatilia ziara ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano huko kisiwani Pemba!! Kutokana na hilo, leo nikaamua kuperuzi peruzi hapa JF. Kitu ambacho kimenishitua sana kama sio kunitisha ni kauli ya Mheshimwa Rais JPM aliyomwambia Mheshimiwa Dk. Shein. Hii ndio kauli ya JPM ambayo imenishitua kwa kweli:
Binafsi nashindwa kuamini ikiwa Rais aliyechaguliwa kupitia sanduku la kura, bado anaweza kuwa na kauli kali na ya vitisho namna hiyo!! Sasa ikiwa ni kweli mtu ameshindikana na Mheshimiwa Shein; yeye Mheshimiwa JPM atamfanya nini huyo mtu ndani ya hizo dakika 5?! Hapa lazima niwe na hofu kwavile JPM ni Commanding In Chief na majeshi yote yapo chini yake! Ni wapi tunaelekea kwenye hili taifa?! Mbona ikiwa mambo yenyewe kama ndo haya mbona hayo magereza yenu hayatatosha kufunga "wachochezi"?
Nafahamu wapo wanaofurahia na kushadadia kauli kama hizi huku wakidhani haziwahusu!! Pamoja na yote hayo, mnapaswa kufahamu fika kwamba; wote nyinyi hata kama mna kadi za CCM bado ni vidampa tu mbele ya yule Kingunge Ngombale Mwiru wa CCM!! Hata kama mna kadi tangia enzi za TANU, wote nyinyi ni vidampa tu mbele ya mtu kama Lowassa au Fredrick Sumaye wa enzi za CCM! Na si ajabu, ni vidampa hata mbele ya mtu kama Lawrence Masha aliyepata kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nchi hii!!
Hii maana yake nini? Usidhani vitisho kama hivi wewe havikuhusu kwa sababu tu wewe ni kada wa CCM! Kama ndivyo unavyodhani, basi uelewa wako ni mdogo kupitiliza! Nimewataja hapo akina Kingunge ambao miezi 30 tu iliyopita nao wangedhani kauli za vitisho kama hizo haziwahusu! Je, mtu kama Lowassa ambae hapo kabla angedhani kauli kama hiyo haimuhusu leo anaweza kudiriki kusema hivyo? Who are you ndani ya CCM compared to Kingunge Ngombale Mwiru? Ingawaje Kingunge ametoka CCM; hivi unaamini vigogo kama Mzee Mwinyi au Pius Msekwa anaweza kukuamini kada wewe kuliko Mzee Kingunge?!
Endeleeni kufurahia kauli za vitisho kama hizi lakini kaa mkifahamu hili si la mmoja! Wakati inapitishwa Sheria y Mitandao niliamini kwamba hainihusu kwa kile nilichoamini nikiwa na akili yangu timamu siwezi kuingia online na kuanza kutukana watu, kuanza ku-post picha za utupu n.k! I swear to God, niliamini hainihusu kabisa na hata hapa niliwahi kuandika kwamba "A black cat may be a bad lucky only if you're mouse!" Lakini leo hii hakuna sheria ninayoiogopa kwenye hii nchi kama sheria ya mitandao ambayo, practically imebadilika kutoka kuwa Sheria ya Mitandao to Sheria Ya Kubana Maoni!
Ajabu ni kwamba, utakuta wengi wanaoshabikia kauli kama hizi hapa JF ni vijana wadogo wengine wakiwa below 30. Don't be stupid, you've a very long way to go!! Hilo hilo unaloshabikia leo wakati hata direction ya maisha yako haija-settle ndio hilo hilo litakalokutafuna kesho kwenye harakati zako za kimaisha!
Ikiwa kupinga kauli ya Rais ni UCHOCHEZI, am ready to face consequences lakini kauli hiyo ya Rais haileti picha nzuri kutoka mdomoni mwa Rais aliyechaguliwa kwa sanduku la kura. Haipendezi kutoka mdomoni mwa Commanding In Chief ambae Majeshi ya Ulinzi na Usalama yapo chini yake!
MUNGU IBARIKI TANZANIA.
Acha uongo!!Acha uongo kila mtu anajuaje CUF walishinda wakati kura hazikuhesabiwa zote na tume haikutangaza matokeo? Mtu kujitangazia kuwa ameshinda ndiyo unataka kuaminisha watu kiupotofu kuwa CUF ilishinda? Endelea kuota ndoto bandia ambazo hazitakuja kutimia.
Pasingekuwa na mchakato wa katiba bali pangetokea ubadilishaji wa katiba hususani ibara inayoweka ukomo wa kuwa madarakani! Hata hivyo si kwamba hilo halitafanyika tena, it's a matter of time! Katu sitarajii kuuona ule ukali wa Mkapa pale baadhi ya watu kwa kujipendekeza tu; wakaanza kunong'ona nong'ona kwamba eti katiba ibadilishwe ili Mkapa aendelee! Mkapa akawajia juu mchana kweupe!Katiba,katiba,katiba.Nina hakika kama huyu mtawala wa sasa angekuwa rais miaka 10 iliyopita hata hule mchakato wa Katiba usingekuwepo,hii style yake si ya kiongozi ni style ya watawala.