Zanzibar: Yaliyojiri kwenye ziara ya Rais Magufuli kisiwani Pemba - Sept 2016: Ampongeza Jecha kusimamia uchaguzi vizuri

Zanzibar: Yaliyojiri kwenye ziara ya Rais Magufuli kisiwani Pemba - Sept 2016: Ampongeza Jecha kusimamia uchaguzi vizuri

KWENYE SUALA LA AMAN CNA SWALI ACHA AIWEKEE MSISITIZO ILA KWA JECHA MMMHHHHH.....
 



Anaeongea kwa sasa ni Rais John Magufuli baada ya kukaribishwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Shein na anazungumzia amani. Anasema mtu hawezi kuja kuwekeza Pemba wakati watu hawasalimiani, anasema mume na mke wakiwa hawaelewani kwa sababu ya vyama vya siasa hajui usiku wanalalaje. Amesema anajua vijana wengi hawana ajira Pemba, watapata ajira endapo wawekezaji watakuja kujenga sehemu ambayo ina amani.

Magufuli: Uchaguzi umeshakwisha na utakuja tena 2020, huo ndio ukweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Uchaguzi umekwisha mimi nikachaguliwa kuwa Rais na naitwa John Pome Magufuli na nimefunga Makufuli yote na funguo nimeshatupa.

Nataka niseme Mhe Dk Shein, wewe ndie Rais na inawezekana umekuwa mpole kidogo, huo upole weka pembeni, unasapoti yangu yote, atakaekuchezea chezea niambie hata kwa kuninong'oneza.

Tushirikiane kwa nguvu zote, wanaojaribu kuchezea amani yetu, mimi niliwahi kwenda Libya, mojawapo ya nchi za Afrika zilizokuwa na raha ni mojawapo. Pakajitokeza watu wachache kwa kuahidiwa ahadi za uongo, Libya leo siyo mahali panapokalika, watu wanamwaga damu kila siku, watu walichezea amani, hata amani inalevya.

Rwanda wakati wa genocide walikufa watu wanaokaribia milioni moja, mmenichagua kuwa Rais wenu, nna wajibu wa kuwaeleza ukweli, wanaofanya chokochoko tunawajua wengine, wafatilieni wote wanaochomachoma washughulikiwe wote bila huruma. Mna bahati mna Rais mpole sana na hata sura yake nzuri tu na ni Rais alietoka Pemba, ni kitu gani kinatusumbua.

Mimi nilifanya nae kazi nikiwa naibu waziri na waziri, ninamfajhamu Dk Shein, mpeni ushirikiano. Kuna mtu alijifungia kwenye chumba alafu akasema ametoka Ulaya, msikubali kudanganywa, hivi karibuni alinunua Meli na zinafanya kazi, kuna maeneo mengi yamepelekwa maji na umeme, watu hamtaki kuyaona haya. Palikuwa na Prof Mbarawa hapa mkamkataa jimbo la mkoani(Mkanyageni) mkamkanyagia hukohuko, mimi nnafahamu umuhimu wake na nikachukua wizara tatu nikaziunganisha zote nikampa mtu aliekanyagwa huku.

Mpeni ushirikiano Dk Shein, imebaki miaka minne tu na kitu na kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar hiki ndio kipindi chake cha mwisho. Nawaomba wananchi tujenge umoja wetu. Tukienda kwa umoja wetu tutafanikiwa, tunataka tuimarishe uvuvi, mazao na serikali iliongeza hela kununua karafuu japo pato lake limeanza kushuka, tunataka tujenge hii nchi. Katika kipindi kifupi Pemba itakuwa kama Ulaya na wanaoharibu Pemba ni watu wachache sana.

Wengine wanasema uchaguzi utarudiwa, kwa kawaida ndoto huwa ni usiku lakini hizo ni ndoto za usiku, lakini ukimkuta mtu anaota mchana, huyo anatafuta ukichaa. Nampongeza sana nh Jecha kwa kusimamia uchaguzi na umeenda vizruri sana na kama kuna tuzo mheshimiwa Shein utatoa, Jecha umpe hizo tuzo. Napongeza sana vyombo vya ulinzi, mmefanya kazi nzuri sana, mmesimamia amani ya Tanzania kwa uzalendo mkubwa sana.


=====
Rais John Magufuli atua Pemba muda mfupi uliopita akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli baada ya mapokezi yaliyombatana na kikundi cha ngoma, ameenda kuzulu kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk Omary Ali Juma. Baadaye saa tisa alasiri atafanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa Gombani ya Kale, Pemba.

==========

Kwangu mimi binafsi napongeza juhudi za serikali ya magufuli kusimamia amani kwa nguvu zote, big up mtu wa Mungu,,
 
Tushirikiane kwa nguvu zote, wanaojaribu kuchezea amani yetu, mimi niliwahi kwenda Libya, mojawapo ya nchi za Afrika zilizokuwa na raha ni mojawapo. Pakajitokeza watu wachache kwa kuahidiwa ahadi za uongo, Libya leo siyo mahali panapokalika, watu wanamwaga damu kila siku, watu walichezea amani, hata amani inalevya.
Huko Libya huko .......... hivi hakuna mfano mwingine!!?
 
Hivi kumbe mkulu Natumia air tanzania? Ile iliyonunuliwa na mkwele ikwap

dah Mkwere sijui kawakosea nini!!! hiyo ndege ilinunuliwa na BWM tena tukaambiwa tule majani lakini ndege ya Rais lazima inunuliwe..
 
wakuu! Ni kweli kuwa huyu rais wa zenj ni mpole kama inavyodaia?
 
Akiwa Pemba Rais Magufuli kamwambia Dr. Shein asiogope na kama kuna mtu anafkiri anamshinda basi amwambie haraka maramoja...
 

Attachments

  • 1472829489815.jpg
    1472829489815.jpg
    48.6 KB · Views: 53
Back
Top Bottom