Zanzibar: Yaliyojiri kwenye ziara ya Rais Magufuli kisiwani Pemba - Sept 2016: Ampongeza Jecha kusimamia uchaguzi vizuri

Zanzibar: Yaliyojiri kwenye ziara ya Rais Magufuli kisiwani Pemba - Sept 2016: Ampongeza Jecha kusimamia uchaguzi vizuri

Alikuwa anatania tu kama utani mwingine.
1. Aliwatania watu wa kigamboni wapige mbizi kama hawawezi kulipa nauli ya 200. Kwani walipiga mbizi?
2. Aliwatania watanzania kwa kuwaagiza kufyatua watoto maana sasa elimu ni bure hadi kidato cha nne, kwani wanafyatua?
3.
4.
Wasukuma wana utani mwingi mkuu.
Kweli wana utani
 
NDUGU WATANZANIA CCM, WAPENDA MAENDELEO NA TBC KWA UJUMLA INAKUKARIBISHA/KUKUTAARIFU KUWA LEO JIONI KATIKA KIPENDI MUDDAARTT KABISA CHA "TUNATEKELEZA" ATAKUWEPO MH KARRISON MWAKYEMBE WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA KUELEZEA MAENDELEO NA MIPANGO/MIKAKATI YA WIZARA YAKE KATIKA KULIPELEKA TAIFA MBELE KIMAENDELEO, KISHERIA NA KUZONGATIA HAKI KWA WOTE. ITAKUSAIDIA SANA. ITAKUNGUA AKILI ZAIDI, HIVYO USIKOSE!!!
Mwandiko wako utafikiri darasa la tano
 
Huyu ndio rais tuliyemuhitaji. Watu tulijisahau sana. By the way hivyo sio vitisho, ila inaonesha seriousness ya kusisitiza jambo. Sio kwamba anatishia bali huo ndio ukweli wake na ndio ukweli tunaouhitaji sisi.
 
HII NDIYO SHIDA YA MTU AKIYEOKOTA EMBE DODO CHINI YA MTI WA MWAROBAINI...

OVA
 
Tanzania yateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Siasa, Ulinzi na USalama wa Nchi za SADC
Seebait.com 2016SeeBait

Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali umemalizika katika mjini Mbabane Swaziland ambapo Tanzania imeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi muhimu na nyeti ya Siasa, Ulinzi na USalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika- SADC- (SADC Organ On Politisc, Defence and Security Cooperation) ambapo nchi ya Angola imeteuliwa kuwa Makamu mwenyekiti wa asasi hiyo.

Jukumu kubwa la asasi hiyo litakuwa ni kuangalia masuala yote yanahusiana na Siasa, ulinzi na usalama katika ukanda wa SADC huku changamoto kubwa ikiwa ni namna ya kutafuta suluhu ya kudumu hususani katika eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo- DRC na Lesotho.

Akizungumzia mambo muhimu yaliyojiri kwenye Mkutano huo wa 36 wa SADC mjini Mbabane – Swaziland, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambaye alimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli amesema mkutano huo umekuwa wa mafanikio makubwa na amehimiza ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa nchi wanachama wa SADC kwa sasa zinatakiwa kuongeza juhudi katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na kuzitafutia ufumbuzi haraka kama hatua ya kujenga ustawi bora wa wananchi wa kanda hiyo.

Kuhusu Mpango wa Mfalme wa Swaziland wa III wa kujenga Chuo Kikuu cha SADC nchini mwake kabla ya mkutano ujao wa SADC hapo mwakani chuo ambacho kwa kuanzia kitatoa ufadhili wa masomo ya Sayansi,Ugunduzi na Utafiti kwa wanafunzi wanaotoka kwenye nchi wanachama wa SADC, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema mpango huo ni mzuri na utasaidia kutoa wataalamu wengi hasa wanasayansi katika ukanda wa SADC na serikali ya Tanzania inaunga mkono mkakati huo.

Kuhusu Tanzania kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama kwa nchi za SADC, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Kikanda na Kimataifa Dkt Augustine Mahiga amesema Tanzania itahudumu katika asasi hiyo kwa mwaka MMOJA na anaimani kuwa changamoto za kisiasa zilizopo katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Lesotho zipatiwa ufumbuzi.

Mkutano wa wakuu wa nchi na serikali wa SADC pia umeiteua nchi ya Swaziland kuwa mwenyekiti wa SADC na Jamhuri ya Afrika Kusini imeteuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa SADC.

Katika mkutano huo wakuu wa nchi na serikali wametia saini rasimu za maboresho ya mikataba mbalimbali ya jumuiya hiyo ikiwemo mkataba wa kuboresha itifaki ya SADC dhidi ya rushwa, maboresho ya itifaki ya ushirikiano wa siasa, ulinzi na usalama ya SADC na maboresho ya itifaki ya biashara.

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais
Mbabane
Swaziland
 
watanzania wakati tutakuwa tumeshindwa watu wa kuwakumbuka ni sawa na kusema uanze kuukumbuka muharisho ulioharisha mwaka jana.
 
"Ndugu zangu Watanzania, najua maisha mnayoishi, taabu mnazozipata na matarajio yenu kwangu. Vilio vyenu ninavisikia na ninavifanyia kazi. Lengo langu ni kuwatoa katika UMASIKINI....sitowaangusha"---Rais John Pombe Magufuli.

SHARE TAFADHALI!
 
"Ndugu zangu Watanzania, najua maisha mnayoishi, taabu mnazozipata na matarajio yenu kwangu. Vilio vyenu ninavisikia na ninavifanyia kazi. Lengo langu ni kuwatoa katika UMASIKINI....sitowaangusha"---Rais John Pombe Magufuli.

SHARE TAFADHALI!
Imekaa vizuri
 
"Ndugu zangu Watanzania, najua maisha mnayoishi, taabu mnazozipata na matarajio yenu kwangu. Vilio vyenu ninavisikia na ninavifanyia kazi. Lengo langu ni kuwatoa katika UMASIKINI....sitowaangusha"---Rais John Pombe Magufuli.

SHARE TAFADHALI!
naona leo umepangiwa shift ya asubuhi na unalipwa kwa kila thread,
sasa mimi nitaziunganisha zote kwenye thread 1 ili upate buku saba tu
 

View attachment 392484 View attachment 392485
Anaeongea kwa sasa ni Rais John Magufuli baada ya kukaribishwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Shein na anazungumzia amani. Anasema mtu hawezi kuja kuwekeza Pemba wakati watu hawasalimiani, anasema mume na mke wakiwa hawaelewani kwa sababu ya vyama vya siasa hajui usiku wanalalaje. Amesema anajua vijana wengi hawana ajira Pemba, watapata ajira endapo wawekezaji watakuja kujenga sehemu ambayo ina amani.

Magufuli: Uchaguzi umeshakwisha na utakuja tena 2020, huo ndio ukweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Uchaguzi umekwisha mimi nikachaguliwa kuwa Rais na naitwa John Pome Magufuli na nimefunga Makufuli yote na funguo nimeshatupa.

Nataka niseme Mhe Dk Shein, wewe ndie Rais na inawezekana umekuwa mpole kidogo, huo upole weka pembeni, unasapoti yangu yote, atakaekuchezea chezea niambie hata kwa kuninong'oneza.

Tushirikiane kwa nguvu zote, wanaojaribu kuchezea amani yetu, mimi niliwahi kwenda Libya, mojawapo ya nchi za Afrika zilizokuwa na raha ni mojawapo. Pakajitokeza watu wachache kwa kuahidiwa ahadi za uongo, Libya leo siyo mahali panapokalika, watu wanamwaga damu kila siku, watu walichezea amani, hata amani inalevya.

Rwanda wakati wa genocide walikufa watu wanaokaribia milioni moja, mmenichagua kuwa Rais wenu, nna wajibu wa kuwaeleza ukweli, wanaofanya chokochoko tunawajua wengine, wafatilieni wote wanaochomachoma washughulikiwe wote bila huruma. Mna bahati mna Rais mpole sana na hata sura yake nzuri tu na ni Rais alietoka Pemba, ni kitu gani kinatusumbua.

Mimi nilifanya nae kazi nikiwa naibu waziri na waziri, ninamfajhamu Dk Shein, mpeni ushirikiano. Kuna mtu alijifungia kwenye chumba alafu akasema ametoka Ulaya, msikubali kudanganywa, hivi karibuni alinunua Meli na zinafanya kazi, kuna maeneo mengi yamepelekwa maji na umeme, watu hamtaki kuyaona haya. Palikuwa na Prof Mbarawa hapa mkamkataa jimbo la mkoani(Mkanyageni) mkamkanyagia hukohuko, mimi nnafahamu umuhimu wake na nikachukua wizara tatu nikaziunganisha zote nikampa mtu aliekanyagwa huku.

Mpeni ushirikiano Dk Shein, imebaki miaka minne tu na kitu na kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar hiki ndio kipindi chake cha mwisho. Nawaomba wananchi tujenge umoja wetu. Tukienda kwa umoja wetu tutafanikiwa, tunataka tuimarishe uvuvi, mazao na serikali iliongeza hela kununua karafuu japo pato lake limeanza kushuka, tunataka tujenge hii nchi. Katika kipindi kifupi Pemba itakuwa kama Ulaya na wanaoharibu Pemba ni watu wachache sana.

Wengine wanasema uchaguzi utarudiwa, kwa kawaida ndoto huwa ni usiku lakini hizo ni ndoto za usiku, lakini ukimkuta mtu anaota mchana, huyo anatafuta ukichaa. Nampongeza sana nh Jecha kwa kusimamia uchaguzi na umeenda vizruri sana na kama kuna tuzo mheshimiwa Shein utatoa, Jecha umpe hizo tuzo. Napongeza sana vyombo vya ulinzi, mmefanya kazi nzuri sana, mmesimamia amani ya Tanzania kwa uzalendo mkubwa sana.


=====
Rais John Magufuli atua Pemba muda mfupi uliopita akiwa na mkewe Mama Janeth Magufuli baada ya mapokezi yaliyombatana na kikundi cha ngoma, ameenda kuzulu kaburi la aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk Omary Ali Juma. Baadaye saa tisa alasiri atafanya mkutano wa hadhara katika uwanja wa Gombani ya Kale, Pemba.

==========

Habari zaidi...
Septemba 2, 2016, Rais John Magufuli amefanya ziara ya kikazi ya siku mbili visiwani Zanzibar, baada ya kukaribishwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Shein na akazungumzia amani. Amesema mtu hawezi kuja kuwekeza Pemba wakati watu hawasalimiani, anasema mume na mke wakiwa hawaelewani kwa sababu ya vyama vya siasa hajui usiku wanalalaje. Amesema anajua vijana wengi hawana ajira Pemba, watapata ajira endapo wawekezaji watakuja kujenga sehemu ambayo ina amani.

Magufuli: Uchaguzi umeshakwisha na utakuja tena 2020, huo ndio ukweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Uchaguzi umekwisha mimi nikachaguliwa kuwa Rais na naitwa John Pome Magufuli na nimefunga Makufuli yote na funguo nimeshatupa.

Nataka niseme Mhe Dk Shein, wewe ndie Rais na inawezekana umekuwa mpole kidogo, huo upole weka pembeni, unasapoti yangu yote, atakaekuchezea chezea niambie hata kwa kuninong’oneza.

Tushirikiane kwa nguvu zote, wanaojaribu kuchezea amani yetu, mimi niliwahi kwenda Libya, mojawapo ya nchi za Afrika zilizokuwa na raha ni mojawapo. Pakajitokeza watu wachache kwa kuahidiwa ahadi za uongo, Libya leo siyo mahali panapokalika, watu wanamwaga damu kila siku, watu walichezea amani, hata amani inalevya.

Rwanda wakati wa genocide walikufa watu wanaokaribia milioni moja, mmenichagua kuwa Rais wenu, nna wajibu wa kuwaeleza ukweli, wanaofanya chokochoko tunawajua wengine, wafatilieni wote wanaochomachoma washughulikiwe wote bila huruma. Mna bahati mna Rais mpole sana na hata sura yake nzuri tu na ni Rais alietoka Pemba, ni kitu gani kinatusumbua.

Mimi nilifanya nae kazi nikiwa naibu waziri na waziri, ninamfajhamu Dk Shein, mpeni ushirikiano. Kuna mtu alijifungia kwenye chumba alafu akasema ametoka Ulaya, msikubali kudanganywa, hivi karibuni alinunua Meli na zinafanya kazi, kuna maeneo mengi yamepelekwa maji na umeme, watu hamtaki kuyaona haya. Palikuwa na Prof Mbarawa hapa mkamkataa jimbo la mkoani (Mkanyageni) mkamkanyagia hukohuko, mimi nnafahamu umuhimu wake na nikachukua wizara tatu nikaziunganisha zote nikampa mtu aliekanyagwa huku.

Mpeni ushirikiano Dk Shein, imebaki miaka minne tu na kitu na kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar hiki ndio kipindi chake cha mwisho. Nawaomba wananchi tujenge umoja wetu. Tukienda kwa umoja wetu tutafanikiwa, tunataka tuimarishe uvuvi, mazao na serikali iliongeza hela kununua karafuu japo pato lake limeanza kushuka, tunataka tujenge hii nchi. Katika kipindi kifupi Pemba itakuwa kama Ulaya na wanaoharibu Pemba ni watu wachache sana.

Wengine wanasema uchaguzi utarudiwa, kwa kawaida ndoto huwa ni usiku lakini hizo ni ndoto za usiku, lakini ukimkuta mtu anaota mchana, huyo anatafuta ukichaa. Nampongeza sana Mh. Jecha kwa kusimamia uchaguzi na umeenda vizuri sana na kama kuna tuzo mheshimiwa Shein utatoa, Jecha umpe hizo tuzo. Napongeza sana vyombo vya ulinzi, mmefanya kazi nzuri sana, mmesimamia amani ya Tanzania kwa uzalendo mkubwa sana.

“Dokta Shein una support yangu yote, ukiona umemshindwa mtu, nambie mimi uone kama itapita hata dk 5”
“Wakati tukinadi kwenye kampeni mimi na Shein, tulisema tunataka Tanzania yenye viwanda”
“Hawezi mtu kuja kujenga kiwanda kama kuna vurugu, watu hawasalimiani, hamna amani.”


“Vijana wa Pemba hawana ajira kama walivyo vijana wa bara, kwa hiyo vijana lazima tuwe wa mbele kujenga amani.”
“Na mimi nataka nikwambie Dk. Shein, wewe ndiyo Rais, na naona umekuwa mpole sana,
“Upole uweke pembeni, uwe mkali kidogo, usikubali kuchezewa na mtu,


“Libya ilikuwa nchi ya amani, wakatumiwa watu wachache kwa ahadi za uongo, sasa Libya hakukaliki, watu wanakimbia…”
“Libya watu wanamwaga damu kila siku, kwa sababu watu walichezea amani.”


Mna bahati ndugu zangu, mna rais mpole sana , hata sura yake nzuri tu, Lakini pia ametoka Pemba, mnataka nini!? Mnataka malaika aje aongoze!?

Alisema rais Magufuli.

Hongera rais wetu
 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasihi wananchi wa Kisiwa cha Pemba kutokubali kurubuniwa na watu wanaowachochea kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani kwa kuwa vitendo hivyo vinarudisha nyuma juhudi za kuwaletea maendeleo na kutatua kero zinazowakabili.

Rais Magufuli amesema hayo tarehe 02 Septemba, 2016 wakati akihutubia Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Gombani ya Kale Wilaya ya Chakechake Mkoani Kusini Pemba, ambao umehudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.

Rais Magufuli amesema Kisiwa cha Pemba kina fursa nyingi za maendeleo ikiwemo Uvuvi wa baharini, Utalii na Kilimo lakini endapo wananchi wataendelea kushabikia uchochezi na vitendo vya kuvuruga amani vinavyofanywa na baadhi ya watu, hakuna mwekezaji atakayekuwa tayari kuwekeza.

""Hawezi akaja mtu kujenga kiwanda wakati hakuna amani, sisi vijana lazima tuwe mstari wa mbele kujenga amani ili wawekezaji waje wajenge viwanda na tupate ajira.

"Hapa Pemba kuna fukwe nzuri ambazo zinafaa kujenga hoteli kubwa za kitalii, nani atakuja kujenga hoteli kama hakuna amani?" Amehoji Rais Magufuli huku akisisitiza kuwa umefika wakati kwa wananchi wa Pemba kubadilika na kujikita katika masuala ya maendeleo.

Hata hivyo Rais Magufuli ameonya kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haitawafumbia macho watu wanaofanya uchochezi unaolenga kuvuruga amani na ameviagiza vyombo vya dola vianze kuwafuatilia wote walioanza kufanya uchochezi huo.

Amesisitiza kuwa uchaguzi umekwisha na kilichobaki sasa ni kwa watanzania kufanya kazi na kujenga nchi yao.

Mapema akimkaribisha Rais Magufuli kuzungumza na wananchi hao, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amewaambia wananchi wa Zanzibar kuwa tangu aingie madarakani yeye na Rais Magufuli wamefanya mambo mengi kwa manufaa ya Watanzania

Dkt. Shein ameongeza kuwa hali ya Muungano ni nzuri na kwamba sehemu kubwa ya kero za Muungano zimetatuliwa huku akibainisha kuwa kwa sasa kazi iliyopo ni kutafuta changamoto mpya za Muungano zenye lengo la kuchochea maendeleo.

Mkutano huo umehudhuriwa na Mke wa Rais Magufuli Mama Janeth Magufuli na Mke wa Rais Shein, Mama Mwanamwema Shein, Mawaziri na viongozi mbalimbali wa Siasa, Dini na Serikali.

Jioni hii (jana) Rais Magufuli amewasili mjini Unguja ambapo kesho tarehe 03 Septemba, 2016 ataendelea na ziara yake kwa kuzuru kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Marehemu Sheikh Abeid Amaan Karume, kuzuru kaburi na kutoa mkono wa pole kwa familia ya aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Aboud Jumbe Mwinyi na baadaye atazungumza na wananchi katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika katika Uwanja wa Demokrasia Kibandamaiti Mjini Unguja.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Unguja

02 Septemba, 2016
 
................Nafahamu wapo wanaofurahia na kushadadia kauli kama hizi huku wakidhani haziwahusu!! Pamoja na yote hayo, mnapaswa kufahamu fika kwamba; wote nyinyi hata kama mna kadi za CCM bado ni vidampa tu mbele ya yule Kingunge Ngombale Mwiru wa CCM!! Hata kama mna kadi tangia enzi za TANU, wote nyinyi ni vidampa tu mbele ya mtu kama Lowassa au Fredrick Sumaye wa enzi za CCM! Na si ajabu, ni vidampa hata mbele ya mtu kama Lawrence Masha aliyepata kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nchi hii.
..............................
MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Tulipoamua kukirudisha CCM mikononi mwa unaotuita 'vidampa', hao uliowataja wakatafuta pengine watakapoabudiwa na CHADEMA wakawa wahanga!
upload_2016-9-3_11-26-30.jpeg

 


Jeshi la Polisi Wilaya ya Chakechake, Pemba limezuia kufanyika mkutano na vyombo vya habari wa Chama Cha Wananchi (CUF) uliokuwa umepangwa kufanyika leo wilayani humo, kupisha ziara ya Rais John Magufuli itakayoanza leo.

Rais Magufuli anatarajia kuanza leo ziara yake ya kwanza visiwani humo tangu achaguliwe kuwa Mwenyekiti wa CCM.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Ikulu, Rais Magufuli atazulu Pemba leo na kesho atakuwa Unguja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba, Shekhani Mohamed Shekhani amesema kuwa zuio hilo la mkutano wa CUF ni kwa sababu eneo wanalotarajia kutumia liko jirani na eneo la uwanja atakaokuwa akihutubia Rais Magufuli.

Hata hivyo, Katibu wa CUF wilaya ya Chake Chake, Saleh Nassor Juma alilalamikia maamuzi hayo ya Jeshi la Polisi kwa madai kuwa wao walitaka kufanya mkutano na vyombo vya habari na sio mkutano wa hadhara. Alisema kuwa tayari walishawaeleza Idara ya Habari Maelezo na waliridhia.

Alisema mkutano huo na waandishi wa habari ulilenga katika kutoa tamko lao kuunga mkono uamuzi uliochukuliwa na Baraza Kuu la chama hicho kumsimamisha uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba pamoja na viongozi wengine 10.

“Niliwakatalia kwa hoja kwamba mkutano na waandishi wa habari ni haki yetu ya kikatiba na tulikwishawataarifu watu wa Idara ya Habari Maelezo juu ya kikao hicho halali ambacho wao pamoja na waandishi wa habari walithibitisha kuwa watahudhuria,” alisema Nassor.

Idara ya Habari Maelezo ilithibitisha kuwa walikubali kufanyika kwa mkutano huo wa CUF na vyombo vya habari lakini baadae walipokea taarifa ya kuahirisha kupisha ugeni wa Rais Magufuli.
 
Back
Top Bottom