Zanzibar yatangaza bei mpya za umeme

Zanzibar yatangaza bei mpya za umeme

Halafu Tanganyika wenye umeme wao bei ziko juu balaa na wamekataa kushusha licha ya kukamilika bwawa la Mwl Nyerere.
 
Huku tuliambiwa "haiwezekani" halafu kule inawezekana na hawana source of power; wanachukua huku. RIP JPM
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (Zura), imetangaza bei mpya elekezi kwa watumiaji wote wa umeme kisiwani humo ambapo zitaaza rasmi Januari 20, mwaka huu.
View attachment 3206161
Kwa mujibu wa Zura, ilipokea maombi ya kubadilisha bei za umeme kutoka Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco) kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya matumizi ya umeme Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na Zura leo Januari 18, 2025, bei hizo zimetoa punguzo la Sh190 kwa watumiaji wadogo ambao walikuwa wakilipa Sh480 kwa uniti kila wanapovuka matumizi ya uniti 50 kwa mwezi ambapo kwa sasa watalipa Sh290 badala ya Sh480.

Meneja wa kitengo cha Uhusiano Zura, Mbaraka Haji amesema tozo ya kutoza huduma kwa watumiaji wadogo kuanzia unit 0 hadi 50 itaendelea kuwa Sh2,100 huku bei ya kuungiwa kwa uniti moja ikiongezeka kutoka Sh79 hadi Sh84.

Wateja wenye matumzi ya kawaida wenye matumzi ya uniti moja hadi 1,500 bei ya kuungiwa kwa uniti moja imepanda kutoka Sh266 hadi Sh280 huku kila uniti inayoongezeka ikitoka Sh288 hadi Sh310 na tozo ya kutoa huduma itaendelea kuwa Sh2100.
Wanakula matunda ya Stiglers
 
Back
Top Bottom