Watanzania jamani tunasikitisha. Yaani mwenzao anajaribu kufanya kitu wengine wanamuona anapenda sifa. Acheni hili linchi liwe na watu masikini manake wananchi wenyewe tuna akili za kimaskini. Hivi mtu awe anananzisha online tv, pay tv, tv channel kwani tatizo lipo wapi? Mchawi aliyeliroga hili taifa sijui kafia wapi manake katuacha watu na husuda zetu.
Big up Diamond, achana na maneno ya wakatisha tamaa wasiopenda kuwaona wenzao wanafanya chochote na wakiona lazima wakitoe kasoro manake hiyo ndo ada yetu. Hata humu majumbani mwetu unakuta mtu ana uwezo wa kumtoa mwenzake kimaisha lakini hafanyi hivyo kwa kuwa anataka kila siku uwe kama jana. Furaha yangu ni kuona wasanii wetu wakifanya mambo mengi zaidi na kama ataanza na Online TV basi baada ya muda aangalie uwezekano wa kuanzisha tv channel za kawaida hata kama ni kwa ubia badala ya kumuona eti anapenda sifa. Na kama anafanya hivyo kwa kupenda sifa bado siwezi kumdhihaki. Swali kwa wale wanaomponda. Je, ni wangapi miongoni mwenu wenye huo uwezo? Au hamtaki kwa kuwa mtaonekana mnapenda sifa?