Zawadi Toka Ikulu

Zawadi Toka Ikulu

21.
Ilinibidi kubadilisha mikao kwanza mana sasa nilikuwa naongea na serikali, kwani ni mtoto wa rais namzungumzia mwana wa mtawala wa taifa hili, namaanisha mwana wa mkuu wanchi hii daah!. Kwa tafsiri nyepesi ni mtawala wa watoto pia katika nchi hii ana sauti kuliko spika za tamasha la mziki.

Nilianza kutetemeka ghafula maana sikuwa na amani tena moyoni mwangu, sikuwa najiamini tena niliona matatizo nayatafuta tena kwa miguu miwili. Tukiachana tu na kile cheo chake cha Urais cha baba yake, kiongozi wetu ana maamzi magumu kuliko hata chuma cha pua, ni mkali zaidi ya moto wa gesi, ukimchokoza hana huruma kama tanulu la tofali.



Ila uzuri nikwamba taarifa hutufikia sisi wananchi juu ya yale anayoyaamua kwa watu wanaokwenda kinyume na matakwa yake, kwani anastaili zake za kuwanyoosha wale wanaomchokoza. Chakushangaza zaidi nilijiona na mimi nilikuwa nimejiandaa kumchokoza, nilikuwa namtafuta ugomvi, nikama nimeamua kushusha mbendera ya taifa iliyo katikati ya kambi ya jeshi tena mchana kweupe.



Nilijiona ninagonga geti la ikulu huku nimelewa na nikitoa matusi machafu najua unakijua kitakachofuata. Bado niliona nnachotaka kukifanya ni kuweka kiganja cha mkono kwenye domo la nguruwe mwenye njaa kali na kitakachotokea ninakijua.



Niligundua nilichokuwa nakifanya ni sawa na kukwea mnazi ukweni huku nimefungamsuli na ndani pakiwa patupu kitakachotokea ni fasihi simulizi itakayodumu milele na milele.

Ulifuata ukimya na ulikuwa ni ukimya wa kustajabisha, wakati nikiyawaza hayo kumbe Jesca alikuwa akinisemesha kwa muda, sikumsikia nilikuwa mbali kimawazo, maana tayari ameesha iharibu kabisa siku yangu. Ninampenda Jesca wangu lakini naanzaje kumueleza hilo?. Mtoto wa Rais sistahili hata kukigusa kiganja cha mkono wake, hivi itakuwaje nikimwambia harafu akakataana kunikasirikia si nitafia jela mimi?. Hudhuni majonzi na kukata tama kulitanda moyoni, mawazo yangu yote yalijikita upande hasi,. Niliwaza tena au akikubali harafu yule mzee akajua itakuwaje?. Jamie we Jamie. Umekuwaje . Hivi unanisikia kweli?.. sikuwa nasikia muda wote huo Jesca alioniita sana na sasa aliamua kuja kunigusa nikashituka kama mtu aliyekuwa usingizini. Jesca alikuja karibu yangu akaketi huku akinipapasa shavuni aliniuliza vipi unaumwa?.... mbona umekuwa hivi ghafla jamani? duh! mikono laini iliusisimua mwili wangu na kujikuta naishiwa nguvu, lakini sauti laini nyembembe na tamu ikaiburudisha nafsi yangu.



Nilihisi nabembelezwa mimi, nilihisi kudeka kwa muda kitu ambacho nimekuwa sikipati kwa muda penzini, nilikuwa nikiisikia sauti yake juu ya kifua change ikiniburudisha, natamani awe wangu natamani sana, nilijihisi niko peponi.



Lakini nilipomkumbuka Mh. Rais na heka heka zake sikuwa na chakumjibu nilinyanyuka na kuamua kuondoka kabisa nikitembea kwa mwendo wa unyonge usiyoweza kuelezeka.



Kwa kifupi nilikuwa nimevurugwa, niliufungua mlango na kutoka nje nilikutana na wasichana wawili warembo waliovalia vizuri suti za kijivu na miwani myeusi. Walionekana si watu wa kawaida kimuonekano tu. Bila shaka walikuwa ni walinzi wa Jesca, sasa naanza kupata picha halisi na nilianza kuyaamini macho na masikio yangu.
 
22.


Jesca kweli alikuwa mtoto wa Rais hakukuwa na swali zaidi maana nimejionea kwa macho, mbali na kusikia kwa masikio yangu akinieleza kwa kinywa chake. Niliingia ndani ya lifti nikiwa mwenye mawazo kwelikweli niliwakuta watu wawili kijana na mzee ndani ya lift nikaungana nao bila kusemeshana na mwisho walishuka nami nikashuka. Sikujua kumbe ilikuwa gorofa ya nane, niligutuka kumbe sijabonyeza namba ya wapi ninaelekea nilirudi ndani ya lift na kubonyeza herufi G iliyoniruhusu kwenda mpaka chini nilishuka nikiwa mwingi wa mawazo mana Togwa limetiwa nzi.



Nilielekea upande wa kulia jirani na Mwanza hoteli ndipo nakutana na rafiki yangu mpendwa ni dreva tax wa siku nyingi Thomas James jina la kazi wanamuita Gwaba. Gwaba aliponiona tu kama kawaida yake ni kulia hali mbaya. aah! Jamie fanya hata buku tano boss wangu mdogo wako hapa hali mbaya, tenki kavu sijanywa hata chai, mdogo wako, fanyafanya bwana kiungwana tu si unajua tena. Huwezi amini leo nimepiga bundi gizani. Gwaba ni rafiki yangu anapenda sana kutumia maneno ya mtaani hivyo kumuelewa inakuwa ngumu kwa mtu asiyemjua akikwambia kapiga bundi gizani anamaanisha kakesha patupu yaani hajapata wateja usiku mzima.



Na akisema tenki kavu anamaanisha ananjaa yani tumboni hakuna kitu. Nilimsogelea Gwaba nikionekana mwenye mawazo hata alichonieleza sikushughulika nacho ingawa nilisikia kila sentensi tena neon kwa neno, hivyo sikumjali kabisa nilipozidi kukaribia hata yeye alijua leo Jamie hayuko sawa.



Maana ni kijana aliyekuwa na mimi kwa muda mrefu kwanza tumefahamiana toka nasoma kipindi hicho alikuwa anapiga debe standi kuu ya Igoma, pili tangu nimeanza kazi hapo NSSF Plaza amekuwa akinisaidia safari za hapa na pale hasa kile kipindi ambacho nilikuwa sijanunua usafiri wangu, hivyo Gwaba ananijua vizuri sana. Alinifungulia mlango nikaingia na kuketi kisha nilimwambia anipeleke nyumbani sikuwa nahitaji bugudha maana akili yangu haikuwa sawa.



Basi tuliondoka kuelekea nyumbani kwangu Busweru, nilihitaji utulivu nikiwa kwenye gari maana nilikuwa nimechanganyikiwa, lakini haikuwa hivyo kwa upande wa Gwaba. Gwaba ni msumbufu sana mana anapenda kuongea ni mchangamfu kupita kiasi. Utamfurahia ukiwa sawa ila ukiwa unahitaji utulivu basi Gwaba si mtu sahihi maa atakuchosha.



Alikuwa akiongea njia nzima na ukimkalia kimya ni sawa na bure tu maana maana atakukomalia mpaka umpe ushirikiano utasikia Jamie mwaka kesho nitanunua gari yangu tena itakuwa kali sana, warembo watanikoma na nina mpango wakuagiza Nissan Murano, au hela ikipungua basi nitachukua kama ile yako Toyota mark X”. Hapo mfukoni hana hata mia katoka kunipiga mzinga wa buku tano lakini ndo maisha ya vijana na ndoto kubwa huku mfukoni hakuna kitu. na hana hata akiba ya senti hamsini na ana ndoto yakumiliki gari mwakani sikutaka kutukana niliendelea kukaa kimya.



Si hilo tu njiani nako kila dereva anajuana naye, yaani ni kero kwa kwenda mbele. Mara asimame kusalimiana na watu, ilihitaji uvumilivu sana kumzoea Gwaba hasa akiwa amekunywa kidogo aah! Unaweza mwambia nishushe nitembee.
 
23.


Nilivumilia hizo kashikashi nikitajiwa kila aina ya gari na bei yake mengine ndo marayangu yakwanza kuyasikia. Thomas Gwaba anawajua matajiri wote wenye magari mazuri na ya thamani kubwa hapa mjini na mikoa ya jirani. Hapa nishahadithiwa mpaka nimechukia lakini sikuwa na jinsi nilivumila na baada ya dakika ishirini na tano tayari nilikuwa nyumbani kwangu niulipumua na kumshukuru Mungu ngoja niepukane na hii kero.



Nilishuka na kumlipa Gwaba akaondoka huku nikipiga ishara ya msalaba kumshukuru Mungu acha nikapumzike. Nilijikokota mpaka mlangoni kwangu ili nikajipumzishe. Niliingiza mkono mfukoni kutoa funguo za nyumba nakutana na funguo za gari, nilishituka maana kumbukumbu ilinirudia haraka kuwa gari nimeiacha supermarket, ilinibidi nijicheke kwanza.







Nilijiona mpumbavu, na mwenda wazimu kabisa mana kwa hali ya kawaida mtu huwezi ukasahau gari tena sehemu hatari kama ile na kwa muda wote huo wote zaidi ya masaa manne.



Ilinibidi nimpigie simu Gwaba arudi, nilimbembeleza maana sikuwa na jinsi ilinibidi tena kutumia usafiri wake maana sikuwa na namna kama kawaida kelele zake sasa zilikuwa za chura hazikunitisha. Nilirudi mpaka jengo la CCM mkoa nikaikuta gari yangu ikiwa imeegeshwa palepale nilipoiacha nashukuru ilikuwa salama niliichukua na kurudi nyumbani.



Nikiwa barabarani nilijitahidi kuwa makini maana akili yangu haikuwa sawa hivyo nilichukua tahadhari mapema ili nisisababishe ajali. Baada ya kufika niliingia chumbani kwangu kujipumzisha maana nilikuwa nimechoka na pia nilizongwa na mawazo kichwani mwangu na kusababisha kichwa kiume. Siwezi kuuficha ukweli nilikuwa nampenda Jesca lakini kikwazo ni kimoja tu cheo cha baba yake, niliwaza na kuwazua lakini sikupata jibu jepesi niliamua kulala kwakuwa nilikuwa nimechoka haikuwa taabu kuupata usingizi maana ulinichukua ndani ya dakika kadhaa.



Najaribu bahati yangu ya kukutana na mrembo Jesca kwa mara nyingine ananichukuwa na kunipeleka sehemu ambayo sikuifahamu, nakaribishwa ndani ya jengo kubwa la kifahari niliingia mpaka ndani na kuketi, ni jumba la kifahari na ni fahari kweli. Wafanyakazi wa kila aina walikuwa wakizunguka huku na kule wengine walipita na chupa ndefu na nzuri za mnvinyo wa kila aina.



Baada ya kujipumzisha kwa mda nililetewa glass yenye muonekano nadhifu ilivutia ni ya mnvinyo. Alikuwa ni mhudumu mmoja wa kiume aliyevalia shati jeupe, shingoni kafunga tai ya kipepeo nyeusi, suruali nyeusi na kiatu kizuri cha moka. Nilivutiwa na muonekano wake kweli kijana alivutia sana, nilitia glass mdomoni nikapiga funda moja nilibaki naitafakari ile radha hakika nilijiona niko peponi. Katika maisha yangu ndiyo kwa mara ya kwanza nakutana na kinywaji chenye ladha nzuri kiasi kile ni ladha tamu na harufu nzuri nilii penda sana.



Nikiwa naendelea kupata mvinyo pale sebuleni nilikuwa nimeketi mwenyewe hakukuwa na mtu katu, aliyeshughulika na uwepo wangu, maana kila mtu alikuwa bize na shughuli zake kwenye hilo jumba la kifahari. Walizunguka huku na kule wakifanya shughulizao.
 
24.
Kuna wengine walipita na kunisalimia “habari mheshimwa” ndo salamu iliyotumika mle ndani nadhani kwa kila mgeni aliyekanyaga jumba lile japo sikuwa na uhakika leo na mimi kabwela naitwa mheshimiwa? Dah kweli tembea na uaridi upate bahati ya kunukia , nilijibu nzuri. Sikuwa na amani muda wote ule niliokaa pale sebuleni maana hapakuwa pa hadhi yangu kiukweli palikuwa na hadhi ya juu sana kuliko maisha ya kawaida.

Mapambo yaliyokuwa ndani ya lile jumba sikuwahi kuyaota wala kukutananayo katika maisha yangu yote. Nimehudhuria harusi nyingi za kifahari na zingine kuangalia kwenye muvi mbwembwe za wapambaji wale kwa kifupi hazitafua dafu ndani ya ule mjengo nikisema mapambo ya kifahari ni ufahari kweli. Basi mwenzenu mtoto wa kisukuma niliudhihilisha ushamba tutaniwao na watoto wa Dar-es salaam kila siku “msukuma mshamba a.k.a Ngosha”.



Baada ya kuniacha kwa muda sasa Jesca anarejea akiwa kapendeza zaidi niliongozana naye wakati tunakuja akaniacha hapa sebuleni sikujua alipokuwa na sasa karejea alikuwa kapendeza zaidi. Nilimpokea na kumkumbatia kisha mfanyakazi mmoja alituonesha kwa ishara sehemu tuliyopaswa kwenda.



Tuliongozana huku tukiwa na tabasamu mwanana, usoni na rohoni ingawa sikujua ninapelekwa wapi lakini imani yangu ilinipa furaha nikijua itakuwa sehemu salama na nzuri kuliko hapa. Basi tulitumia dakika kadhaa mpaka kufika tulikokuwa tunaenda ni mwendo kama wa dakika saba tulitembea ingawa ni mwendo wa kawaida lakini huwezi amini tulikuwa bado tuko ndani ya lile jumba la kifahari.



Mazingira tuliyopita yalivutia zaidi kuliko ya awali na kunifanya nitamani kusonga mbele zaidi. Mkono wangu ukiwa umekishika vyema kiuno cha mtoto Jesca nilijiona mfalme ndani ya jumba la kifalme, nilihisi dunia yote sasa iko mikononi mwangu.



Tulizidi kupiga hatua na kuufikia uwazi ambao pia ulizungukwa na majengo ya kifahali, lilikuwa ni eneo la wazi tulivu lililozungukwa na viyoyozi na kulikuwa na bwawa kubwa la kuogelea. Basi yule kijana alitukaribisha kwenye meza moja iliyokuwa na chupa ya mvinyo alivuta kiti huku akiinama na kuweka mkono wake kifuani ishara ya heshima kwetu, Jesca aliketi kwa utaratibu huohuo alikuja upande wangu pia nikaketi.



Alimimina kinywaji nusu glass na kunikabidhi kisha akafanya hivyo kwa Jesca na mwisho alitukaribisha kwa heshima tukagonga glass na kuendelea. Jesca alionesha ishara ya kumuomba atupishe kwa kichwa hali hii iliashilia tulikuwa na faragha, kijana alitii kwa kuinama huku mkono ukiwa kifuani kisha akageuka na kuondoka.



Jesca alinikaribisha kwa upendo tulikunywa mvinyo, tulitaniana, tukacheka na kufurahi. Basi kadri muda ulivyozidi kwenda mambo yalizidi kunoga kwakuwa ilikuwa giza tulijikuta tukijisahau na kujiachia zaidi pale nje tulibusu mara kadhaa na baadae tukajisahau kabisa kana kwamba ni wapenzi wa muda mrefu. Jesca anaonekana amelegea zaidi na alitamani niwekaribu yake zaidi hali hiyo ilisababisha tukajikuta tumekumbatiana na ndimi zetu zilikuwa vinywani huku tukikumbatiana kwa mahaba mazito.
 
25.
Staki kueleza juu ya miguno na kazi ya mikono bali ni kupagawa na hisia za mahaba wote tunaonekana kuzidiwa huku Jesca jicho limemlegea lilionekana kama nusu mwezi, anaonekana kuwa fundi zaidi yangu mpaka nikajiuliza mtoto wa Ikulu kajifunzia wapi hivi vitu?. Kiukweli staki kueleza kilichotokea ila Ilikuwa ni zaidi ya raha.



Baada ya mambo kuwa mambo Jesca aliomba tutoke eneo lile na sasa alinishika mkono tukapandisha ngazi na kuifikia lifuti iliyotupeleka golofa ya kwanza tulitoka huku tukiwa tumeshikana mikono mpaka kwenye chumba kimoja alichokifungua na kunivutia ndani.



Alinibana kwenye ukuta na kuanza kubusu na kutomasana ilikuwa ni kutupa nguo bila mpangilio. Na hatimaye nilimurusha juu ya kitanda kizuri kilichotandikwa kwa ustadi na manjonjo ya kila aina. Mashuka meupe yenye mvuto wa ajabu yalivutia kuyatizama,blanketi na mito mizuri laini ya thamani ilikipamba kitanda kile. Ukiniuliza lilikuwa ni godoro la aina gani stakujibu nitakwambia nililala kwenye kitanda maridhawa kuwahi kutokea duniani, kiukweli kile kitanda ni kitanda kizuri hakuna mfano, godoro laini lakunesanesa, nilihisi niko peponi.



Marashi ya chumbani yalizivutia pua zangu na kunifanya nihisi niko mbinguni, kiukweli kitanda kile kinasahaulisha uwepo wa shida katika ulimwengu huu, nahapo ndipo nilijiuliza kama hiki ni kitanda cha mtoto cha baba kikoje? “Haki ya Mungu ndo maana watu hawataki kuachia madaraka Afrika” nilijisemea kimoyomoyo.



Basi ukawa ni utani juu ya kitanda kukimbizana na kurushiana mito wakati mwingine tulishuka na kuizunguka ile nyumba kwa furaha. “Hakika sihitaji mke zaidi ya huyu katika maisha yangu” nilijisemea. Nilijiona nimechelewa kumjua, nilijuta kutokumueleza mapema kuwa nampenda pengine hizi raha ningeanza kuzipata mapema zaidi ya hapa.



Hisia zilionekana kumuelemea Jesca akiwa kajilaza juu ya kifua changu huku akipumua kwa hisia kali, nilikuwa nikizidi kumbembeleza kwa maneno matamu ili kuufurahisha moyo wake. Jesca ndiye msichana niliyemchagua, ndiye mpenzi wangu wa pekee, nilikuwa najiona kidume na mwanaume aliyekamilika, nilijiona mwanaume pekee mwenye bahati katika dunia hii, leo hatimaye nafanikiwa kuwanaye huyu mrembo katika kitandana cha kifahari ndani ya jumba la Kitawala la Ikulu.



Tukiwa tumelala Jesca kakiweka kichwa chake juu ya kifua changu, tulianza mazungumzo juu ya mahusiano yetu. Tuliaongea mengi sana nilimuuliza Jesca itakuwaje iwapo Rais angejua juu ya mahusiano ya mwanaye? Jesca aliniambia Rais ni mtu muelewa na anamheshimu mwanaye kuliko kawaida na pia anampenda sana hivyo atamsikiliza maana ndiye mwanaye wakike pekee. Pia kama hato elewa basi mama yake Jesca angeingilia kati swala hilo na lingeisha. Kwa upande wake hakuliona kama ni tatizo alinisihi nisiogope. “Nakupenda sana Jamie handsome wangu inakuwaje unakuwa na mashaka juu yangu, mambo ya familia yangu niachie mimi” ni maneno mazuri ya kunifariji yalivutia kuyasikia na pia yalitia moyo.



Jesca aliendelea kunipa faraja kuwa hakuna mtu wakumuamulia ampende nani katika maisha yake, pia akasema hali ya mtu huamliwa na Mungu, hakuna mwanadamu apangaye juu ya maisha yake isipo kuwa muumba peke yake. Jesca alizidi kunifariji sana na kunitia moyo kuwa nisiwe na uoga kwani kila lipangwalo na Mungu hakika hakuna binadamu wakulipangua ni maneno ya faraja yaliyonifanya nijione nimezaliwa upya ndani ya hilo jumba la kifalme. Basi baada ya hayo maneno matamu tuliendelea kuliwadhana juu ya kitanda chetu tulichokichagua kwa siku hiyo natamani ungetuona bila shaka ungetamani kuwa wewe mana furaha ilitawala nyuso zetu.



Hii ilikuwa ni siku niliyoitamani toka siku ya kwanza nakutana na Jesca na leo niko naye kwa karibu zaidi, niko naye katika kitanda kimoja, niko naye tukiwa watupu, nilikuwa nikiutafakari uzuri wake na siupatii picha, ngozi yake laini kila nilipoitomasa ilinitia hamasa, staki kukizungumzia kifua chake kilicho umbwa kikaumbika, Jesca ni binti mwenye mikono laini yenye mbinu katika mapenzi.

JE HUU NI MWISHO???
ITAENDELEA
 
26.
Ufundi wake wa mchezo wa kichokozi ulizidi kunipagawisha na kunifanya nizidi kumpenda zaidi huyu mwana wa Ikulu, tabasamu na kicheko chake vilinifurahisha maradufu kila nilipo kisikia kicheko na kuliona hilo tabasamu maridhawa nilizidi kuwa teja wa mahaba, ni mwana wa Ikulu muite Jesca Jones Manguli na sasa naweza kusema ulikuwa ni muda muafaka wa mimi na Jesca kulianza penzi letu rasmi.



Siwezi kukisema kilicho endelea ninachokikumbuka ni mlango kugongwa kwa nguvu tena ilikuwa ni nguvu na siyo masihara. Kelele za mlango zinatukurupusha na kubaki njia panda baada ya Jesca kusema huyo lazima atakuwa baba yake basi tulianza kulaumiana tukitupiana maneno huku nisijue pakukimbilia. Nilikuwa nikilia huku namlaumu Jesca kwanini kanileta Ikulu mimi mwana wa masikini, maana sasa nilikuwa sijui itakuwaje iwapo nitaangukia mikononi mwa Rais.



Nilikuwa nikisali kila aina ya sala huku machozi yakinitiririka naweza kusema ni muda mfupi sana lakini niliomba mamia ya sala ambayo ukiniambia nirudie hata tatu siwezi kukumbuka. Kweli binadamu akikwama ndipo huukumbuka uwepo wa Mungu, haijalishi ni mpagani kiasi gani, huwa pia haijalishi kakwama katika tatizo gani.



Hatimaye Jesica alipata wazo alinichukua na kwenda kunificha ndani ya kabati la nguo zake, kabati lilikuwa kubwa limepangwa vizuri, nilijificha huku nikizidi kusali sala zote nilizozijua.



Basi rais aliingia na walinzi wake huku nikiwa nachungulia kwenye kitundu kidogo cha mlango waliangaza huku na kule hawakuona mtu. Basi wakaamua kutoka lakini kabla hawajatoka mmoja aliona kiatu cha kiume kikiwa karibu na kitanda aliwaita wenzake wakarudi.



Nilijua nimekwisha, na sasa nilianza kulia kwa uchungu nikimlaumu huyu mwanamke, naapa sikuwahi kulia hivyo hapo kabla tangu nizaliwe. Walirudi wakaangaza mle chumbani hawakuona mtu, kuanzia chooni, sebuleni na sasa walisimama mbele ya malango wa kabati nililojificha na mlango ukatikiswa.







Walianza kuhangaika kuuvunja mlango wa kabati lakini walishindwa na sasa waliamua kufuata nyundo ili waje kuuondoa kabisa, waligonga kwa nguvu ule mlango na hapo ndipo nilikurupuka kutoka usingizini nikiwa nimetweta kwa jasho huku nikipumua kwa hofu. Nilikuwa nahema juujuu kama nimenusurika kukata roho, nilikuwa nameza mate kwa shida huku koo limenikauka.



Wakati huohuo mlango wangu ulikuwa ukigongwa bila shaka kelele hizo ndizo zilizoniamsha. Niliamka kwa unyonge kuelekea mlangoni nilifungua nikakutana na Dominic. Nilimkaribisha ndani na tukaketi, Dominic alinishangaa mana sikuwa kwenye hali yangu ya kawaida, nilikuwa nimelowa jasho mwili mzima huku nahema juuju, alijitahidi kunihoji ili ajue ni nini kinanisibu kulingana na hali niliyokuwanayo, sikuwa na budi kumueleza kila lililonisibu maana nilikuwa natafuta suruhu na mtu pekee awezaye kunipa suruhu walau nikaridhika ni Dominic rafiki yangu kipenzi.
 
27.


Nilimhadithisia Dominic, kuanzia nilipomuacha pale hotelini kwa lengo la kwenda kumtafuta Jesca na nikafanikiwa kumpata nikaenda naye mpaka hotelini alipofikia tukakaa na kuongea lakini tumeshindwana. Dominic alishitushwa na kauli ile alitaka kujua kwanini tumeshindwana, nilimueleza yule mwanamke siyo wa hadhi yangu.



Kila nilicho mueleza kiliibua swali alijenga maswali alihoji kwanini asiwe wa hadhi yangu? Nikahaba?, nitajiri kuliko familia yako?, au hajiheshimu?. Nilimwambia Dominic anaweza kujiuliza maswali mengi ila kuna moja ambalo ni gumu kulitambua na hajalihusisha kweny maswali yake. “Dominic hivi ikitokea ukapendwa na mtoto wa Rais, tena Rais huyu tuliyenaye kwasasa Mzee jones Manguli utafanyaje?” niliuliza kama mtego. “Aaah! itategemea kama kweli binti yake kanipenda naweza kukomaa ila kwa tahadhali sana mana huyo mzee mwenyewe hasomeki unaweza kujikuta unaozea segelea” Alijibu kwa uoga uoga bila kujiamini. “lakini Jamie hizo ndoto zimeanza lini?” alihoji huku.

Nilimuuliza ndoto gani “ hizo za kuota wewe unatoka kimapenzi na mtoto wa Rais mpaka uniulize?” aliniuliza. “Kaka siyo ndoto Jesca ni mtoto wa Rais” nilimjibu kwa upole. Kauli ile ilimfanya acheke sana mpaka alianguka chini huku machozi yakimtoka.



Nilihisi ameanza kuleta uchuro ni kama anageuka kuwa mnafiki, basi nilikaa kimya sikutaka kuongea nae tena. Basi mwenyewe akacheeka mpaka basi najua hajui, ndiyo maana anacheka, hatimaye alilidhika baada ya kucheka kwa muda aliohisi unamtosha “Jamie na ujanja wako wa mjini wote, yaani ujuaji wote bado unadanganywa na hivi vitoto vya mjini? Kaka watoto wa Rais wote nawajua na hawawezi wakawa wanaishi hapa nchini, kile ni kitoto cha kabwela mwenzetu mmoja hapa town kinakuzingua hebu fungua kichwa utatapeliwa ndugu yangu”.



Dominic kwa kifupi alikuwa ameesha nikera alitakiwa anisikilize kwanza lakini haikuwa hivyo, badala ya kutafuta suruhu sasa anaanza kunikejeli na kunidharau.

Basi nilijitahidi kumuelewesha juu ya ushahidi nilionao ili aamini lakini hakutaka kusikia na badala yake aliendelea kunisakama kwa maneno ya kejeli na dharau na kunikatisha tamaa. Na chaajabu zaidi alikuwa akinitolea maneno ya dhihaka kana kwamba mimi siwezi kujisimamia. “Jamie wanawake watakufanya bwege mpaka lini kaka, amka mdogo wangu amka, usiwe mpumbavu, kumbuka Maria alivyokutesa mpaka sasa unahangaika kujinasua mtegoni, alisha kugeuza ATM yake. Leo tena hiki kikalagosi nacho kinataka kukugeuza mtelemko aah! Hapana jiangalie ndugu yangu” nilimsikiliza kwa makini nikayapima maneno yake yenye kejeli ndani yake, maana haikuwa tabia yake kunivunjia heshima sasa niliona anavuka mpaka. Nilimpenda sana rafiki yangu tunapendana na tunajuana toka kitambo alipo yeye mimi nipo na nilipo mimi yeye yupo pia.
 
28.
Dominic, alikuwa akizidi kuongea maneno ya kijinga yaliyonifanya nizidi kujaa sumu, lakini yeye hakuwa anajua kuwa nilikuwa nimekasirika kupita kiasi. “haya baba endelea kumwamini huyo mtoto wa Rais huenda mkapewa zawadi ya bombardier siku ya harusi yenu”. Hakuishia hapo aliendelea “Jamani mijitu mingine sijui huwa haijiulizi umetoka kwenye maisha ya dhiki bado unakubali kuendeshwa na wanawake kama gali bovu unapelekwa tuuu!, wewe niwakwenda tu, kushoto kulia, nyuma mbele. Sikia kama huwezi kuamua tushirikishe wenye maamzi huenda tukakusaidia”. Nilijitahidi kuzikusanya hasira lakini kwa bahati mbaya hazikutosha nilishusha pumzi na kuanza kuikusanya amani moyoni mwangu nilitumia dakika kama mbili kwa kiwango kilichohitajika hakika ilinitosha nilikaa kimya na ikawa kimya kweli.



Nilirudi nyuma na kuketi juu ya sofa nikaendelea kumsikiliza Dominic kwa makini, basi aliongea kila aina ya neno. Alitukana kila tusi alilohisi linanifaa, sijui mbwa asiye ng’ata kwangu sawa tu, mara aliniita nyuki wa mashineni mla unga asiyeng’ata mimi kimya, mara aliniita ATM, kwangu sawa tu, kiukweli tukiacha unafiki yale maneno yalikuwa yanaumiza sana na nilijikaza sana kuyavumilia.

Nadhani urafiki ni kusaidiana, kujengana na kushauriana, siwezi kumsema kwa mabaya Dominic maana ni rafiki yangu wa kitambo sana ila leo ninamuona mpya na ni mtu tofauti kabisa. Siyo Dominic Martine niliyemjua leo nakutana na Dominic Martine tofauti kabisa.



Kulingana na hali aliyonikuta nayo nilidhani atakuwa msaada kwangu na sasa kageuka kuwa karaha na kero kubwa kwangu. Moyo wa mtu ni pango huwezi jua umehifadhi nini ndani yake mpaka uingie ndani yake, bado nampenda Rafiki yangu hivyo nilijitahidi sana kuwa mwema na ndiyo maana pamoja na yote aliyoniambia bado nilijikaza na kuyavumilia huku nikizidi kuwa mtu mwema kwake.



Nilikuwa nimejaa hasira mpaka natweta kwa jasho, “Dominic, nimekuelewa brother nashukuru kwa ushauri wako nitafanyia kazi, sawa ndugu yangu?, ila kwasasa naomba uniache nipumzike” nilianza kutafuta njia yakumuondoa nyumbani kwangu maana nimechoshwa na kelele zake. Bado hakulidhishwa na kauli yangu “aaah! Kweli mapenzi yananguvu kuliko sumaku, leo Jamie niwakunifukuza mimi nyumbani kwako?, sababu ya yule kahaba wako anayejiita mtoto wa Rais? Ila sishangai maana nchi hii tuna marais wengi huenda ni mtoto wa Rais wa masharobaro, au Rais wa TFF huenda ni Rais wa chama cha riadha au Rais wa Monduli maana kila mtu ni Rais siku hizi.



Nashukuru bwana, mkwe mtarajiwa wa Rais mi naondoka zangu, naisubiri hiyo zawadi ya Hummer siku ya harusi yenu wewe na princes Jesca usinisahau bwana kwenye ufalme wako mi nitaridhika hata ukinipa kusimamia kamati ya vinywaji siku ya harusi yenu ili nilewe mpaka nizime data”.
 
29.
Aliondoka lakini kabla hajalifikia gari lake alinigeukia na kuanza kucheka upya alicheka sana tena kwa dharau kubwa kisha akasema. “jitahidi kuota usiku ndugu yangu hizi ndoto za mchana huambatana na uchizi, eti leo Jamie na mtoto wa Rais wakati hata mkuu wa wilaya yako hakujui wapi na wapi, fungua kichwa we bwege nyie ndo huwa mnakufa kibudu huna mbele wala nyuma. Mi naondoka bwana utamsalimia Rais na shemeji yangu sawa kaka?” niliendelea kumuangalia aliwasha gari, mlinzi wangu alifungua geti na akaondoka zake.



Nilihisi miguu inaishiwa nguvu nikajikuta nadondoka, nilijitahidi kujikokota mpaka ndani kwangu nikaketi sebuleni, huku moyo ukinienda mbio mithili ya pangaboi, nilikuwa sina nguvu kabisa hasra zimenijaa. Ujasiri pekee ndiyo ilitakiwa kuwa ngao ya maisha yangu kwa wakati huo na katika maisha yangu huwa sikubali kushindwa.



Nilikuwa jasiri na kuamini kila kitu naweza kupambana nacho, niliisogelea friji iliyokuwa jikoni nikachukua maji yangu yakunywa hayakuwa ya baridi sana nilikunywa ili kuupoza moyo urudi kwenye hali yake. Ilichukua muda na hatimaye mapigo yalianza kushuka na kurudi kwenye hali yake ya kawaida.



Nilirudi sebuleni na kuketi kwa utulivu huku nikiwaza na kuwazua juu ya mambo yanayozidi kuniandama kwanini ni mimi tu, sina mpenzi na naona kama hata rafiki nimempoteza sababu ya kulisaka penzi la Jesca. Siwezi kumlaumu mtu maana nimeyataka mwenyewe, huenda Dominic yuko sahihi au mimi niko sahihi hivyo hakuna jibu la moja kwa moja. Nilikuwa naongea peke yangu kama mwehu narusha mikono na kujidharau nilikuwa kama mwehu alieyeshindikana Milembe.



Maisha huwa na vituko na yakikuamualia unaweza kuwa kichekesho, katika maisha yangu sijawahi hufurahia mapenzi, kwa hilo nisiwadanganye, ni wanawake watatu niliowahi kuwa nao katika mahusiano, lakini kila mtu na vituko vyake.



Wakwanza ni Anna Mwanjerwa mtoto kutoka Mbeya huyu alikuwa anatupanga kama behewa za treni akitoka huyu anaingia huyu nikavumilia mwisho yakanishinda watu walikuwa wanamuita maharage ya Mbeya yaani maji maramoja.



Wapili Salome Mchunguzi huyu ni mhaya mmoja kutoka huko mapenzi yalikokulia. Yeye kila kitu afanyiwe, masaa yote anataka uwenaye hata ukiwa kazini anatamani ukaenae ofisini tangu asubuhi mpaka muda wa kuondoka, hapiki, hafui, hasafishi nyumba, haoshi vyombo wala kutandika kitanda pesa anatumia kama mchwa akitaka kitu mpaka kipatikane ndo amani itarejea ndani alinishinda nuikamwambia ajaribu kwingine.



Wa tatu ni Maria huyu yeye na pesa kama ATM, mdomo hauna breki ni matusi kwa kwenda mbele ungemkuta anaongea ungedhaani ni wapigadebe wa standi waliozurumiana shilingi mia maana hayo matusi yalimfurahisha mwenyewe anatokwa maneno kama kapoteza koki.
 
30.
Sasa nahitaji mpenzi wa tofauti nahitaji mpenzi wakunifariji, nahitaji mpenzi atakayeniheshimu, nahitaji mpenzi atakayejali shida zangu. nahitaji mpenzi atakayeficha aibu zangu, nahitaji mpenzi atakayenitunza na kuifanya furaha hii idumu milele. Ukweli hautapingika simujui hanijui kiundani lakini maongezi yetu yananipa picha kuwa Jesca ni mwanamke pekee atakaye nifaa maishani.



Ilikuwa yapata saa tano usiku sasa nilinyanyuka kwenda chumbani nakuta simu yangu niliyokuwa nimeitoa sauti inatoa mwanga kuashiria ilikuwa inaita. Alikuwa ni mama tulisalimiana na tukaongea mambo kadhaa vilevile alikuwa analalamika mgongo unamsumbua nilimshauri aende hospital na pia nikaahidi kwenda kumtembelea siku yoyote. Baada ya kuishusha simu ile kutoka sikioni, nilikuta missed calls tisini na tisa za namba ngeni, nilishituka kidogo maana siyo kitu cha kawaida. Niliamua kupiga simu iliita kwa muda kisha ikapokelewa ni msichana mmoja aliniuliza we nani? Nilimjibu kwa jeuri kuwa mimi ndiye nilipaswa kumuuliza we nani maana amenipigia mara 96 alicheka kisha akasema ni Auntie J ngoja nimpe simu. “hallo! Ilikuwa ni sauti ya Jesca Manguli.







Ilikuwa ni sauti ya Jesca Jones Manguli ililalamika amenikosea nini mpaka niondoke kwa hasira pale Gold Crest leo mchana, “Jamie hukupaswa kufanya hivyo, hivi unahisi nilijisikiaje kipindi unaondoka?, labda nikwambie tu kuwa nimejisikia vibaya kuliko ulivyodhani, umeniumiza sana kitu ambacho sikukidhania” Jesca aliendelea kunitupia lawama, alikuwa hajapenda nilichomfanyia na nikweli hata mimi nilihisi kumkosea, tena sana. Alilaumu kwanini sikupokea simu zake nimemfanya alie kama mtoto.



Meneno ya Jesca yalinishitua sasa nahisi ananipenda na hapo ndipo niliporudi na kuitafakari ndoto niliyoiota muda mfupi uliopita, na sasa nagundua Jesca kweli alikuwa na dhamira ya dhati yakuwa na mimi ingawa hajasema moja kwa moja.



Ilikuwa yapata saa tano na robo usiku tuliendelea kunogewa na maongezi, tulipiga soga mpaka mate yakakauka, nilikuwa nikibadilisha vinywaji tu pale sebuleni. Basi tuliulizana mengi mpaka nikapata taarifa juu ya familia ya Rais na familia marafiki zilizoruhusu kupewa.



Haikuwa kazi ndogo lakini huo ndiyo ulikuwa uhalisia maana penzi limekwisha chipua mizizi mioyoni mwetu. Hatukuishiwa maneno na sikumbuki yalitoka wapi, simu ilichemka sikioni mpaka ikapoa yenyewe huku nikiendelea kupiga soga tu. Kiukweli jesca hachoshi kumsikiliza. Hakutaka kukata simu nami sikuchoka kuisikia sauti yake ya upole, ucheshi na unyenyekevu.



Nilikuwa napiga miayo na kuendelea kupiga soga mara kadhaa alinitania nitammeza kutokana na kupiga miayo mara kwa mara, penzi lilichipua bila sisi kujua na huo ndiyo ulikuwa mwanzo mzuri wa mahusiano yetu. Utani, vituko na ucheshi ulinivutia sana na kunifanya nizidi kumpenda msichana huyu.
 
31.
Alam ya saa yangu ya chumbani iligonga ikinitaka kwenda kwenye mazoezi, nilishituka ni saa kumi na moja alfajiri sijalala nilishangaa, lakini sikujali maana Jesca furaha yangu alikuwa akizidi kunipa maneno matamu na sasa sauti yake ilikuwa ikikwaruza kidogo kama vile ametoka usingizini na kuifanya iwe bora zaidi.


Hakuna cha maana tulichokizungumza lakini tulikuwa bize utadhani watoa huduma kwa wateja kwenye makampuni ya simu. Basi tuliendelea kuongea hatimaye saa kumi na mbili asubuhi nilijishangaa imewezekanaje leo niwakuongea na simu masaa yote hayo? Lakini ndiyo hali halisi mapenzi hayana mwenyewe, dalili za kukwama zimeesha jidhihilisha nimenaswa kizembe, nilifanana kama nyati aliyenaswa kwenye mtego wa sungura, nakumbuka simu ilikatika saa kumi na mbili na nusu asubuhi mara baada ya Jesca kuniaga kwa busu tamu kisha akakata simu.



Nililipapasa sikio langu maana sikuamini nilichokisia lakini huo ndo uhalisia, mtoto alikuwa amejaa kweye kumi nanane. Niliingia bafuni nikiwa na furaha, sijui hata ilikotoka hiyofuraha, nilioga huku nikipiga miluzi.



Basi nilirudi nikachagua nguo kwenye zile nguo zangu mpya siku hiyo niliamua kuvaa suti. Ilikuwa ni suti nyeusi ilikaa vizuri nika vaa na kiatu changu cheusi saa ya dhahabu nilinyonga tai nyekundu nikaweka na kitambaa changu chekundu kwenye mfuko wa suti kifuani. Baada ya kumaliza nilipiga unyunyu wenye manukato safi. Nilibeba begi langu na kuliweka kiti cha nyuma cha gari yangu leo niliamua kutumia gari yangu mpya ambayo huwa ni nadra sana kutoka nayo.



Haikuchukua muda nilikuwa nimepaki gari yangu mbele ya jengo la NSSF, niliingia ndani nikaweka begi langu na kuanza shuguli zangu.Nilikuwa na furaha sana hivyo nilifanya kazi zangu kwa furaha sana, na namshukuru Mungu ziliisha haraka na zote zilifanyika kwa ufanisi. Niliiangalia saa yangu ilikuwa ni saa sita mchana nilisema ngoja nikampitie Domi maana ulikuwa ni muda wa kwenda kupata chakula cha mchana, toka asubuhi sijaonana naye.



Niliingia ofisini kwake nikiwa na furaha lakini nilidakwa na maneo ya kejeli “aisee! nakuona mkwe wa Rais naona umeanza kubadirika sasa ni mwendo wa suti, kiatu cha thamani, saa kali nimepita hata nje leo umetoka na ndinga mpya hutaki kuonekana mshamba mbele ya mtoto wa Rais, haongera bwana jitume mtoto wa kiume ule vya bure” Ni maneno ya Domi kiukweli alinikatisha tamaa huyu jamaa na rafiki yangu wa kitambo tulishibana na kupenda mno lakini inaonekana amedhamiria kuuvuruga urafiki wetu, sikuwa na hamu tena yakueleza kilichonileta mule ndani. Nilimsalimia Domi lakini hakuwa tayari kupokea salamu yangu, basi nilikaa kimya na kuamua kuondoka.
 
32.


Nikiwa mwenye mawazo nilitoka moja kwa moja nje, mara nilipofika tu simu yangu iliita niliitoa na kuangalia jina alikuwa ni Jesca. “Jamie hope utakuwa ofisini kwako mimi nipo hapa nilipofikia Gold Crest natamani nikutoe lunch kama hauto jali” niliishusha simu toka sikioni na kutabasamu. “okey nipo hapa nje nakusubiri” nilimjibu kwa haraka zaidi. Moyo ulichanua kwa tabasamu na kujikuta nayasahau yote yaliyonitokea muda mfupi uliopita.



Ilimchukua dakika tano kufika nilipokuwa nimepaki gari, Jesca alikuwa kapendeza sana alikuwa kavaa gauni lake la kitenge refu halikuwa na mikono (mchinjo) lilivutia sana, juu kafunga kilemba kilicho fungwa kwa ustadi mkubwa huku kikilandana kwa karibu na gauni hilo alilokuwa kalitinga, usowake mzuri ulipambwa kwa miwani mikubwa ya jua maana jua lilikuwa kali kidogo ila hakukuwa na joto kali.



Viatu vyake virefu vya wazi vilikamilisha muonekano wake wenye umbo zuri la kupendeza. Huku tabasamu lake mwanana lililovuta hisia zangu mara tu aliponiona lilinifanya niwe taabani. Nilimkaribisha ndani ya gari alishangaa “hii ni gari yako?” nilimwambia ndiyo aliongeza tabasamu maradufu.



Alinikumbatia mara baada ya kuketi, sikusahau kumsifia maana alipendeza “umependeza Jesca sina mfano mzuri wakufananisha, natamani kuuelezea uzuri wako ila nashindwa umependeza msichana mrembo, wewe ni zaidi ya mzuri” nilimsifia bila unafiki alikuwa kalivunja kabati.



Alishukuru na kuniambia nimependeza pia na kisha akaniambia suti ndilo vazi linalonifaa na anatamani kila siku anione nimevaa suti maana kwa muonekano nilionao leo umemvutia zaidi. Basi tulicheka kwa furaha na kukumbatiana tena na safari hii tulibusu kidogo.



Baada ya kumbatio alionekana akivuta pumzi ndeefu kisha akacheka kwa furaha, Jamie usiniambie unatumia Chibu pafyum?” nilijibu “yap” huu ni unyunyu wangu toka bidhaa hii inaanza kuzalishwa nchini. Aisee nimependa sana harufu yako staki kusema inasikikaje ila umetisha sana. Mwanaume unatakiwa unukie hivi bwana siyo mwanaume unanuka shombo la samaki kama pungo kapita. Ilinibi niangue kicheko, maana ukiwa na Jesca matani na vijimaneno vya kejeri havikatiki.



Niliuliza wapi tunaelekea, alinicheka na kuniambia ananisikiliza mimi. Tulitizamana na kuangua kicheko “Jesca hebu kuwa makini bwana punguza utani tulicheka na mwisho alisema twende zetu Kapri-Point.” Sikuona haja yakumbishia na safari ikaanza.



Ni Victoria Hotel nilipoliegesha gari langu nikamsubiri mlembo akashuka kisha tukaongozana na kuingia ndani, tuliagiza ugali na samaki wa kupaka wakati tukisubiri, tuliendelea kupata juice maridadi huku tukipisoga.



Katika kupiga soga ndipo nilipouliza maswali kwanini Jesca kuna wakati anatembea bila ulinzi na wakati mwingine ana ulinzi? Jibu lilikuwa jepesi tu “Jamie kila nilipo ninaulinzi unaweza kuwa wa moja kwa moja ama usio wa moja kwa moja. Ninalindwa wakati wote ukiona niko peke yangu usiniamini jua kuna watu nyuma yangu. Kwa Mwanza kuna wakati naweza kuwa huru zaidi maana ni watu wachache wanaonijua” alimaliza lakini aliona bado nina dukuduku.
 
33.
“najua unajiuliza walinzi walikuwa wapi siku napanda daladala au walikuwa wapi siku tunakutana supermarket jibu ni kwamba usiniamini huenda hata hapa tulipo nalindwa tafadhali yasikushughulishe saana hayo”



Wakati tukiongea nyuso zetu zilikili kuwa hakukuwa na shaka kuwa penzi limeesha ota katikati yetu na ilikuwa ni kazi yetu kulistawisha, najua hakuna aliyemwambia mwenzake lakini kila ishara ya upendo ilikuwepo.



Stori zilitukolea, hatimaye mhudumu aliyechukua oda zetu alikuja na kijana mmoja wakiwa na sahani zetu, ziliwekwa mezani tukaanza kupata chakula. Tulilishana tukanyweshana, tulikuwa kivutio kwa kila aliyekuwa karibu yetu. Jesca sasa alikuwa kaangukia kwenye penzi zito la fukara, alikuwa haoni wala hasikii.

Tulimaliza kula akaniomba nirudi ofisini, nilikataa nikamwambia nimeesha maliza kazi zote ofisini, aliniuliza kama nimeaga nikakataa basi alinyanyuka na kuniambia tuondoke nirudi ofisini si uungwana kuondoka bila kuaga wakati masaa ya kazi bado yangali yanaendelea, tulinyanyuka ingawa sikupenda kabisa kutoka kwani nilitamani tuendelee kuwepo pale victoria.



Mkono ukiwa kiunoni mabusu kila hatua ni tabasamu na vicheko ndivyo vilipamba nyuso zetu, tulipofika nilipopaki gari pasipo kutarajia tulikuta kuna ugeni ukitusubiri ni Dominic na Maria walikuwa wameegemea gari langu.







Kwakuwa nilisha hisi lengo lao sikuwaza nilifika pale waliposimama sikuwasemesha niliwapita kimyakimya na kuwaacha wakiangua kicheko kama wanawake waliokolea umbeya wamefunga safari kwenda kumsuta shoga yao na tayari wameesha mtia mikononi. “He! he! Heee! mbona mtoto wa Rais, tutakoma mwaka huuu”. Waliongea kwa pamoja kwa sadifa, Jesca aliwasikia akageuka kisha akaniuliza kama nawafahamu nilimwambia twende aachane nao.



Nilimfungulia mlango wa gari huku nikizidi kupokea maneno ya kejeli “mwenzetu tunaona unandoto yakuoa Ikulu, jikaze baba kuhudumia mtoto wa rais wa manzese huenda ipo siku TipTop itakukumbuka” maneno hayo yote Jesca aliyasikia vyema.



Nilijikaza kama sijayasikia wakati nataka kuondoka Maria alikuja kusimama mbele ya gari yangu kisha akasema “Jamani wanaume kwa kupenda sifa hamjambo kudanganywa tu ooh! Mimi ni mtoto wa rais bila hata kuchunguza ndo huyo umeanza kuazima gari mpaka suti mtakufa masikini wapenda mitelemko nyinyi”.



Yalikuwa ni miongoni mwa maneno yaliyoniumza zaidi siku hiyo, katika maisha yangu sijawahi kumuomba mtu, wala kumuazima mtu kitu tofauti na kalamu pindi nikiwa shule. Lakini leo natuhumiwa kuazima suti mimi? Yaani niazime nguo pamoja na gari ili nipate nini? Na ili iweje? Nilijiuliza maswali hayo na majibu sikuwa nayo!, moyo ulichafuka ghafla nikajikuta nashindwa kabisa kupumua vyema.



Kilichoniuma zaidi ni gari nililoliota siku nyingi nikajikamua nikajumlisha na mikopo ambayo mpaka leo sijamaliza kulipa nalo naambiwa nimeazima, nisiwe muongo ukweli yalikuwa ni maneno ya udhalilishaji kwangu.
 
34.


Tuhuma hizo kwangu halikuwa tatizo, ila tatizo lilikuwa kwa Jesca ningemueleza nini maana tayari nimejigamba hii ni gari yangu na anaelewa hivyo, na huo ndio ulikuwa ukweli na sasa anapata taarifa kuwa nimeazima hivi naanzaje kumtizama machoni. Nilijitahidi kukaa kimya niliwasha gari nikaondoka na kuwaacha wakizidi kunizonga kwamaneno yasiyo na mantiki.



Nakumbuka hatukusemeshana na Jesca mpaka nilipoegesha gari pale nje ya ofisi yangu ila kabla hajashuka aliniuliza “uliniambia hii gari niyako?” alihoji kutaka kujua. Nilichokifanya nilichukua kadi ya gari na kumpa kisha niliendelea kuwa kimya baada ya kuipitia naamini alilidhika kuwa alichokisikia sicho.



Baada ya kuisoma ile kadi ya gari na vidhibitisho vingine, alinirudishia kisha akashuka bila kuniaga akaondoka zake kuelekea jengo la jilani ilipo Hotel ya Gold crest alipokuwa kafikia.



Niliendelea kumuangalia mpaka alipoingia ndani. Nilijua kabisa nilikuwa nimemkwaza iliniuma sana, nilipaki vizuri gari nikashuka na kuingia ofisini. Nililia sana baada ya kufika ofisini kwangu, hasira zangu humalizwa na kilio ni ngumu sana kunikuta nazozana na mtu katika maisha yangu huwa naiamini amani kwanza kuliko kitu chochote na hili malanyingi watu hulitumia kama fimbo yakuni nyanyasa.



Watu huniona kama mnyonge lakini mimi si mnyonge nina kabla sijachukua hatua huwa najifikiria mimi kwanza. Mimi ni mtu hatari sana baba yangu kanilea katika malezi ya mazoezi magumu maana alikuwa anacheza kunf-u na karate, pia nimefunzwa vyema na makocha kadhaa wa mchezo huo hatari mpaka namaliza chuo kikuu nilikuwa na mkanda mweusi nimehifadhi ndani.



Sheria moja wapo ya michezo hiyo ni kutokupigana na mtu asiye na mafunzo ya michezo hiyo hata kama kakuudhi vipi ukithubutu kufanya hivyo huenda ukafia jera au ukakutana na adhabu ambayo hutaisahau maishani.



Sheria nyingine ya mchezo huu inasema huruhusiwi kupigana ila ikibidi pigana ila usiumize, sheria hiyo inaendelea kusema kwa kujilinda umiza ila usiuwe na mwisho inatoa ruhusa ya kuua. Kuna masharti magumu sana ndani ya mchezo huu amabyo sikupaswa kuyaopuuza maana mani ni tunu niliyobarikiwa tangu nikiwa mtoto.



Uvumilivu ni silaha lakini pia nilifundishwa machozi hupunguza uchungu na kunywa maji hupunguza hasira nilichukua chupa yangu ya maji ya kilimanjaro nikanywa huku nikishusha pumzi kwa nguvu.



Niliketi kwenye kiti changu cha kuzunguka nikatuliza mawazo yangu sikuwa na pupa ya kuhangaika na wajinga. Niliwaza na kuwazua kwanini Domic hataki niwe na Jesca? Inakuwaje anapambana na mimi tena kwa kushirikiana na Maria?. Uswahiba wao umeanza lini mpaka kufikia hatua hiyo waliyopo?.
 
35.


Hii inanipa picha kuwa huenda hata kipindi cha nyuma yeye na Maria walikuwa marafiki na inawezekana walikuwa wakinizunguka kimahusiano. Wazo hili nilianza kuliamini kulingana na mienendo niliyokuwa naiona baina yao.



Niliendelea na shughuli zangu za kawaida maana zile za lazima nilikuwa nimeesha kamilisha hivyo sikuwa bize sana siku hiyo. Baada ya muda nasikia mlango uligongwa kwa nguvu niliruhusu “ingia” aliyeingia ni Maria tena akiwa kafura kama mbogo sura imemshuka kama turubai la msibani. Kabla hajaongea chochote nilinyoosha mkono wangu nikiashiria arudi anakotoka, alijitahidi kuongea ujinga alioujua yeye lakini nilibaki na msimamo mmoja mkono wangu uliendelea kunyooka ukimtaka aondoke maana sasa nilikuwa nimechoshwa na tabia zao. Alitoa matusi, akajigeuza geuza pale na mwisho aliondoka.



Sijui walichokwenda kuhadithiana na ndugu yake maana baada ya muda mfupi nilisikia tena mlango ukigongwa nilifungua na kuwakuta wote wawili. Nilirudisha mlango nikiwaacha wanacheka kwa dharau huku wakipeana zamu ni vicheko vya kijinga tu visivyo na maana wala sababu za msingi.



Muda wa kufunga ofisi saa kumi jioni, nilitoka ofisini nilipofika nje niliwakuta Domi na swahiba wake kipenzi sijui walikuwa wakijadili nini. Niliwapita taratibu nikaingia jengo la jirani la Gold Crest Hotel mpaka golofa ya nne nilifika kwenye chumba alichokuwa akiishi Jesca, niligonga na kusubiri kwa muda lakini kabla sijafunguliwa nilijikuta niko katikati ya watu watatu na wote walikuwa wasichana wakiwa wamevalia suti huku bastora zikielekezwa kichwani kwangu.



Nilinyoosha mikono juu nikihitaji amani “unatafuta nini kwenye chumba hiki?” mmoja alihoji. “Nilikuwa namuulizia Jesca tafadhali” nilijibu kwa uoga huku nikitetemeka. “Jesca yupi na unamfahamu kama nani?”. Sasa nilihisi mkojo unapita maana wale watu walionekana siyo wakawaida.

“Mimi? … aaah! Ni Jamie rafiki yake … ndiyo ni rafiki tu”. Niliona dada mmoja anainua mkono kuelekea kwenye sikio lake alikandamiza kile kidole huku akiinamisha kidevu chake kwenye bega lake, aliongea maneno nisiyoyajua ni mchanganyiko wa namba herufi na mengine siwezi hata kuyahadithia maana sikujua ni Lugha gani na mwisho akataja jina langu Jamie. Baada ya kushusha mkono wake yule dada, bastora tatu zilizokuwa zimekilenga kichwa change zilisogea zaidi.



Basi nilijua nimekwisha hivyo nikabaki kama nilivyo kwa dakika tano hivi. Niliwaza vitu vingi sana ndani ya muda mfupi lakini kubwa lilikuwa ningejua ambalo daima huja baada ya safari.



Nilipekuliwa kama mwizi, mikono ilipita kila kona na baada ya kuhakikisha sina kitu zaidi ya simu na waleti, walinitanguliza mpaka kwenye lifti, nilimuona mmoja wa wale wasichana akibofya kitufe chenye herufi G na safari ilielekea chini tulipofika chini haraka niliingizwa ndani ya gari na gari likaondoka kwa kasi.









Sikujua napelekwa wapi nilichokijua nilikuwa nimekamatwa, hofu ikiwa imeutanda moyo wangu. Sikujua nimekamatwa kwa sababu gani nilichokijua nilikuwa nimejitafutia matatizo mwenyewe. Nilikuwa nikiwaza mle ndani ya gari sikujua nawaza nini maana ni mlundikano wa mawazo yasiyo na mfano nikiwaza namna ya kujinasua mikononi mwa hawa watu, niliwaza hiki kabla kile hakijaisha, nimewaza hiki, hakijafika mwisho nawaza kile yaani ilikuwa shagara bagala.
 
tuna maneno 31003 simulizi iishe.......... ITAENDELEA
BURE SERIES
 
36.
Nilipokuwa nikiziangali sura za wale wasichana zilivyo kavu hapo ndipo nilianza kuuona umhimu wa maneno ya Domi na huyo kichaa mwenziye. Kilichoniuma zaidi mimi sijawahi kukamatwa wala kulala kituo cha polisi si hilo tu hata kesi ya kusingiziwa sijawahi kuwa nayo, lakini sababu ya mapenzi naziona dalili za kulala selo leo.



Sikuwa najua tunaenda wapi kwani ile gari ilikuwa haioneshi nje, ukiwa ndani hautaweza kuona kinachoendelea nje. Baada ya mwendo mfupi hatimaye ilifunga break eneo ambalo sikulijua, mlango wa gari ulifunguliwa nikatoka, na kwa wakati huu nikama nilikuwa huru maana hakuna aliyenizonga wala kushughulika na mimi.



Ni kapre-point kwenye lile geti la kipindi kile nilipokuja kumsaka Jesca nilibaki najiuliza kwanini nimeletwa hapa? Kuna nini kinaendelea?. Maswali lukuki yasiyo na majibu yalizidi kuniandama.



Geti lilifunguliwa nikaruhusiwa kuingia kwa bahati nzuri nilimuona Jesca akija kwa tabasamu mwanana. Jesca ndiye aliyenipokea kwa furaha tukakumbatiana huku akinikaribisha ndani kwa furaha. Tulikumbatiana na kisha akageuka kwa kutumia kidole chake alibofya kitufe kilichokuwa ukutani na geti likafunguka bila shaka lilikuwa linatumia alama za vidole.



Kwa mara ya kwanza nilipata nafasi ya kuingia ndani ya ile nyumba nilikuwa nashangaa kila nilichokiona. Jamani kuna maua humu duniani mengine ndo kwanza niliyaona hapo. Maua mazuri na yanavutia yalipandwa kwa ustadi yalivutia kuyatazama.



Tulilifikia geti la pili ambalo Jesca alilazimika kulifungua kwa kutumia lenzi ya jicho lake kwani kulikuwa na ulazima wakuingiza uso wake sehemu maalumu na geti likafunguka. Tukaendelea na safari baada ya hatua chache kulikuwa na geti lingine ambalo lilihitaji mawimbi ya sauti hivyo kuna maneno alizungumza likafunguka pia. Kabla hatujaendelea alinipa maelekezo “Jamie hili eneo tunaloingia linalindwa na mbwa hatari tafadhari hupaswi kuonesha ishara yoyote ya kuinama narudia tena kuwa makini na hili. Naomba unyoke mpaka nitakapokwambia sasa uko salama” nilimsikiliza kwa makini na safari ikaanza.



Nilinyooka mithili ya mpapai tulitembea mle ndani huku nikiwa naangaza huku na kule sikuona mbwa wala paka waliosemwa basi nikaendelea kushangaa maana mazingira nayo yalishawishi kuyaangalia tu maana yalikuwa fahari ya acho yangu. Huku nikiendelea kujikaza mapaka nikafika tulipokuwa tunaelekea Jesca alisimama kisha akashusha pumzi.



Tulielekea karibu na mlango mmoja nilivyo mjinga si nikainama kutaka kuvua viatu vyangu, asikwambie mtu ni mbwa zaidi ya ishirini sijui walitoka wapi. Zisingekuwa juhudi za walinzi wa eneo lile kuzuia sijui kama ningebaki hai.



Hakuna mbwa aliyenigusa ila nilikuwa najuta kwanini nimeingia eneolile. Jesca alinitizama akacheka kwa maskitiko “Jamie si nimekwambia mapema usiiname? Mbona unataka kunitafutia matatizo bure?” Jesca alikuwa kakasirika sana maana nilienda kinyume na alichonielekeza. “unadhani ungejeruhiwa na hawa mbwa ningejibu nini mimi kwa baba yangu?” alikuwa akiongea kwa uchungu na alizidi kunionya “tafadhali hapa ni Ikulu si pahala salama kama maeneo mengine kutokana na ulinzi wake. Ngoja niwe wazi tu kwako ukikiuka masharti kuna gharama utalipia ambazo ni ghari mno moja ni kujeruhiwa vibaya na pili ni kifo. Sitaki kabisa tufike huko hebu jitahidi kufuata ninachokwambia mimi, sawa Jamie?” Niliitia kwa kichwa na sasa ndo nagundua kumbe nilikuwa jengo la Ikulu ndogo ya Mwanza huwa nasikia tu kuna Ikulu ndogo hapa Mwanza na sasa nilikuwa ndani ya Ikulu mtoto wa kabwela, tabasamu kwa mbaaali baada ya kauli ile sikuwaza tena kuhusu mbwa bali furaha ilijidhihirisha.



Tuliingia ndani tulipofika sebuleni kulikuwa pazuri mno na kama peponi ni pazuri zaidi ya hapa basi mbinguni kuna raha ya milele. Nilikutana na vigae vya ajabu kuwahi kukutana navyo, sakafu ilikuwa mithili ya bwawa la maji ilionekana kama blue bahari na zilionekana mikunjo ya mawimbi madogo ya majini ungechungulia ungejiona kama tufanyavyo kwenye maji.



Kila hatua ukikanyaga kulikuwa na ishara ya mistari ya duara ikisambaa kama yafanyavyo maji uyakanyagapo au kutupa kitu ndani yake, lakini huwezi amini hapakuwa na maji ni urembo tu uliofanisiwa kiustadi. Jamani Ikulu aaah! Acheni paitwe Ikulu bwana.



Jamani kwa uzuri huu hivi viongozi wa afirika wanawezaje kuachia madara? Bila shaka ni ngumu tena ngumu haswaa maana wanajiuliza wakitoka hapa wakaishi wapi tena?. Hii naambiwa ni ikulu ndogo vipi kuhusu makao makuu ya mheshimiwa huko anakoishi kila siku? Staki kuwa mnafiki mtu akikabidhiwa Ikulu akaiachia kwa amani basi ana mungu ndani yake bila hivyo lazima mmtoe kwa mabavu maana atapaganda kama kupe.
 
37.


Mara tu tulipofika ndani kuna ngazi zilishuka chini, basi tuzifuata na kukuta kule chini kumejengeka ni uwazi mkubwa na eneo la kutosha kiukweli ilikuwa fahali ya macho kwangu. Tulitembea kidogo tukakutana na ngazi zingine zilizozidi kutupeleka chini zaidi na hatimaye tukakutana na eneo jingine zuri zaidi. “Jamie karibu sana ndugu yangu, jisikie uko nyumbani” basi wahudumu walikuja na kutuletea juice huku tukiendelea na maongezi.



Jesca aliniambia walinzi wake wamemwamuru kuhama kule alikokuwa kulingana na hali ndogo yakiusalama. Mle ndani wamekuwa wakiingia watu ambao huenda wanawahofia hivyo ili aendelee kuwa salama zaidi ameamuliwa kuja kuishi hapa. “Nimetolewa pale hotelini mnamo saa nane mara baada tu yakutoka kula chakula cha mchana hivyo niko hapa kwa sasa. Na ndiyo maana hata ulipokwenda kunifuata najua hawajakupokea vizuri hizo ni changamoto na huo ndiyo ukubwa.



Karibu sana rafiki yangu kipenzi hizi ni nyumba za baba yangu kwa sasa na hazitatutambua mara tu akiondoka madarakani hivyo karibu sana na ujisikie huru” alinikaribisha kwa upendo.



Nilifurahi sana na sasa sikuwa na shaka tena juu ya ukweli wa binti huyu niliamini kweli ni mtoto wa rais wala hakukuwa na shaka juu yake. Tuliendelea kuzungumza mambo mengi Jesca alitamani sana sikumoja nimpeleke akawaone wazazi wangu ingawa kwa upande wangu sikutamani hata sikumoja kukutana na baba yake maana nilikuwa namuogopa balaa.



Macho yangu hayakuchoka kuangaza maana yalikuwa yakitamani kukiona kila yalichodhani ni kizuri. Niliangaza huku na kule ili kukidhi kiu ya macho yangu, ukweli asikwambie mtu jamani Ikulu ni pazuri, Ikulu pana mvuto waajabu na nashawishika kuiunga mkono kauli ya mwasisi wetu na rais wa kwanza wa taifa hili kuwa ikulu ni mahala patakatifu.



Sikuwa na ndoto za kukanyaga Ikulu leo Jamie Justine niko ndani ya Ikulu ni furaha iliyoje?. Pamoja na kuwa ni ikulu ndogo huenda ipo siku nitakanyaga ilipo ikulu kubwa tuombeane kheri.



Tuliendelea na mazungumzo, Jesca alinieleza kuwa mimi ni zaidi ya ndugu kwake alinikumbusha jinsi nilivyomsaidia kipindi cha ile kesi yake na mpaka sasa ninavyozidi kuwa karibu na yeye. Jesca alionekana kuguswa sana na alikuwa msichana muelewa hivyo hakusita kutoa shukrani zake mara kwa mara kwangu akisema “Wewe ni rafiki yangu wakwanza katika maisha yangu kukuleta ndani ya nyumba hii” alisema Jesca.



Aliendelea kuhadithia kuwa walinzi wake walibaki Gold Crest na walipopiga simu aliwaomba wanilete, “nakuthamini sana na nimetokea tu kukuweka moyoni, najua inakuwa hivi sababu ya upole wako na ukarimu, pia thamani unayoitoa kwa watu bila kujali matabaka yao.



Mimi ni miongoni mwa watu unaowaheshimu na kuwapenda najua hukunisaidia kwasababu ni mtoto wa rais, ulinisaidia kama mtu mwingine mwenye shida ahsante sana.” Nilitabasamu huku nikiupokea mkono wake ulioelekezwa kwangu kivivu niliupokea na kuuelekeza kinywani kwangu ili niubusu maana ulivyokuwa umekunjwa ulihitaji kupata huduma hiyo. Lakini kabla sijafanya hivyo Jesca aliuchomoa kwa nguvu na kujikuta nabusu mkono wangu huku akinicheka.



Basi wote tulifurahi na nilivutiwa zaidi na tabasamu la Jesca, lilikuwa na mvuto usio wa kawaida. Jesca Jones Manguli msichana mrembo mwenye hadhi ya kiafrika na sifa za kiafrika halisi. Hana nyodo, hajisikii ni mtu anayeishi maisha ya kawaida kabisa ya kumheshimu kila mtu anajichanganya na kutumia usafiri wa umma kama tufanyavyo sisi.



Tuliendelea na maongezi lakini katikati ya maongezi ni kama alikumbuka kitu aliniuliza “Jamie yule dada aliyetukuta Victoria leo nikama niliwahi kumuona ofisini kwenu ni mfanya kazi mwenziyo?” aliuliza kwa tahadhari kubwa nilimjibu kuwa nikweli alikuwa mfanyakazi mwenzangu na ndiye aliyekujibu vibaya siku umekuja kuomba msaada wa kumtafuta George Faru.



Kisha niliendelea, Si hilo tu hata yule jamaa waliyekuwa naye nilimwambia pia alikuwa ni rafiki yangu, na pia ni boss wangu pale kazini. Alitikisa kichwa kuashiria ameelewa. Aliuliza swali jingine “unawezaje kuwa na marafiki wa aina hiyo na bado ukaendelea kuwaita marafiki mbele za watu? Watu walioweza kukuaibisha mbele ya kadamnasi na bado ukaendelea kuwatambulisha kama marafiki? Au ndo urafiki wa siku hizi ulivyo?” nilicheka kidogo baada ya swali hilo kisha nikamjibu. Unyenyekevu ni silaha katika maisha ya binadamu.



Kabla sijamaliza Jesca alidakia na awamu hii alionekana kuwa serious zaidi alitoa kauli hii “Unyenyekevu huwa ni ujinga ukikubali kunyenyekea mambo yanayokuumiza, kwa kuogopa kukosana na watu. Kumbuka hakuna mtu wakuamua juu ya maisha yako bali ni wewe mwenyewe” nilibaki kimya sikujibu kitu maana alichokisema kilikuwa kweli asilimia miamoja.



Jesca alionekana kukwazika sana na kile kilichotokea leo “Jamie wewe ni mwanaume hebu kuwa na tabia ya kukemea ujinga, unadhani mungekuwa mnaishi kwa kuheshimiana hao unaowaita wafanyakazi wenziyo wangekuja na kukudhalilisha leo pale victoria?” aliniuliza “Hapana isingetokea” nilijibu kwa aibu aibu. “Hebu badilika, kijana mzuri na mtanashati kama wewe, unahitaji heshima na siyo kukubali kudhalauriwa. Nibora akudharau asiyekujua kuliko mtu unayeishi naye kila siku na na unamuita rafiki. Lakini nibora udhalauliwe kimyakimya kuliko kuanikwa mbele za watu. Jamie sikufundishi uishi vipi ila jifunze kuyatatua matatizo yakiwa madogo usisubiri yakue maana mwisho wake huwa fedheha. Kwa picha ile inaonesha hawajaanza leo kukudharau si ndiyo?.” Yote aliyoyasema Jesca yalikuwa kweli kabisa na sasa niligundua upole wangu ndio uliokuwa ukisababisha nizidi kudhalauriwa.
 
Back
Top Bottom