Zaytun Swai amuomba Rais Samia mashamba yafufuliwe ili kuinua uchumi wa Arusha

Zaytun Swai amuomba Rais Samia mashamba yafufuliwe ili kuinua uchumi wa Arusha

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

MHE. ZAYTUN SWAI AMUOMBA RAIS SAMIA MASHAMBA YAFUFULIWE ILI KUINUA UCHUMI WA ARUSHA

Mbunge wa Viti Maalum CCM - Arusha na Mjumbe wa Kamati ya Bajeti ya Kudumu ya Bunge Mhe. Zaytun Swai amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufufua Mashamba ya Maua na mbogamboga Arusha.

"Mashamba haya ni ajira kwa wananchi, vilevile kutuongezea fedha za kigeni. Mara kadhaa kupitia Bunge tumeishauri Serikali kufufua Mashamba" - Mhe. Zaytun Swai

"Mheshimiwa Rais tuna wafanyakazi zaidi ya 500 ambao wanadai mafao yao. Tunaomba Mhe. Rais ulichukulie jambo hili kwa ugumu wake" - Mhe. Zaytun Swai

"Mhe. Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, Ujio wako wa Arusha ni baraka sana kwetu, vilevile maendeleo unayoyaleta Arusha ni makubwa na tunayathamini sana" - Mhe. Zaytun Swai
 
Back
Top Bottom