Kada,
Umeliwa! Sisi tunajua mchezo wanaoucheza kina Rostam. Wamewatumia watu wengi kutetea mafisadi kwa njia mbalimbali. Wanalotaka ni kutuondoa kwenye mjadala wa kitaifa ulioibuliwa na wapinzani, laini hatuondoki ng'o! Naona wewe umeshajitumbukiza kwenye viatu vyao, kujaribu kutufanya na sisi tuelekeze mawazo yetu WANAPOTAKA wao. Hivi unafanya makusudi kutimiza haja yao au nawe umekumbwa bila kujua? Bwana ee, turudi square one, tujadili hoja ya msingi. Achana na hoja za kina Rostam na Lowassa kupitia Ze Comedy, tena tutawazomea hata hao Ze Comedy! Kada, amka usingizini usitumiwe!
mkuu umenikuna,
nadhani hao ze comedy wakiendekeza njaa za kuwakumbatia mafisadi dawa yao ni kuwazomea.. na hivo kibarua chao kuota majani ghafla!
Kwahiyo hawa mafisadi wanataka kutwambia kwamba kwa vile Slaa alifanya kosa huko nyuma basi nao ni halali wazidi kuiba pesa zetu?? na kutuingiza mikenge ya mikataba mibovu tena miaka 50??
Vyovyote vile ama slaa alikula hizo hela ama hajala... sisi shida yetu ni mafisadi wa raslimali za Taifa letu period!