Zelensky: Hakuna nchi inayoweza kustahimili vita na Urusi peke yake

Zelensky: Hakuna nchi inayoweza kustahimili vita na Urusi peke yake

Awe makini tu Putin asije kumpatia yeye hicho anachoongelea yani kuuweka usalama wa maisha yake mashakani
Huyu ni mjinga na kwa ujinga wake anataka kuishirikisha dunia iingie gharama
Akubaliane na Putin maisha yaendelee aache udwanzi
Kama hawa watu/washirika wa ukraine wangekuwa na akili wangeingia vitani na Russia moja kwa moja
Wameshindwa kuishinda Russia kwasababu
Mfano mimi nina mishale elfu tatu wewe una mishale mia mbili unaomba maswahiba zako wakusaidie mishale ya kupambanna na mimi mmoja anakupa mishale mia mwingine anakupa mia mbili na mwingine anakupa hamsini jumla unakuwa na mishale 550
Ukija kwangu ninayo 3000 utatoboa vipi sasa

Hawa maswahiba zako wanazo stock za kutosha sana lakini hawako tayari kutoa kiasi kikubwa kwaajili yako sasa ushindi utapata vipi hapo

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Angefuata mkataba wa amani yote yasingemkuta yy kajitutumia kwa kutegemea silaha za msaada halafu puttin alivyo mhuni yy anateka sehemu muhimu tu za kiuchumi sasa hv kambakishia bandari moja tu ya odessa ikichukuliwa na hyo atakuwa km burundi au rwanda land lock
 
Tumuulize Zelensky kama alimaanisha mpaka US au lah .🤔

Lakini kwa maelezo yake Zele ni kuwa hata US hawezi mshinda Russia akiwa peke yake.
Ndio anachosema zelensky. Kwani anae supply silaha Ukrainei kwa sasa ni ni nani? Si kibaka Mmarekani? Zelensky alipewa wito wa kusaini kusitisha vita kunako 2022, akapigwa mkwara na Bori Johnson, akarudi nyuma. Bado siku kadhaa tu majeshi ya Warusi wafike Kyiv, aendelee kushupaza fuvu tu mpaka wamfikie! 😀 😀 😀
 
Ndio anachosema zelensky. Kwani anae supply silaha Urusi kwa sasa ni ni nani? Si kibaka Mmarekani? Zelensky alipewa wito wa kusaini kusitisha vita kunako 2022, akapigwa mkwara na Bori Johnson, akarudi nyuma. Bado siku kadhaa tu majeshi ya Warusi wafike Kyiv, aendelee kushupaza fuvu tu mpaka wamfikie! 😀 😀 😀
Nadhani kimoyomoyo anajutia sana ile Fursa
 
Nilisema humu na nitaendelea kusema kuwa; Russia ni dubwasha lenye nguvu mno kivita siyo nchi ya kuikabili kirahisi katika mapigano ya kivita.
Silaha nyingi alizo deploy dhidi ya Ukraine ni zile za Soviet era, Zelensky alikosea na anaendelea kukosea kuwategemea "walimwengu" kumsaidia.
Marekani, ujerumani, uingereza, polandi, Latvia n.k wamejitahidi kupeleka silaha na wanajeshi uwanja wa vita dhidi ya Russia lakini wameishia kupata hasara

Ifike mahala akubali kukaa meza moja na Hilo dude wayamalize kiujirani. Jiografia ya marekani kuisaidia Ukraine at a full scale haisapoti.

Taifa pekee duniani la kukabiliana na Russia kivita wakatoshana nguvu labda marekani ( of course number matters a lot).

Warusi ni jamii korofi na yenye kujiamini sana.
Ila mbona kule Nagorno-karabakh Russia alimshindwa Uturuki mwaka jana?
Russia ni giant fusa"by penguins of Madagascar's voice".
Ila usi draw general implication kuwa ni US pekee ndio inaweza kusimama na Russia.
 
US hawez enda head to head na Russia bila washirika wakuu.

US hawezi kujirisk kupigana na linchinkama Russia, Ni risk kubwa sana.

Russia angekuwa soft NATO wangekuwa washamvamia na kuondoa Serikali, lakin wanahofu kubwa sana na wako makini sana.

Imagine silaha tu za kumpa Zelensky apige Moscow hawataki na wanaogopa. Why??
Nikajua silaha za kupiga mosco washamkabidhi kumbe maneno tu hamna kitu
 
Kiongozi wa Ukraine anahimiza ulimwengu kuungana dhidi ya Moscow

Hakuna nchi inayoweza kustahimili vita na Urusi peke yake - Zelensky

Vladimir Zelensky wa Ukraine ameitaka jumuiya ya kimataifa kufanya kazi pamoja dhidi ya Urusi, akisisitiza kwamba hakuna taifa linaloweza kunusurika vita na Moscow peke yake.

Katika mahojiano na vyombo vya habari vya Asia ya Kati siku ya Jumamosi, Zelensky alisema lengo linapaswa kuwa kuhakikisha kwamba Rais Vladimir Putin "anafikiria juu ya maisha yake na usalama wake," na kwamba "Warusi wanafikiria jinsi wanaweza kuepuka kupoteza uhuru wa nchi yao. - bila kuwatishia - kwa kuonyesha tu jinsi ulimwengu ulivyo na umoja, jinsi ulivyo na nguvu."

Umoja huo unahitajika kwa sababu "hakuna anayeweza kustahimili vita kamili na Warusi peke yake," kiongozi huyo wa Ukraine alisema, kama alivyonukuliwa na gazeti la mtandaoni la Kazakh la Vlast.

"Tulikuwa peke yetu, tulikuwa peke yetu" wakati Urusi ilipoanzisha operesheni yake ya kijeshi dhidi ya Ukraine mnamo Februari 2022, Zelensky alidai. "Lakini basi tulikubaliana na washirika wetu juu ya aina fulani ya vikwazo, aina fulani ya silaha na mambo mengine," alisema. alisema, akimaanisha msaada uliotolewa na nchi za Magharibi tangu kuanza kwa mzozo huo.

Hata Beijing "lazima ilinde Ukraine kwa sababu tulishambuliwa," kama "China inasema kwamba uadilifu wa eneo lazima uheshimiwe," mwanasiasa huyo alisema.

My Take:
😷
Taifa la Mungu Israeli likiingia front wakiwa na Mungu - Yehova YWHW, dakika sifuri Russia anasamaratishwa. rejea vita ya Daudi na Goliathi
 
Taifa la Mungu Israeli likiingia front wakiwa na Mungu - Yehova YWHW, dakika sifuri Russia anasamaratishwa. rejea vita ya Daudi na Goliathi
kama alivyoisambaratisha hamas na kuokoa maagaaidi wake wote wanne waaliotekwa na hamas😁😁😁
 
Kiongozi wa Ukraine anahimiza ulimwengu kuungana dhidi ya Moscow

Hakuna nchi inayoweza kustahimili vita na Urusi peke yake - Zelensky

Vladimir Zelensky wa Ukraine ameitaka jumuiya ya kimataifa kufanya kazi pamoja dhidi ya Urusi, akisisitiza kwamba hakuna taifa linaloweza kunusurika vita na Moscow peke yake.

Katika mahojiano na vyombo vya habari vya Asia ya Kati siku ya Jumamosi, Zelensky alisema lengo linapaswa kuwa kuhakikisha kwamba Rais Vladimir Putin "anafikiria juu ya maisha yake na usalama wake," na kwamba "Warusi wanafikiria jinsi wanaweza kuepuka kupoteza uhuru wa nchi yao. - bila kuwatishia - kwa kuonyesha tu jinsi ulimwengu ulivyo na umoja, jinsi ulivyo na nguvu."

Umoja huo unahitajika kwa sababu "hakuna anayeweza kustahimili vita kamili na Warusi peke yake," kiongozi huyo wa Ukraine alisema, kama alivyonukuliwa na gazeti la mtandaoni la Kazakh la Vlast.

"Tulikuwa peke yetu, tulikuwa peke yetu" wakati Urusi ilipoanzisha operesheni yake ya kijeshi dhidi ya Ukraine mnamo Februari 2022, Zelensky alidai. "Lakini basi tulikubaliana na washirika wetu juu ya aina fulani ya vikwazo, aina fulani ya silaha na mambo mengine," alisema. alisema, akimaanisha msaada uliotolewa na nchi za Magharibi tangu kuanza kwa mzozo huo.

Hata Beijing "lazima ilinde Ukraine kwa sababu tulishambuliwa," kama "China inasema kwamba uadilifu wa eneo lazima uheshimiwe," mwanasiasa huyo alisema.

My Take:
😷
Hata urusi haiwezi kustahimili vita pekeake pia. Msaada wa silaha ndio habar ya mjini
 
Back
Top Bottom