Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
Kama bara la Afrika tungejali mali za wananchi wetu, tungekuwa tumepiga hatua kubwa sana.
Kuhusu yale majibizano, Trump amefeli vibaya mno, kwani kwa mara ya kwanza katika historia, BBC inasema haijawahi kutokea—na huenda isitokee tena—Rais wa Marekani kujibiwa kwa urahisi namna hiyo mbele ya Ikulu yake. Jambo hili linapaswa kuwa somo kwa marais wa mataifa mengine wasikubali kuuza utu wao kwa mabeberu kijinga.
Nasema wazi kwamba Trump hatathubutu tena kuonyesha mazungumzo yoyote na Zelensky, na hata akifanikiwa kuongea naye tena, sina shaka hana hamu. Naamini hata kanisani leo hajaenda, bado anawaza yale majibizano, maana waliomdhania ni mtu wa kusaini makaratasi bila kuuliza maswali walijikuta wakikosea vibaya.
Licha ya uwezo wake wa kudhibiti mitandao ya kijeshi, bado ataendelea kuwa mgombea bora wa urais wa 2025, lakini hakuweza kufanikisha lengo lake kwa sababu huwezi kumwita mtu dikteta kisha umualike Ikulu ukidhani utachukua rasilimali zake kirahisi, jambo ambalo haliwezi kutokea katika bara fulani.
Pale alipomwambia huwezi kucheza na ‘strong cards’, alijibiwa kwa wepesi, "Sikuja hapa kucheza kadi." Kwa kweli, Trump alijuta kumwita yule bwana Ikulu, maana walizoea kudharau viongozi wa bara letu, wakiweka masharti ya kishenzi na kubeba mali zetu bila upinzani.
Hakuna sehemu amenifurahisha kama pale alipomwambia, "Unagamble na vita ya dunia ya tatu," kisha akajibiwa kwa ujasiri, "Trump, kwa hiyo umeniita hapa kugamble na madini ya Waukraine? Nimekuja kwa ajili ya wananchi wa Ukraine, mali zao na ulinzi wao, na kama hakuna sehemu ya kuwalinda kwenye mkataba huu, basi naomba niondoke."
Jambo hili linapaswa kuwa funzo kwa viongozi wa Afrika, hata kidogo tu, kwa sababu somo hili halihitaji hata diploma.
Kwa kweli, mwanangu mtarajiwa namsubiri Mei nimpe jina la Zelensky, nikimshukuru mama yake kwa kukubali jambo hili. Viva Ukraine, Viva Zelensky, maana Trump alimdhania kama USAID au UNAIDS, mtu wa kupelekeshwa kirahisi, lakini alikutana na moto!