Zelesnky ni Rais bora duniani kwa mwaka 2025 na hatokaa atokee

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Kama bara la Afrika tungejali mali za wananchi wetu, tungekuwa tumepiga hatua kubwa sana.


Kuhusu yale majibizano, Trump amefeli vibaya mno, kwani kwa mara ya kwanza katika historia, BBC inasema haijawahi kutokea—na huenda isitokee tena—Rais wa Marekani kujibiwa kwa urahisi namna hiyo mbele ya Ikulu yake. Jambo hili linapaswa kuwa somo kwa marais wa mataifa mengine wasikubali kuuza utu wao kwa mabeberu kijinga.

Nasema wazi kwamba Trump hatathubutu tena kuonyesha mazungumzo yoyote na Zelensky, na hata akifanikiwa kuongea naye tena, sina shaka hana hamu. Naamini hata kanisani leo hajaenda, bado anawaza yale majibizano, maana waliomdhania ni mtu wa kusaini makaratasi bila kuuliza maswali walijikuta wakikosea vibaya.

Licha ya uwezo wake wa kudhibiti mitandao ya kijeshi, bado ataendelea kuwa mgombea bora wa urais wa 2025, lakini hakuweza kufanikisha lengo lake kwa sababu huwezi kumwita mtu dikteta kisha umualike Ikulu ukidhani utachukua rasilimali zake kirahisi, jambo ambalo haliwezi kutokea katika bara fulani.

Pale alipomwambia huwezi kucheza na ‘strong cards’, alijibiwa kwa wepesi, "Sikuja hapa kucheza kadi." Kwa kweli, Trump alijuta kumwita yule bwana Ikulu, maana walizoea kudharau viongozi wa bara letu, wakiweka masharti ya kishenzi na kubeba mali zetu bila upinzani.

Hakuna sehemu amenifurahisha kama pale alipomwambia, "Unagamble na vita ya dunia ya tatu," kisha akajibiwa kwa ujasiri, "Trump, kwa hiyo umeniita hapa kugamble na madini ya Waukraine? Nimekuja kwa ajili ya wananchi wa Ukraine, mali zao na ulinzi wao, na kama hakuna sehemu ya kuwalinda kwenye mkataba huu, basi naomba niondoke."

Jambo hili linapaswa kuwa funzo kwa viongozi wa Afrika, hata kidogo tu, kwa sababu somo hili halihitaji hata diploma.

Kwa kweli, mwanangu mtarajiwa namsubiri Mei nimpe jina la Zelensky, nikimshukuru mama yake kwa kukubali jambo hili. Viva Ukraine, Viva Zelensky, maana Trump alimdhania kama USAID au UNAIDS, mtu wa kupelekeshwa kirahisi, lakini alikutana na moto!
 
worst president ever na lijinga halijuu diplomacy. Alipaswa asiende kama alijua atabarazwa. Analeta uanaharakati wa kishoga hahaha na bado he will be disposed through impeachment jinga hilo. Limekubali watu wake wafe kisa kuwafurahisha marekani na USA
 
Ile Cabinet ya Trump ni ya hovyo mno.
Kwanza reporter wa hovyo anauliza swali ..kwanini hukuvaa suti?
Ikiwa juma moja limepita,Elon alienda Oval office kama yupo Chooni vile..hovyo kabisa.
No Trump na team yake wapo poa. Sema wewe na wenzako mmekaririshwa uongo uongo. Yaani ni mjinga pekee atakayeshabikia ukrain kuendeleza vita kwa maslahi ya usa na eu. Ukraine has benefited nothing kabisa kwenye hii vita. Na kauli yake ilipaswa kusema no NATO wala psingekuwa na vita
 
Hongera mwenzetu mwenye akili.
Naona upo Cabinte ya Mmarekani,sikuwa nimejua.Hongera sana Mkuu.Timiza wajibu mwenye akili.
 
Hongera mwenzetu mwenye akili.
Naona upo Cabinte ya Mmarekani,sikuwa nimejua.Hongera sana Mkuu.Timiza wajibu mwenye akili.
adrenaline mnakera mkuu. Unajua before Trump kila kiongozi mkubwa wa Ulaya alikuwa ana tout about haki za binaadamu za ushoga na kiongozi africa alikuwa akipinga wanamnyima missada and it was that kinda of thinking, hebu tell me leo kuna kima wa ulaya kanyanyua mdomo wake kuhusu ushogaaaaa??? So Trump is for American 🇺🇸!
 
Mzee Trump is the best,zingine porojo
 
Kwenye mitandao ya kijamii imeonyesha raia wengi wamefedheheshwa na Trump hadi wengine wamefika mbali xaidi kwa kusema " nimejisikia aibu kwa alichokifanya rais wangu"
Ni aibu kwa Taifa kama Marekani kufanya walichofanya.Yale yalikuwa ni mazungumzo official sana kwa Taifa kama lile.
Dharua na viburi vinafanya taiafa kubwa lionekane kama watu wake hawako njema upstairs.
Walimcheka Biden kuwa hajua kiwakilisha Taifa.

Maisha huwezi kuta Putin akawa na vikao vya kiwaki kama kile.Hovyo kabisa.
Sijapinga Trump is for America na awe hivyo.
Approach waliotumia kuita kikao na kuwa reporter kama yule kenge anahoji kwanini mtu hakuvaa suti unahisi wana akili?
Ule ni mkutano mkubwa sana,wao wameamua kuendesha kama mkutano wa Vikoba Mkuu.

Tafakari sipingi namna zao,nachopinga ni Taifa kama Marekani kuwa hewani na kuhojiana na Bwana Zelensky kama wapo kijiweni vile.

Hadhi ya ukubwa ya America ipo wapi?
Ndio maana hata Elon anaweza kuja na Kobasi na Tshirt pale Ikulu kama chumbani kwake.

Hoja zao zilikuwa sahihi lakini njia walizotumia ni kama tulikuwa tunaangalia comedy za mitaani.Hakuna Heshima..
 
Mkuu alipaswa kuvaa suit huo ujinga wake ni wa huko huko nchini kwake. In fact jifunze, usipende kujionesha/kujisemea matatizo yako kwa watu hakuna wa kukuonea huruma!
 
Mkuu alipaswa kuvaa suit huo ujinga wake ni wa huko huko nchini kwake. In fact jifunze, usipende kujionesha/kujisemea matatizo yako kwa watu hakuna wa kukuonea huruma!
Sasa kama wenyewe walituonyesha Elon yupo Ikulu na Tshirt..nije na Suti isaidie nini?Kubeba madini?
Zelensky amefanya kama ilovyostahili.

Na ndipo wakaonekana wajinga hata kama wana hoja za maana.
Kuna respect flani hivi imepungua kwa Superpower...tusipiane moyo..sio jibwa tena linabweka kama zamani.

Oval office imekuwa kijiwe cha kahawa na misuto fullstop...wakajifunze kwa PUTIN huko namna ya kuheshimisha Nchi na Uongozi...
 
HATA vicoba Wana HESHIMA yule n mwehu trump
 
Ushoga umeingiaje tena kwenye uzi hivi kuna mahali mleta uzi kaongelea ushoga
 
Si kwamba haijawahi ila ni kwamba haijawahi kutokea mbele ya camera. Hawakutegemea aanzishe mazungumzo yale pale. Hata wao wanakwambia pale ilikuwa kuwataarufu watu kuwa wanakuja sign mkataba hayo mengibe walitegemea watayazungumza off camera ila jamaa akayaibua.
Vyovyote iwavyo vita ashaishindwa kitakachofuata ni propaganda za kumwondoa madarakani kwanza
 
Ila mkumbuke, USA under Trump wanamuona Zelensky kama mtu mfu anaetembea, soon mtasikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…