Nifah
JF-Expert Member
- Feb 12, 2014
- 34,020
- 79,098
Mkono mtupu haulambwi!
Naam, ndivyo ninavyoweza kulielezea hili.
Wikiendi iliyopita Rais alijumuika kwenye uzinduzi wa albam ya msanii wa kizazi kipya Harmonize akiwa kama mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa wengine ambao ni viongozi na wadau wa tasnia ya burudani.
Katika uzinduzi huo Rais alitangaza rasmi ushiriki wa wasanii katika ziara zake ikiwemo ziara inayotarajiwa hivi karibuni nchini Korea ya Kusini, kisha kufuatiwa na ile ya Marekani.
Japo tangazo lake hilo lilikuja ikiwa tayari wasanii (waigizaji) walishaanza kufunga safari kuelekea nchini huko kabla ya Rais kuungana nao hapo baadaye.
Zengwe katika wasanii watakaosafiri na Rais
Kuna mchezo mchafu umefanyika katika nafasi za wasanii watakaoungana na Rais ziarani hapo. Safari hii ya Korea ya Kusini Rais ataambatana na waigizaji filamu.
Mkurugenzi wa bodi ya filamu nchini Dr. Kiagho Kilonzo anatajwa kufanya upendeleo kwa kupoka nafasi ya muigizaji mmoja mwanamama (jina linahifadhiwa kwa sasa) kisha kumuweka mwanadada mwingine anayedaiwa kuwa mpenzi wake.
Upendeleo huo wa waziwazi umewaumiza na kuwasononesha wengi, lakini Mkurugenzi hakujali hilo zaidi ya kuweka maslahi ya mpenzi wake mbele!
Kupitia chanzo changu nyeti,
Nifah.