Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Usikute huyo msanii wa kiume vetting imegomaView attachment 3002202
Mkono mtupu haulambwi!
Naam, ndivyo ninavyoweza kulielezea hili.
Wikiendi iliyopita Rais alijumuika kwenye uzinduzi wa albam ya msanii wa kizazi kipya Harmonize akiwa kama mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa wengine ambao ni viongozi na wadau wa tasnia ya burudani.
Katika uzinduzi huo Rais alitangaza rasmi ushiriki wa wasanii katika ziara zake ikiwemo ziara inayotarajiwa hivi karibuni nchini Korea ya Kusini, kisha kufuatiwa na ile ya Marekani.
Japo tangazo lake hilo lilikuja ikiwa tayari wasanii (waigizaji) walishaanza kufunga safari kuelekea nchini huko kabla ya Rais kuungana nao hapo baadaye.
Zengwe katika wasanii watakaosafiri na Rais
Kuna mchezo mchafu umefanyika katika nafasi za wasanii watakaoungana na Rais ziarani hapo. Safari hii ya Korea ya Kusini Rais ataambatana na waigizaji filamu.
Mkurugenzi wa bodi ya filamu nchini Dr. Kiago Kilonzo anatajwa kufanya upendeleo kwa kupoka nafasi ya muigizaji mmoja mwanamama (jina linahifadhiwa kwa sasa) kisha kumuweka mwanadada mwingine anayedaiwa kuwa mpenzi wake.
Upendeleo huo wa waziwazi umewaumiza na kuwasononesha wengi, lakini Mkurugenzi hakujali hilo zaidi ya kuweka maslahi ya mpenzi wake mbele!
Kupitia chanzo changu nyeti,
Nifah.
Unajaziajazia minyama ili kujustify ulichoandika. Kama list ilishaandaliwa na wahusika wakapewa taarifa alafu mtu from nowhere akate jina huo ni uongo.Yani safari ilishapangwa na washiriki wakapangwa wakajiandaa kwa safari kisha baadae ghafla mshiriki anaondolewa anawekwa mwingine halafu unasema hakuna cha ajabu?
Eti bwaanaa!We Nifah vaa viatu vya mkurugenzi kama ingekuwa ni wewe ziara yenyewe matembezi tu ya hisani
Sikutegemea tofauti kutoka kwako, nimeshakuzoea.Unajaziajazia minyama ili kujustify ulichoandika. Kama list ilishaandaliwa na wahusika wakapewa taarifa alafu mtu from nowhere akate jina huo ni uongo.
Maana kumbuka hiyo ni ziara ya raisi, kabla ya kuteua wa kwenda nae lazima list ipiiwe na iangaliwe kwa ukaribu sana maana pia usalama wa raisi unazingatiwa sana. Sasa mtu tu from nowhere hawezi kukata jina kienyeji hivyo na aweke anayetaka yeye.
Labda useme ilikua ni provisional list tu, na kama ilikua ni provisional basi hakuna haja ya hizi lawama.
Mlipaji ni yule yule, Hazina ya Tanganyika a.k.a Shamba la BibiHizo gharama analipa nani..inaonekana watanganyika tumeshafanywa mafala sasa
View attachment 3002202
Mkono mtupu haulambwi!
Naam, ndivyo ninavyoweza kulielezea hili.
Wikiendi iliyopita Rais alijumuika kwenye uzinduzi wa albam ya msanii wa kizazi kipya Harmonize akiwa kama mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa wengine ambao ni viongozi na wadau wa tasnia ya burudani.
Katika uzinduzi huo Rais alitangaza rasmi ushiriki wa wasanii katika ziara zake ikiwemo ziara inayotarajiwa hivi karibuni nchini Korea ya Kusini, kisha kufuatiwa na ile ya Marekani.
Japo tangazo lake hilo lilikuja ikiwa tayari wasanii (waigizaji) walishaanza kufunga safari kuelekea nchini huko kabla ya Rais kuungana nao hapo baadaye.
Zengwe katika wasanii watakaosafiri na Rais
Kuna mchezo mchafu umefanyika katika nafasi za wasanii watakaoungana na Rais ziarani hapo. Safari hii ya Korea ya Kusini Rais ataambatana na waigizaji filamu.
Mkurugenzi wa bodi ya filamu nchini Dr. Kiago Kilonzo anatajwa kufanya upendeleo kwa kupoka nafasi ya muigizaji mmoja mwanamama (jina linahifadhiwa kwa sasa) kisha kumuweka mwanadada mwingine anayedaiwa kuwa mpenzi wake.
Upendeleo huo wa waziwazi umewaumiza na kuwasononesha wengi, lakini Mkurugenzi hakujali hilo zaidi ya kuweka maslahi ya mpenzi wake mbele!
Kupitia chanzo changu nyeti,
Nifah.
Safari ya Raisi sio rahisi hivyo mtu aamue kukata jina ambalo lilishaenda ikulu. Pengine ungesema wakati wa mchakato wa kupata majina ndio hapo watu walichomekea majina.Sikutegemea tofauti kutoka kwako, nimeshakuzoea.
Habari zilizojaziwa minyama ndizo hujawahi kukauka kwenye hizo threads 😀
Ungetuliza tu akili ukajiuliza hicho chanzo kinachoweza kunipa habari nyeti kama hii wala usingeandika hayo yote.Safari ya Raisi sio rahisi hivyo mtu aamue kukata jina ambalo lilishaenda ikulu. Pengine ungesema wakati wa mchakato wa kupata majina ndio hapo watu walichomekea majina.
Mm nasoma chochote nachokutana nacho, nikiona kinafaa nakikubali, nikiona uongo nasema ni uongo
SureMkuu kula ugali wako ulale, you can’t fix everything.
Mambo mengine ni ya kuyaacha tu.
Wasanii wanaenda wengi, wasanii wana marafiki wengi, marafiki wa marafiki zao nao wapo wengi. Hapo lazima habari zitakua nyingi na za kila ainaUngetuliza tu akili ukajiuliza hicho chanzo kinachoweza kunipa habari nyeti kama hii wala usingeandika hayo yote.
Hata hivyo, habari zangu si za kuokoteza? We ipotezee tu.
Kila fanani na hadhira yake.