Zengwe zito uchaguzi TFF

Mkuu ikithibitika kwamba anatumia fedha/rushwa kutaka kuendelea kubaki madarakani, basi huyo hatufai hata kidogo.
ukiwasikia wanatembeza bakuli kuomba fedha za timu ya taifa utafikiri hawana fedha.
tanzania mpira bado sana
 
Nadhani hujui kazi ya pccb
 
Wame audit pesa za walizowapa, au hujui TBL alimtoa Serengeti Breweries kwa kuingiza kitita kinono cha zaidi ya 5 bil !?

Sent from my Infinix HOT 4 using JamiiForums mobile app
TBL anafanya biashara na TFF na siyo kwamba anatoa msaada kwa TFF.

TFF wanaweza licha ya external Auditor, kukaguliwa na FIFA au serikali iki-sense kuna ufujaji na ukiukwaji wa sheria ya nchi kuhusu kodi na nidhamu(rushwa na ubadhilifu).

TBL anaweza kuondoa udhamini wake ambao ni wa kibiashara hasa pale ripoti za hivyo vyombo zikionesha kuna ufujaji na utovu wa nidhamu.Au anaweza kumwomba TFF ampe ripoti jinsi hela ulivyotumika kulingana na mahitaji ya mkataba baina. Sidhani km TBL ana mamlaka ya kukagua mahesabu ya TFF
 
Ukiwa na akili pana ya kufikiria jambo hili utagundua kabisa kuna suala la uchaguzi linahusika sana kwenye issue ya hawa jamaa, na nina hakika FIFA wamenusa kitu hapa ila ngoja tusubiri tuone kwani fitina za kwenye mpira zinajulikana sana!
 
Kwahiyo mtu anafoji na kuiba pesa huku soka tunazidi kushuka kiwango wewe unaona sawa tu?nadhani wewe ulijui soka na hata huna uchungu nalo utakuwa mshabiki wa bongo flava huku sio kwako mkuu.
Tatizo la wabongo mnapenda kuendekeza majungu, fitna na kutumia taarifa ambazo azijathibishwa kisheria kama ndio taarifa sahihi. Malinzi yupo mahakamani kwa tuhuma tu bado hazijathibitishwa na mahakamani. Jifunze kutatua matatizo yako ya kimaisha na sio kuhamishia chuki kwa watu wengine ambao wamepiga hatua
 
Unakataa kumtetea wakati unamtetea.
Situation iliyopo imekwishakutokea na tuhuma zimewekwa mezani tayari.
Sasa utueleze hilo zengwe unalosema anawekewa Malinzi ili kumbeba nani?
Ama haya mambo unataka yawekweje kwa mfano?
Dadavua mambo ambayo unaona wewe kuwa yanatakiwa kwenda katika njia 1,2,3.
Lakini hii ya kusema walikuwa wapi, hivi kuanza kwa jambo huwa kunampangilio maalumu?
Kwa mfano unapoanza kusinzia saahizi unaweza kujenga swali kuwa kwanini haujasinzia kabla ya muda huu?
Umetengeneza swali linaloegemea upande wa utetezi wa Malinzi ambaye katuhumiwa kwa wizi. Acha sheria ichukue mkondo wake bila kujali kuwa tuhuma hizi zimeibuliwa kwenye mchakato wa uchaguzi.
 
Hawa wanakamati ni wapuuzi, wakiendelea na huu ujinga, magufuli futa hii tff pesa tuelekeze kwenye Mambo mengine!

Hawa walishahongwa kitambo na malinzi!
Kweli wewe ni bendera fuata upepo na inaonekana ni mweupe kabisa katika masuala ya TFF. Pesa muelekeze sehemu ingine wapi? Uliambiwa TFF ni taasisi ya serikali au inaendeshwa kwa kodi za wananchi?
 
Sasa unabishana na dhana ! ?...amini unakiamini
 
Malinzi amepiga hatua !....ushabiki maandazi shida sana
 
Kweli wewe ni bendera fuata upepo na inaonekana ni mweupe kabisa katika masuala ya TFF. Pesa muelekeze sehemu ingine wapi? Uliambiwa TFF ni taasisi ya serikali au inaendeshwa kwa kodi za wananchi?
Ipo kwa maslahi ya nani ? ...ni kampuni binafsi ?
 
Hafungiwi mtu, hata wao corruption imewagharimu. Sepp na katibu wake wapo wapi ?

Tatizo lako wewe licha ya kuyasema sema vibaya baadhi makabila hapa nchini kutokana na inbuilt inferiority complex, sioni kama unaelewa vizuri mbinu zilizo tumika kumuondoa Sepp madarakani - you have no idea kwamba mipango yote ilisukwa na Taifa fulani for Geopolitical reason kuliko masuala ya mpira - FIFA ilikuwa hijacked na wapuuzi hao ambao SOKA sio mchezo wao wa asili wanajitia kimbele mbele tu kuvuruga mchezo unaopendwa sana Duniani, wao hawajawahi ku-contribute chochote cha maana katika masuala ya kuendeleza SOKA Duniani, wao wapo kwenye Ulimwengu wa Baseball na Basketball michezo ambayo hipo confined nchini mwao tu - hakuna Mataifa yanayo chukulia seriously michezo yao.

Sepp amekuwa victim wa a well organised scheme ya mafiosa for Geopolitics reasons - all in all nina uhakika ata bounce back fighting fit - the World inapaswa kumuheshimu Sepp kwa kujitahidi kuondoa siasa kwenye michezo wa SOKA, kusaidia sana third World kuendeleza michezo ya soka kwa kuzipatia fedha za kutosha hakuwa na chembe ya u-racism au dharau - binadamu wote wenye akili timamu wanajua vizuri msimamo ya Sepp wanajua vile vile kwamba usimamizi na msimamo wake ndiyo umewezesha Africa, Asia including Arabuni kukubaliwa ku-host World Cup kwenye Continents tajwa bila ya kujali mashinikizo ya Mataifa ya magharibi kushinikiza World Cup kuchezwa Ulaya, Amerika Kaskazini na Latin Amerika - Sepp stood his ground ndiyo maana walijitahidi sana kumjengea mizengwe ya kumuondoa madarakani - najua mtakuja hapa na madai lukuki lakini ukweli ndio huo.
 
Dunia yote inajua fifa ni wala rushwa, rejea kisa cha Sepp na Platini. Uhaya TFF si wa bahati mbaya...chew it or swallow it !
 
ndugu amini usiamini hakuna uchaguzi ,naona kabisa hii tume ya uchaguzi TFF ilipangwa uwabebe akina Malinzi,inavyoonesha hawa wajumbe 4 kesho na wao watabandika matokeo yao ya usahili mbali na yale ya mwenyekiti
TISS washaingia humo Malinzi hata afanyeje hana chake humo, ajipange tu ni kwa namna gani atasafisha jina lake ili mbeleni huko anaweza kuja kuganga njaa kwenye ubunge kwenye chama chetu kile, cha ndioooooo[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
AlikuwA na Ndolanga na katibu waku Isumaili aka wazee wa kutafuna[emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
AlikuwA na Ndolanga na katibu waku Isumaili aka wazee wa kutafuna[emoji2] [emoji2] [emoji2]

Mkuu nashukuru kunikumbusha Ndolanga, hivi jamaa huyu yupo wapi siku hizi? Looking back now unafikiri kuna chochote kilicho badirika linapokuja suala la kugombea uongozi wa TFF au kug'ang'ania kuendelea kubakia madarakani - hukuna kilicho badirika mkuu - mizengwe imebaki ile ile miaka nenda rudi. Ndiyo maana bado na insist kwamba Viongozi wawe wanachaguliwa/teuliwa na Wizara.
 
Yule hakimu alinusa akagundua ni kubaya ....akachomoa
 
Yule hakimu alinusa akagundua ni kubaya ....akachomoa

Ndiyo maana nasema TFF kuna a deep seated tatizo pale, si bure!! Wataendelea kubadirisha badirisha Uongozi kama nuts za kuunganisha mashine lakini hakuna lolote litakalo badirika - Wizara ndiyo inapaswa kuajiri Director/Manager wa kusimamia kitengo hicho - huo ndio unaweza kuwa ni mwarobaini wa kukomesha matatizo sugu ya Uongozi wa TFF.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…