juan de otaru
JF-Expert Member
- May 23, 2013
- 211
- 113
mwaka 2014 wakati tbl wakiwa wadhamini WA taifa stars wapi audti mkuuTBL ndiyo wana -audit TFF?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
mwaka 2014 wakati tbl wakiwa wadhamini WA taifa stars wapi audti mkuuTBL ndiyo wana -audit TFF?
Home boy Sio!! [emoji2] [emoji2]TFF kunaweza kuwa na matatizo lakini hayaja anza leo,hata wakati wa Tenga mambo yalikuwa hivi hivi hasa wakati wa uchaguzi panajitokeza mizengwe ya ajabu sana, tatizo kuu ni ulaji sio kusaidia uendelezaji wa kandanda nchini, mambo mengi ni maigizo tu. Hivi tukijiuliza imekuwaje PCCB na vyombo vingine vya upelelezi ndiyo yanalivalia njuga suala la TFF at the eleventh hour miaka yote walikuwa wapi?
Mambo ya kuingiza fitna kwenye chombo kinacho simamia soka nchini siyo fresh hata kidogo - nguvu zote zinazotumika ni kutaka kumuengua Malinzi kwa nguvu hawataki agombee tena Uongozi kutokana na wivu tu, sasa Taasisi ya kuendeleza mpira Duniani/Afrika ambayo ndiyo ilitoa fedha za kuendeleza soka nchini ikija hapa na kusema wamefanya an independent uchunguzi na kugundua fedha zimetumika kihalali nyie au Wizara itasema nini kama hatutaonekana ni watu wa ajabu - nakumbuka miaka ya nyuma kuliwahi kutokea mizengwe za kumuengua jamaa fulani kwa fitina na uzushi mpaka taasisi ya kimataifa ya mpira ilipo ingilia kati ndiyo akaruhusiwa kugombea - ya Malinzi yanafuata mkondo huo huo.
Mkuu waambie hao wanakaririshwa tu maneno.Zungumza maneno yenye hekima, lugha zako za vijiweni speaks volume kuhusu tabia zako, labda nikulize swali dogo:Hivi tangu Serikali ya awamu ya kwanza iondoke madarakani unaweza kunipatia takwimu ni lini Tanzania ilifanikiwa kuleta kikombe cha ushindi nchini? Eti kafoji sijui nini ndiyo maana kiwango cha mpira nchini kimeshuka, tangu lina kiwango cha mpira kikapanda nchini - lini? Kiala siku magazeti yamejaa taarifa za infight ndani ya taasisi ya TFF wanagombania ukwapuaji majungu, fitina na tuhuma zisizo kuwa na kichwa wala miguu, nimewahoji tuna uhakika gani kama fedha za FIFA zimeliwa kweli - je wakija FIFA wenyewe wakasema fedha zao zimetumika vizuri nyinyi mtasema nini? Bila shaka mnajua hoja yangu ina mshiko ndiyo maana mnakuja na hoja mbadala eti Malinzi na kundi lake wametumia vibaya michango ya Serengeti, sijui Malinzi na kundi lake wameforge nini - lawama na madai chungu mzima, mnayesema hayo wakati hamjui mahakama itasema nini kuhusu tuhuma hizo.
Unamjua sepp blatter???Well said, nimekupata vizuri sana mkuu - narudia kusema kwamba sio kwamba namtetea Malinzi na kundi lake - mkuu mimi binafsi nimefanya kazi na Govt Agencies za wenzetu weupe si rahisi kukwapua fedha zao bila ya kubainika, wako makini kweli kweli, sasa swali? Unakuwaje FIFA isewe na wasi wasi na Malinzi na kundi lake, kumbuka FIFA wanatoa fedha nyingi kwenye masuala ya kuendeleza mpira nchini - sasa iweje tena kwa sisi kudai kwamba Malinzi na wenzake ni wezi wa kutupwa, kisa? Eti wamekwapua fedha za michango ya Serengeti Boys, kuna ukweli gani katika madai hayo kama si majungu na fitina za kujaribu kutafuta sababu za kumuengua Malinzi hasiwanie kiti cha Uongozi wa TFF - kwa nini msiwachie wapiga kura ndiyo wachague mgombea wanaye mtaka wao, yaani masaa yote maadui wake wanatumia vyombo vya habari ku-demonise binadamu wenzao - hivi inaingilia akilini kwamba Malinzi atakimbilia kukwapua michango ya Serengeti Boys yaani akose chembe ya Uzalendo, hivi Malinzi ana njaa ya kufikia kujidhalilisha kweli? Personally I don't think so, if anything angekimbilia fedha za FIFA ambazo zilikuwa ni nyingi ukilinganisha na za Serengeti Boys.
Watz tuna huruma za ajabu sana.Kwahiyo mtu anafoji na kuiba pesa huku soka tunazidi kushuka kiwango wewe unaona sawa tu?nadhani wewe ulijui soka na hata huna uchungu nalo utakuwa mshabiki wa bongo flava huku sio kwako mkuu.
If that the case, let it beMkiingilia uchaguzi fifa inapiga kitanzi
Halafu point yako ingemtoa Malinzi knockout kwenye kampeniLakini.sababu si inafahamika jamaa wapo mahabusu.hawakuwepo kwa kupenda.na wale si wakosefu.ni watuhumiwa.
mkuu wale vijana wa serengeti boys hawajapewa stahiki zao mpaka leo
Angalia yule nahodha anajitibia mwenyewe mguu ambao kaumia akiwa na timu ya Taifa
nilimsikia mwesiga anasema zile pesa walienda kulipia deni wanalodaiwa na TRA ,ndiyo maana hawakuwapa stahiki zao wachezaji
Ok!Waje tu hao FIFA, hapa kazi tu
Wame audit pesa za walizowapa, au hujui TBL alimtoa Serengeti Breweries kwa kuingiza kitita kinono cha zaidi ya 5 bil !?TBL ndiyo wana -audit TFF?
Hafungiwi mtu, hata wao corruption imewagharimu. Sepp na katibu wake wapo wapi ?Naomba FIFA waje na watufungie hata miaka saba tu ili tutulie na tujipange vema.
mbona ni rahisi sana, hiki ndio kipindi cha mavuno malinzi wametuma rushwa kwa wajumbe ili wawachague katika uchaguziMkuu siyo kwamba namtetea Malizi na kundi lake, ninacho tilia shaka ni timing - kwa nini tuhuma hizi zijitokeze kwa kasi kubwa wakati wa maadalizi wa uchanguzi - kwa nini kipindi chote cha Uongozi wa Malizi watu walikuwa wamekaa kimya, sikuwahi kusikia kwamba Polis/Upelelezi au PCCB amekwenda kuhojiwa na taasisi hizo - WHY NOW? Kwa maneno mengine kwa nini wahibuke na tuhuma lukuki at the eleventh HOUR??
Iweje taasisi zetu zizinduke kutoka kwenye usingizi wa pono na kumkaba koo Malizi na kundi lake wakati wakiwa kwenye maadalizi ya uchaguzi, hii kama sio mizengwe tuiteje - tukiendelea kuendesha taasisi ya kuendeleza soka nchini kama vyama vya siasa basi Tanzania itabaki wasindikizaji wa mataifa mengine kimpira - Watanzania majungu, fitina na wivu vimetuzidi sana.
Hapa kuna tatizo mahali, kwanini iwe kutuhumiwa tu unapoteza haki zako nyingine za kiraia? Hivi kwanini usiangeandaliwa utaratibu akasailiwe huko huko mahabusi? Simuungi mkono Jamal lakini ni vema akatendewa haki.Malinzi aliyumia mbinu aliyotumia Mkuu Lowasa kuwa na wajumbe watiifu katika uchaguzi,na alikuwa anaenda kushinda kwa kishindo
mbona ni rahisi sana, hiki ndio kipindi cha mavuno malinzi wametuma rushwa kwa wajumbe ili wawachague katika uchaguzi
Hiki kitaasisi magufuli akifungie tuu ni useless bora tusitambulike na FIFA ila sio kua na wanakamati na viongozi mbumbu wenye maslahi binafsindugu amini usiamini hakuna uchaguzi ,naona kabisa hii tume ya uchaguzi TFF ilipangwa uwabebe akina Malinzi,inavyoonesha hawa wajumbe 4 kesho na wao watabandika matokeo yao ya usahili mbali na yale ya mwenyekiti