Ziara hii ya Waziri Mkuu mbona haina utulivu?

Ziara hii ya Waziri Mkuu mbona haina utulivu?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Msafara wa Waziri Mkuu wiki hii hapa Iringa umekuwa si wa kawaida.

Si wa kawaida kwa kuwa tumezoea viongozi wa kitaifa wakianza Ziara kwa Mkoa fulani, huifanya yote mpaka imalizike.

Lakini nahisi waliopanga Ziara ya Waziri Mkuu kwenye Mkoa wa Njombe hawajaipanga kiumakini.

Juzi Waziri Mkuu alipita hapa ikisemwa anatokea Njombe kwenda Dodoma. Jana alipita tena ikisemwa anatokea Dodoma kwenda Njombe kuendelea na Ziara ya Mkoa wa Njombe.

Leo inaonesha alitakiwa awe Manda bandarini huko Ludewa, na inasemwa kuwa watu walikuwa tayari wamekusanyika ,lakini tena inasemwa anarudi tena Dodoma.

Nani ameipanga hovyo hii Ziara ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kiasi kwamba inaonekana haina utulivu?
 
Hivi nyie watu mbona mna Mambo ya ajabu sana ni kwa nini mnatia hasira nyie kwa hiyo mnataka kumpangia waziri mkuu nia yenu ni nini maana naona sijui mnataka kusikia Tanzania imekuwa ya ajabu sana hii miaka.
 
Hivi nyie watu mbona mna Mambo ya ajabu sana ni kwa nini mnatia hasira nyie kwa hiyo mnataka kumpangia waziri mkuu Nia yenu ni nini maana naona sijui mnataka kusikia Tanzania imekuwa ya ajabu sana hii miaka
Mimi napingana na wewe. Tanzania haijawa ya ajabu hata mara moja bali kuna watu wamefanya na wanafanya Tanzania ionekane ya ajabu.
 
Back
Top Bottom