Ziara hii ya Waziri Mkuu mbona haina utulivu?

Ziara hii ya Waziri Mkuu mbona haina utulivu?

giphy.gif
 
Msafara wa Waziri Mkuu wik hiii hapa Iringa umekuwa si wa kawaida.

Si wa kawaida kwa kuwa tumezoea viongozi wa kitaifa wakianza Ziara kwa Mkoa fulani, huifanya yote mpaka imalizike.

Lakini nahisi waliopanga Ziara ya Waziri Mkuu kwenye Mkoa wa Njombe hawajaipanga kiumakini.

Juzi Waziri Mkuu alipita hapa ikisemwa anatokea Njombe kwenda Dodoma. Jana alipita tena ikisemwa anatokea Dodoma kwenda Njombe kuendelea na Ziara ya Mkoa wa Njombe.

Leo inaonesha alitakiwa awe Manda bandarini huko Ludewa, na inasemwa kuwa watu walikuwa tayari wamekusanyika ,lakini tena inasemwa anarudi tena Dodoma.

Nani ameipanga hovyo hii Ziara ya Mheshimiwa Waziri Mkuu kiasi kwamba inaonekana haina utulivu??
Hivi ni kwa nini waTanzania mnapenda sana maneno ya kinafiki nafiki? Inakusaidieni nini?
 
Hivi ni kwa nini waTanzania mnapenda sana maneno ya kinafiki nafiki? Inakusaidieni nini?
Sasa hapo unafiki upo wapi?

Au unadhani anatumia hela zake za mfukoni na siyo kodi yetu?

Hao waliopanga hiyo Ziara wanajua gharama za mafuta toka Njombe - Iringa mara sita?

Au hujui kama msafara ni gharama?
 
Back
Top Bottom