Uchaguzi 2020 Ziara ya Dkt. Magufuli Kilimanjaro imebeba ajenda za msingi

Huyu mgombea wa ccm ni mbaguzi. Na kutokana na chuki zake binafsi tu dhidi ya wachaga amewatumbua sana wachaga ktk kipindi chake Cha miaka 5.

Na huku tulijiqpiza tangu Xmas ya kwanza tulipo mgundua kuwa ana chuki nasi kuwa tutamuadhibu!!!
Haya! Kupanga ni kuchakua!
 
Na Thadei Ole Mushi.

Watu wa Kilimanjaro sio wajinga kiasi hicho, watamchagua Rais Magufuli kwa Kura nyingi Sana kuliko wagombea wengine wa uraisi. Twende sawa na agenda zetu..
Hongera Sana Rais wetu kwa kazi kubwa unayotufanyia Watanzania. Mungu aendelee kukupa nguvu. Kura zote safari hii za kwako hapa Kimanjaro na kwa CCM, tumeamua kwa hakika. Mwenyewe umejionea
 
Huyu mgombea wa ccm ni mbaguzi. Na kutokana na chuki zake binafsi tu dhidi ya wachaga amewatumbua sana wachaga ktk kipindi chake Cha miaka 5.

Na huku tulijiqpiza tangu Xmas ya kwanza tulipo mgundua kuwa ana chuki nasi kuwa tutamuadhibu!!!
Chuki hiyo unayo wewe binafsi moshi na kilimanjaro kwa ujumla tutamchagua jpm .mitano tena kwa baba mwenye nyumba.
 
Ndo ivyo chagua diwani,mbunge na rais kutoka ccm ili upate maendeleo ya kweli acha na huyo tapeli wenu lissu
 
Huyo ndiye Rais Magufuli kipenzi cha Watanzania
 
Kuhusu FAO la kujitoa je?

Kwa Nini wabunge walipwe pension zao zote halafu wafanyakazi wafanyiwe figusu?

Wabunge wanapewa pension, yote na kwa Kodi za wananchi...Wakati 😰 wafanyakazi wanaporwa haki zao, akiba zao.

Mtu mkataba imeisha au amefukuzwa kazi...kwa Nini asipewe hela zake akajiajiri?

Kwani Ni lazima aajiriwe maisha yake yote? CCM inaleta akili za kitumwa, slavery.

Kikwete na MKAPA walilipa FAO la kujitoa

Kwa Nini Magufuli alifuta, hizi Pesa za NSSF na PSSSF anapeleka wapi?

Kama mtu sio kilaza, aje na hoja
 
Hio ndo nature ya siasa ulimwenguni hata nchi zilizoendelea... lazima ufanye lobbying kwa mamlaka ya juu yako iwe diwani kwa mbunge, mbunge kwa waziri then kwa Rais yoyote atayemaliza shida yako sawa tu zaidi ya hapo utakua unafanya harakati tu
 
Hio ndo nature ya siasa ulimwenguni hata nchi zilizoendelea... lazima ufanye lobbying kwa mamlaka ya juu yako iwe diwani kwa mbunge, mbunge kwa waziri then kwa Rais yoyote atayemaliza shida yako sawa tu zaidi ya hapo utakua unafanya harakati tu

..kwenye nchi za wenzetu wana-lobby with leverage.

..yaani kunakuwa na nipe-nikupe, siyo hapa kwetu Raisi "asipojisikia" kupeleka mradi eneo fulani "imekula" kwa wananchi.

..mahusiano ya wabunge / bunge kwa upande mmoja na raisi / serikali kwa upande kwa hapa Tz hayaruhusu lobbying kufanyika.

..Kinachofanyika hapa Tanzania ni submission kwa Raisi ili kupata maendeleo kitu ambacho sio sahihi.

..kuna ulazima wa kufanya UGATUZI wa mamlaka ili kuondoa mfumo wa Uraisi wa " Kifalme " na Kiimla.
 
Huo uwongo wenu wa chadema mwisho wenu ni October
Kumbe Watanzania wote walioporwa haki wanakuwa Chadema, kumbee

Watu wote TANAPA iliowauwa Ni Chadema kumbee

Bureau De Change zote Ni za Wanachadema

MO DEWJI NI Chadema

Manji Ni Chadema

Wafanyakazi wote walioporwa haki za FAO LA KUJITOA NI Chadema

Kumbeee..Ni hivyo

Sasa wafanyakazi wanyonge waliokosa nyongeza ya mishahara Ni Chadema.

Basi nyie CCM NDIO mmewafukuza ili wawe Chadema...

Hongera Sana Bia Yetu.

Umewafumbua Watanzania.
 
Hio "nipe nikupe" kwenye siasa/uongozi/kushinda dola unadhani utampa nini Rais especially kama mpo chama tofauti?
 
It shows that, you do not know the meaning of leverage.
 
Ni mara ya pili tu anafika Kilimanjaro tangu 2015 unafikiri mtu huyu ana agenda ya maana K'Njaro?
 
Najua unatafuta teuzi.

Bahati mbaya umechelewa sana.

Wachagga huwajui uliza Davis Mosha.

Hutaamini kinachoenda kutokea, jipe muda.
 
Kodi ninayolipa

Ili akule bure, alale bure, atibiwe bure, etc etc
Umepotea njia mkuu... hapa tunaongelea 'nipe nikupe' kati ya viongozi mfano Rais na Mbunge, Mbunge na Waziri etc, sio kati ya wananchi na Rais
 
Hio "nipe nikupe" kwenye siasa/uongozi/kushinda dola unadhani utampa nini Rais especially kama mpo chama tofauti?

..hukunisoma vizuri.

..ngoja nikupe mfano ktk demokrasia zilizoendelea.

..Kunaweza kuwa na mswada au sheria ambayo inahitaji kupigiwa kura na wabunge.

..Sasa Raisi na Serikali lazima washawishi idadi ya kutosha ya wabunge ili mswada au sheria ipite.

..Wabunge nao wanachomeka mambo / miradi yao kwamba ili wapitishe mswada basi wanahitaji kitu[mradi...] fulani toka serikalini / kwa Raisi.

..Ili hilo litokee ni lazima kuwe na mfumo wa utawala ambao umetenganishe mihimili ya Mahakama, Bunge, na Serikali.

..Mfumo wa utawala ambapo wananchi waliochagua chama cha upinzani wanakuwa watazamaji, au wanapata "makombo", ktk miradi ya maendeleo siyo mzuri, na ni wa KIBAGUZI.
 
Acha uongo.

Pindi Lissu anatoka Rombo, alisimamishwa Marangu, wamama walikuwa na Masale barabarani.

Mbowe hai kakarbishwa na masale mara nyingi sana.

Sijui hizi bongo zenu zikiwa Lumumba huwa zipoje, Duh!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…