Uchaguzi 2020 Ziara ya Dkt. Magufuli Kilimanjaro imebeba ajenda za msingi

Huyu mgombea wa ccm ni mbaguzi. Na kutokana na chuki zake binafsi tu dhidi ya wachaga amewatumbua sana wachaga ktk kipindi chake Cha miaka 5.

Na huku tulijiqpiza tangu Xmas ya kwanza tulipo mgundua kuwa ana chuki nasi kuwa tutamuadhibu!!!
Haya! Kupanga ni kuchakua!
 
Na Thadei Ole Mushi.

Watu wa Kilimanjaro sio wajinga kiasi hicho, watamchagua Rais Magufuli kwa Kura nyingi Sana kuliko wagombea wengine wa uraisi. Twende sawa na agenda zetu..
Hongera Sana Rais wetu kwa kazi kubwa unayotufanyia Watanzania. Mungu aendelee kukupa nguvu. Kura zote safari hii za kwako hapa Kimanjaro na kwa CCM, tumeamua kwa hakika. Mwenyewe umejionea
 
Huyu mgombea wa ccm ni mbaguzi. Na kutokana na chuki zake binafsi tu dhidi ya wachaga amewatumbua sana wachaga ktk kipindi chake Cha miaka 5.

Na huku tulijiqpiza tangu Xmas ya kwanza tulipo mgundua kuwa ana chuki nasi kuwa tutamuadhibu!!!
Chuki hiyo unayo wewe binafsi moshi na kilimanjaro kwa ujumla tutamchagua jpm .mitano tena kwa baba mwenye nyumba.
 
..Suluhisho ni kupeleka madaraka kwa WANANCHI.

..Hii habari ya kuwa ombaomba kwa Raisi ndiyo inayochelewesha maendeleo.

..Wananchi wa Kilimanjaro walichagua wapinzani baada ya kuona wabunge wa CCM na serikali zao hawana msaada kwao.

..Ni makosa makubwa sana kuwa na mfumo ambao Raisi ndiye funguo au kufuli la maendeleo ya eneo husika.

..Yaani wabunge nchi nzima wote wakapige magoti mbele ya Raisi? Je, nchi hii ni ya Kifalme au ni Jamhuri?
Ndo ivyo chagua diwani,mbunge na rais kutoka ccm ili upate maendeleo ya kweli acha na huyo tapeli wenu lissu
 
Na Thadei Ole Mushi.

Watu wa Kilimanjaro sio wajinga kiasi hicho, watamchagua Rais Magufuli kwa Kura nyingi Sana kuliko wagombea wengine wa uraisi. Twende sawa na agenda zetu....

1. Kilimanjaro ina makabila mawili makubwa, Wachaga na wapare. Kwa silka ya makabila haya yapo profit oriented. Makabila haya haswa wachaga ni opportunist in nature.

Kuwa opportunist sio kosa au kitu kibaya kwa Kiingereza wanaelezewa watu wenye tabia hiyo kuwa huwa kila fursa inayojitokeza mahali huwa inatumika effectively ( *Opportunists are people who see a chance to gain some advantage from a situation,an opportunist seizes every opportunity to improve things for himself* )

Ndio maana wanakuambia kuwa ukiona mahali hayupo mchaga ondoka hakuna fursa Wala fedha.

Mwaka 2015 kwa jinsi Hali ya Mambo yakivyokuwa waliona kabisa kuwa Edward Lowassa atakuwa Rais, wakaamua kuside nao ili mambo yao yaende. Baada ya Uchaguzi hawakuamini kilichotokea.

2020 wanajua wazi kuwa uelekeo upo wapi leo kuanzia Mwanga Hadi Moshi mjini km 80.7 watu walisimama na majani ya Masale Kumpokea Rais Magufuli akitokea Same mkoani Kilimanjaro alikofanya mkutano Jana.

Kitendo hicho kimemgusa Sana Rais Magufuli na kwenye hotuba yake amerudia zaidi ya Mara 20 kuwa hakuwahi kupata Mapokezi makubwa kiasi hiki popote na haswa Mkoa wa Kilimanjaro.

Jani la *Isale* Lina maana nyingi lakini maana kubwa zaidi hutumika kumpokea mtu mwenye heshima na kuomba msamaha kwa watu waliokoseana. Kiutamaduni wa Kabila letu ukiombwa msamaha na Jani Hilo huna budi kuutoa msamaha huo. Rais Magufuli kalizungumzia Jani Hilo Mkoani hapa Kilimanjaro. Na amesema amesameheana na watu wa Kilimanjaro kwa makosa waliofanyiana mwaka 2015.

2. *Win win situation* nimeielezea Sana. Mara nyingi Rais Magufuli anasema kwenye Kampeni zake nichague nikuletee maendeleo. Hili halifichi huwa analisema hadharani. Mkoa wa Kilimanjaro una agenda nyingi ambazo zinatakiwa ziende ambazo zimekuwa haziendi.

Tuna Mambo makubwa matatu ambayo bila kura za kutosha tutaweza kuchelewa Sana kuvipata. Moja Moshi kupata hadhi ya Jiji. Hakuna mtu asiyejua faida za Jiji. Kihistoria Moshi ni mojawapo ya miji mikongwe Sana, kutanguliwa na Miji mingine kuwa Jiji ni aibu kubwa. Moshi ina Vigezo vyote kuwa Jiji. Watu wa kupush hili ni Mbunge anayeweza kufanya lobbying. Ni Dhahiri tukitaka huu mji uwe Jiji hata Kesho kutwa ni kuichagua CCM tu.

Jambo la Pili kubwa lipo Jimbo la Vunjo ambalo wanahitaji Sana kuwa na Halmashauri yao. Rais Magufuli kalizungunzia hili Sana. Hapa panahitaji political will yaani maamuzi ya kisiasa. Vunjo ikipata Halmashauri itarahisisha kujiletea maendeleo kwa haraka sana. Mji Mdogo wa njia panda unakua kwa haraka sana Kama Vunjo ikifanikiwa kujinasua Moshi Vijijini itaharakisha sana maendeleo ya eneo hili.

Jambo la tatu Kuna issue ya Barabara ambazo kwa muda mrefu wabunge wa Upinzani wameshindwa kufanya lobbying ya kukamilishwa kwake. Barabara zote za Old Moshi, Barabara ya Mabogini ambayo ni Kero Sana eneo hilo. Rais Magufuli kaizungumzia Barabara hii. Nani anayeweza kupishana na bahati hii?

3. Mkoa wa Kilimanjaro niliwahi kusema umebeba Mzigo wa Misumari. Gunia lenyewe ni kuwa Jamvi la Wapinzani. Yaani Wapinzani wamekuwa wakitaka kwenda Bungeni lazima wapitie Kilimanjaro. Kwangu Mimi ninavyoona Upinzani umedumaza Sana maendeleo ya Kilimanjaro.

Kudumaza maendeleo sio kwamba maendeleo hayapo Bali yapo Ila yaliletwa na watu wengine na sio Wapinzani. Tulipo tumesimama hatuendelei mbele matokeo yake tunaanza kupitwa kimaendeleo. Mkoa wa Kilimanjaro haupaswi kuwa Kama ulivyo. Hata Rais Magufuli kasema Mkoa wa Kilimanjaro unajichelewesha wenyewe. Kwa nature ya Wapinzani wa Taifa hili si watu wa round table si watu wa kufanya Lobbying ni watu wa kupinga kila kitu. Mkoa wa Kilimanjaro mwaka huu watajitua gunia hili la Misumari libebwe Tena na Singida au Mbeya. Hatuhitaji wabunge wakupinga tu, tunahitaji wabunge wanaoweza kufanya lobbying ya kumfuata rais Ikulu na kumuomba maendeleo ya maeneo yetu.

Wabunge wetu wamekuwa wakitumia nafasi zao za kibunge kujenga mahekalu ya nyumba nyumbani kwao huku wananchi wakibakia kupanua vidole tu. We need to change this kwa miaka Mitano tu.

4. Pamoja na Mambo Mengine leo Jambo la kufurahisha zaidi ni Askofu Mkuu KKKT kutokea kwenye Uwanja Leo na kufanya Sala ya kuombea Taifa.

Askofu Mkuu wa KKKT Dr Fredrick Shoo ni mojawapo ya watu wenye influence Sana kisiasa Mkoa Kilimanjaro.

Dr Shoo kwa namna Moja au nyingine amekuwa ana misimamo mikali Sana kuhusu Siasa za Tanzania Ila Kitendo Cha yeye kuwepo Kwenye mkutano leo wachambuzi wa Mambo ya kisiasa wamelitafsiri tofauti Sana na ni kiashiria Cha Rais Magufuli kukubalika na Makundi yote hata wale wenye msimamo mkali.

Rias bado anaendelea na Mikutano Mkoani Kilimanjaro. Tuendelee kulijadili Mkoa wetu na mustakabali wa maendeleo yetu. Kwa kichaga Kuna msemo usemao Mangi akikutembelea ndio wakati wa kumueleza shida za eneo husika. Kilimanjaro na Magufuli....

Ole Mushi

0712702602
Kuhusu FAO la kujitoa je?

Kwa Nini wabunge walipwe pension zao zote halafu wafanyakazi wafanyiwe figusu?

Wabunge wanapewa pension, yote na kwa Kodi za wananchi...Wakati 😰 wafanyakazi wanaporwa haki zao, akiba zao.

Mtu mkataba imeisha au amefukuzwa kazi...kwa Nini asipewe hela zake akajiajiri?

Kwani Ni lazima aajiriwe maisha yake yote? CCM inaleta akili za kitumwa, slavery.

Kikwete na MKAPA walilipa FAO la kujitoa

Kwa Nini Magufuli alifuta, hizi Pesa za NSSF na PSSSF anapeleka wapi?

Kama mtu sio kilaza, aje na hoja
 
..Suluhisho ni kupeleka madaraka kwa WANANCHI.

..Hii habari ya kuwa ombaomba kwa Raisi ndiyo inayochelewesha maendeleo.

..Wananchi wa Kilimanjaro walichagua wapinzani baada ya kuona wabunge wa CCM na serikali zao hawana msaada kwao.

..Ni makosa makubwa sana kuwa na mfumo ambao Raisi ndiye funguo au kufuli la maendeleo ya eneo husika.

..Yaani wabunge nchi nzima wote wakapige magoti mbele ya Raisi? Je, nchi hii ni ya Kifalme au ni Jamhuri?
Hio ndo nature ya siasa ulimwenguni hata nchi zilizoendelea... lazima ufanye lobbying kwa mamlaka ya juu yako iwe diwani kwa mbunge, mbunge kwa waziri then kwa Rais yoyote atayemaliza shida yako sawa tu zaidi ya hapo utakua unafanya harakati tu
 
..kwenye nchi za wenzetu wana-lobby with leverage.

..yaani kunakuwa na nipe-nikupe, siyo hapa kwetu Raisi "asipojisikia" kupeleka mradi eneo fulani "imekula" kwa wananchi.

..mahusiano ya wabunge / bunge kwa upande mmoja na raisi / serikali kwa upande kwa hapa Tz hayaruhusu lobbying kufanyika.

..Kinachofanyika hapa Tanzania ni submission kwa Raisi ili kupata maendeleo kitu ambacho sio sahihi.

..kuna ulazima wa kufanya UGATUZI wa mamlaka ili kuondoa mfumo wa Uraisi wa " Kifalme " na Kiimla.
 
Huo uwongo wenu wa chadema mwisho wenu ni October
Kumbe Watanzania wote walioporwa haki wanakuwa Chadema, kumbee

Watu wote TANAPA iliowauwa Ni Chadema kumbee

Bureau De Change zote Ni za Wanachadema

MO DEWJI NI Chadema

Manji Ni Chadema

Wafanyakazi wote walioporwa haki za FAO LA KUJITOA NI Chadema

Kumbeee..Ni hivyo

Sasa wafanyakazi wanyonge waliokosa nyongeza ya mishahara Ni Chadema.

Basi nyie CCM NDIO mmewafukuza ili wawe Chadema...

Hongera Sana Bia Yetu.

Umewafumbua Watanzania.
 
..kwenye nchi za wenzetu wana-lobby with leverage.

..yaani kunakuwa na nipe-nikupe, siyo hapa kwetu Raisi "asipojisikia" kupeleka mradi eneo fulani "imekula" kwa wananchi.

..mahusiano ya wabunge / bunge kwa upande mmoja na raisi / serikali kwa upande kwa hapa Tz hayaruhusu lobbying kufanyika.

..Kinachofanyika hapa Tanzania ni submission kwa Raisi ili kupata maendeleo kitu ambacho sio sahihi.

..kuna ulazima wa kufanya UGATUZI wa mamlaka ili kuondoa mfumo wa Uraisi wa " Kifalme " na Kiimla.
Hio "nipe nikupe" kwenye siasa/uongozi/kushinda dola unadhani utampa nini Rais especially kama mpo chama tofauti?
 
It shows that, you do not know the meaning of leverage.
 
Ni mara ya pili tu anafika Kilimanjaro tangu 2015 unafikiri mtu huyu ana agenda ya maana K'Njaro?
 
Na Thadei Ole Mushi.

Watu wa Kilimanjaro sio wajinga kiasi hicho, watamchagua Rais Magufuli kwa Kura nyingi Sana kuliko wagombea wengine wa uraisi. Twende sawa na agenda zetu....

1. Kilimanjaro ina makabila mawili makubwa, Wachaga na wapare. Kwa silka ya makabila haya yapo profit oriented. Makabila haya haswa wachaga ni opportunist in nature.

Kuwa opportunist sio kosa au kitu kibaya kwa Kiingereza wanaelezewa watu wenye tabia hiyo kuwa huwa kila fursa inayojitokeza mahali huwa inatumika effectively ( *Opportunists are people who see a chance to gain some advantage from a situation,an opportunist seizes every opportunity to improve things for himself* )

Ndio maana wanakuambia kuwa ukiona mahali hayupo mchaga ondoka hakuna fursa Wala fedha.

Mwaka 2015 kwa jinsi Hali ya Mambo yakivyokuwa waliona kabisa kuwa Edward Lowassa atakuwa Rais, wakaamua kuside nao ili mambo yao yaende. Baada ya Uchaguzi hawakuamini kilichotokea.

2020 wanajua wazi kuwa uelekeo upo wapi leo kuanzia Mwanga Hadi Moshi mjini km 80.7 watu walisimama na majani ya Masale Kumpokea Rais Magufuli akitokea Same mkoani Kilimanjaro alikofanya mkutano Jana.

Kitendo hicho kimemgusa Sana Rais Magufuli na kwenye hotuba yake amerudia zaidi ya Mara 20 kuwa hakuwahi kupata Mapokezi makubwa kiasi hiki popote na haswa Mkoa wa Kilimanjaro.

Jani la *Isale* Lina maana nyingi lakini maana kubwa zaidi hutumika kumpokea mtu mwenye heshima na kuomba msamaha kwa watu waliokoseana. Kiutamaduni wa Kabila letu ukiombwa msamaha na Jani Hilo huna budi kuutoa msamaha huo. Rais Magufuli kalizungumzia Jani Hilo Mkoani hapa Kilimanjaro. Na amesema amesameheana na watu wa Kilimanjaro kwa makosa waliofanyiana mwaka 2015.

2. *Win win situation* nimeielezea Sana. Mara nyingi Rais Magufuli anasema kwenye Kampeni zake nichague nikuletee maendeleo. Hili halifichi huwa analisema hadharani. Mkoa wa Kilimanjaro una agenda nyingi ambazo zinatakiwa ziende ambazo zimekuwa haziendi.

Tuna Mambo makubwa matatu ambayo bila kura za kutosha tutaweza kuchelewa Sana kuvipata. Moja Moshi kupata hadhi ya Jiji. Hakuna mtu asiyejua faida za Jiji. Kihistoria Moshi ni mojawapo ya miji mikongwe Sana, kutanguliwa na Miji mingine kuwa Jiji ni aibu kubwa. Moshi ina Vigezo vyote kuwa Jiji. Watu wa kupush hili ni Mbunge anayeweza kufanya lobbying. Ni Dhahiri tukitaka huu mji uwe Jiji hata Kesho kutwa ni kuichagua CCM tu.

Jambo la Pili kubwa lipo Jimbo la Vunjo ambalo wanahitaji Sana kuwa na Halmashauri yao. Rais Magufuli kalizungunzia hili Sana. Hapa panahitaji political will yaani maamuzi ya kisiasa. Vunjo ikipata Halmashauri itarahisisha kujiletea maendeleo kwa haraka sana. Mji Mdogo wa njia panda unakua kwa haraka sana Kama Vunjo ikifanikiwa kujinasua Moshi Vijijini itaharakisha sana maendeleo ya eneo hili.

Jambo la tatu Kuna issue ya Barabara ambazo kwa muda mrefu wabunge wa Upinzani wameshindwa kufanya lobbying ya kukamilishwa kwake. Barabara zote za Old Moshi, Barabara ya Mabogini ambayo ni Kero Sana eneo hilo. Rais Magufuli kaizungumzia Barabara hii. Nani anayeweza kupishana na bahati hii?

3. Mkoa wa Kilimanjaro niliwahi kusema umebeba Mzigo wa Misumari. Gunia lenyewe ni kuwa Jamvi la Wapinzani. Yaani Wapinzani wamekuwa wakitaka kwenda Bungeni lazima wapitie Kilimanjaro. Kwangu Mimi ninavyoona Upinzani umedumaza Sana maendeleo ya Kilimanjaro.

Kudumaza maendeleo sio kwamba maendeleo hayapo Bali yapo Ila yaliletwa na watu wengine na sio Wapinzani. Tulipo tumesimama hatuendelei mbele matokeo yake tunaanza kupitwa kimaendeleo. Mkoa wa Kilimanjaro haupaswi kuwa Kama ulivyo. Hata Rais Magufuli kasema Mkoa wa Kilimanjaro unajichelewesha wenyewe. Kwa nature ya Wapinzani wa Taifa hili si watu wa round table si watu wa kufanya Lobbying ni watu wa kupinga kila kitu. Mkoa wa Kilimanjaro mwaka huu watajitua gunia hili la Misumari libebwe Tena na Singida au Mbeya. Hatuhitaji wabunge wakupinga tu, tunahitaji wabunge wanaoweza kufanya lobbying ya kumfuata rais Ikulu na kumuomba maendeleo ya maeneo yetu.

Wabunge wetu wamekuwa wakitumia nafasi zao za kibunge kujenga mahekalu ya nyumba nyumbani kwao huku wananchi wakibakia kupanua vidole tu. We need to change this kwa miaka Mitano tu.

4. Pamoja na Mambo Mengine leo Jambo la kufurahisha zaidi ni Askofu Mkuu KKKT kutokea kwenye Uwanja Leo na kufanya Sala ya kuombea Taifa.

Askofu Mkuu wa KKKT Dr Fredrick Shoo ni mojawapo ya watu wenye influence Sana kisiasa Mkoa Kilimanjaro.

Dr Shoo kwa namna Moja au nyingine amekuwa ana misimamo mikali Sana kuhusu Siasa za Tanzania Ila Kitendo Cha yeye kuwepo Kwenye mkutano leo wachambuzi wa Mambo ya kisiasa wamelitafsiri tofauti Sana na ni kiashiria Cha Rais Magufuli kukubalika na Makundi yote hata wale wenye msimamo mkali.

Rias bado anaendelea na Mikutano Mkoani Kilimanjaro. Tuendelee kulijadili Mkoa wetu na mustakabali wa maendeleo yetu. Kwa kichaga Kuna msemo usemao Mangi akikutembelea ndio wakati wa kumueleza shida za eneo husika. Kilimanjaro na Magufuli....

Ole Mushi

0712702602
Najua unatafuta teuzi.

Bahati mbaya umechelewa sana.

Wachagga huwajui uliza Davis Mosha.

Hutaamini kinachoenda kutokea, jipe muda.
 
Hio "nipe nikupe" kwenye siasa/uongozi/kushinda dola unadhani utampa nini Rais especially kama mpo chama tofauti?

..hukunisoma vizuri.

..ngoja nikupe mfano ktk demokrasia zilizoendelea.

..Kunaweza kuwa na mswada au sheria ambayo inahitaji kupigiwa kura na wabunge.

..Sasa Raisi na Serikali lazima washawishi idadi ya kutosha ya wabunge ili mswada au sheria ipite.

..Wabunge nao wanachomeka mambo / miradi yao kwamba ili wapitishe mswada basi wanahitaji kitu[mradi...] fulani toka serikalini / kwa Raisi.

..Ili hilo litokee ni lazima kuwe na mfumo wa utawala ambao umetenganishe mihimili ya Mahakama, Bunge, na Serikali.

..Mfumo wa utawala ambapo wananchi waliochagua chama cha upinzani wanakuwa watazamaji, au wanapata "makombo", ktk miradi ya maendeleo siyo mzuri, na ni wa KIBAGUZI.
 
Nina heshimu sana hoja iliyotolewa, ijapokuwa kwa uelewa wangu wa kawaida tu juu ya jamii za Wachagga, ni nadra sana kukuta majani ya aina ya "masale" kutumika ktk shughuli za kisiasa tena yakimhusisha mtu asiyekuwa wa kabila lao. Majani haya hutumika ktk shughuli zao za kiutamaduni tu.

Wewe chunguza, hakuna mbunge yeyote yule ktk majimbo yote ya Kilimanjaro ambaye amewahi kufanyiwa mapokezi kwa kutumia majani ya mmea huu. Kwa wale wenye ueelewa juu wa watu wa jamii hii, watatambua tu kwa vyovyote tukio hilo litakuwa limeratibiwa na "vyasaka" ili tu kuweza kumfurahisha "chasaka".
Acha uongo.

Pindi Lissu anatoka Rombo, alisimamishwa Marangu, wamama walikuwa na Masale barabarani.

Mbowe hai kakarbishwa na masale mara nyingi sana.

Sijui hizi bongo zenu zikiwa Lumumba huwa zipoje, Duh!
 
Back
Top Bottom