Ziara ya Rais Samia nchini Kenya, Mama anakosea

Ziara ya Rais Samia nchini Kenya, Mama anakosea

Kunawakati tunapaswa kujadili maswala ya kitaalaam kwa utulivu na weredi ,hadi nimetamani Jf ingelikuwa na kipengele cha mtu kuruhusiwa kujadili hoja kutokana na TAALUMA yake , hapa unakuta mtu kwakuwa tu anajua kusoma na kuandika anajikuta anajadili kilimo huku akiwa hata hajui utofauti wa aina za mbolea ,eneo la Uchumi ni pana Sana na siyo kila mbinu nilazima ianze chino ,zingine ukija kwenye kuwagawia wa NDANI unakuta tayari ushafanya mlipuko mkubwa na wenye tija .

Tanzania iko hapa ilipo kwa makosa mengi yakiwemo tunayojihubiria hapa.

Watu wenye fikra za aina wzeeka ndiyo huwa mnakuwaga wachawi tu [emoji12] , ukiona mtoto wa yuko smart kuliko wa kwako unaona the best option ni kumdedisha tu au umnyime baadhi ya mahitaji ambayo yqtamfanya asongembele zaidi kwakuhisi wakakwako watapoteza u ora nakudharilika which is not true badala ya kufurahia uwepo wake na huku ukiangalia namna nzuri ya kuutumia uwepo wake ili na wa wajamii yako wawe bora hata kumpita .

Hii tabia yakukumbatia tulivyonavyo haiajawahi kuleta matokeo chanya zaidi ya kutudumaza tu kifikra .

Kanuni ya Biashara inatutaka tuuze tulivyonavyo huku tukizielekeza faida kwenye vitu vitakavyotuzidishia faida maradufu .

Kwa wasiyojua sera yetu ya Uchumi haiwezi kutatuliwa kwa uwepo wa gas bali maboresho mazito ya sera yetu ya elimu (kutoka kwenye elimu ya kukarili kwenda kwenye elimu ya utambuzi (creming education to cognitive education) elimu itakayohakikisha haizalishi wategemezi kwa Taifa kama ilivyo sasa kundi la kuanzia darasa la saba kuwa mzigo tu kwa Taifa , wahitimu wa kidato cha nne kutokuwa na sifa siyo tu za kuajirika lakini hata tu wenyewe wakawa hawana uwezo wakujiajiri nje ya kuwa na sifa za nyongeza achilia mbali cheti cha muhitimu wa chuo kikuu kukosa thamani ya kutumika kama collateral [emoji12] itakayomuwezesha walau kukopesheka na kupata mtaji wa kuanzishia ile taaluma ambayo serikali imemuidhinishia ufaulu (refer to China).

Mama anaendelea kufanya vizuri sana hebu tujipe utulivu na tumpe muda .

Tusiishi kwa kukarili ,Dunia inakwenda kasi sana .
 
Hili suala la kuweka restriction za corona na kujipendekeza kwa watu sijajua mshauri ni nani, inatuletea picha ya udhaifu! Akimaliza hii ya Magufuli, itakuwa ngumu sana mimi kumpigia kura, niwe mkweli, nachukia udhaifu dhaifu kwenye uongozi! Tunarudi tena enzi za msoga sasa..
Ustaarabu sio udhaifu, na Kiburi sio uimara.
 
Kwani kwa wakati huu ambao hawajaunganishiwa hizo ajira ziko wapi?
Huwaoni vijana waliowengi wakiwa watazamaji?
Tatizo sio kuuza gesi bali mazingira yametengenezwaje.
Hata sasa mbona kama wewe sio mwana siasa ni mtazamaji na msikilizaji wa maamuzi ya akina kibajaji?
Nadhani hapo kwenye kibajaji mmenielewa
 
Uliposema viwanda na gesi, nimekumbuka, Dangote alinyimwa gesi akaamua kutumia Makaa, wakamkatalia pia.

Bakhresa, akanyimwa gesi pale Mwandege.

Gesi ya serikali iliyobaki imesambazwa majumbani kwa staffs wa TPDC na Kinyerezi Tanesco.

Ngoja tuone viwanda vyetu hivi vya mikocheni(TPDC) na Kinyerezi vitakavyoshindana na vile vya urithi vya Kenya vitakavyozalisha kwa urahisi wa gesi yetu wenyewe.
hawa hawakunyimwa mkuu. hivi kwa akili ya kawaidavtu serikali inaweza mmnyima muwekezaji gesi. issue ni kuwa hawa walitaka gesi kwa bei ya chini mno ndio waliposhindwana. katika biashara hivi ni vitu vya kawaida sana.
 
Kinachonishangaza Zanzibar waliondoa maswala ya gesi na mafuta kuwa siyo vitu vya muungano lakini leo hii mzanzibar anaenda kusaini mkataba wa gesi ya Tanganyika hii siyo halali
Interesting!!
Kazi kweli kweli na huu ni mwanzo mpya si kwamba kazi inaendelea ati .....
This is the new beginnings of almost everything which runs Tanzanian economical politics .... Oh LORD have mercy.
 
"Najua mtanikumbuka kwa mazuri tu na si mabaya"
(Mwenda zake 2021AD)
Kwahili kweli tutamkumbuka JPM

Mama Samia asijilegeze kwa Wakenya, Hawa watu sio wazuri wanataka tuendelee kuwa soko la viwanda vyao ilihali products zingine tunaweza kuzitengeneza wwnyewe

Mama awe makini sana na aendelee kuwapiga pini kama JPM alivyofanya.

Shauri yetu Wadanganyika
 
Kwahiyo kuwa pushover ndio ustaarabu sio?
Tembea nchi za wenzetu ujionee, tatizo mmezaliwa Mbalizi, mkakulia ilula na hata passport ya kusafiria huna, huwezi jua nchi za wenzetu wanaishije. Watanzania mnahisi tuko zama za ujamaa kwamba uchumi wetu ni wa state owned control. Tembeeni muone hata China huko wameingia mikataba mingi kuuza bidhaa zao nje ndio umeona maendeleo. Huwezi kuwa na bidhaa ukakaa nayo eti kisa mtu atakupita uzalishaji.
 
Mwanamke huongozwa na mwanaume!eti leo hi mwanamke anaongoza wanaume zaidi ya milion,kadili muda unavyozidi kwenda tutegemee kufeli zaidi
Hayo maneno ya mkosaji !!fikra za miaka ya 50!!, wanawake wameongoza wazungu na kuleta maendeleo makubwa itakuwa kwa mwafrika, tena mtanzania?!!huyo mwanaume aliyeongoza miaka mitano , maendeleo gani ameyaleta?hao kina mseveni, mugabe, derby, biya, sasongweso zaidi ya miaka 30, madarakani walifanya nini?!acheni hizo muhukumuni mtu kwa uwezo wake na sio JINSI, yake.MAMA KANYAJA TWENDE,
 
Nashangaa wanaosema viwanda havijaunganishwa. Nenda kaulize Azam mwandege na viwanda vya bidhaa mbalimbali ambavyo viko barabara ya kwenda mkuranga vinatumia nini kama siyo gesi. Mpaka maeneo y mwandege zimewekwa outlets za gesi kwa ajili ya viwanda vinavyotegewa kujengwa kwamba siku vikijengwa tu wanaunga moja kwa moja kwenye gesi
 
Kwahili kweli tutamkumbuka JPM

Mama Samia asijilegeze kwa Wakenya, Hawa watu sio wazuri wanataka tuendelee kuwa soko la viwanda vyao ilihali products zingine tunaweza kuzitengeneza wwnyewe

Mama awe makini sana na aendelee kuwapiga pini kama JPM alivyofanya.

Shauri yetu Wadanganyika
Siasa za ki magufuli za kishamba zilishapitwa na wakati huu sio muda wake, haya miaka yote hiyo alifanya figisu nini cha maana alikipata?waulize wakulima wa mikoa ya kaskazini nini kiliwapata baada ya mazao yao kukuosa soko, kisa wakenya hawaji kuyanunua!!nchi ya tano duniani kwa kuwekeza Tz, badala ya kuweka mikakati ili uone na wewe unatoka vipi, unawaza kumkwamisha!!sasa rafiki yako awe burundi kuna faida gani hapo?
Mama hana mawazo hayo ya kizamani, hivyo ndio maana umeona heshima aliyopewa, mtu ameajiri watu 50, 000 nchini kwako bado, unamuona tishio?
 
Nashangaa wanaosema viwanda havijaunganishwa. Nenda kaulize Azam mwandege na viwanda vya bidhaa mbalimbali ambavyo viko barabara ya kwenda mkuranga vinatumia nini kama siyo gesi. Mpaka maeneo y mwandege zimewekwa outlets za gesi kwa ajili ya viwanda vinavyotegewa kujengwa kwamba siku vikijengwa tu wanaunga moja kwa moja kwenye gesi
Usitufanye watoto wadogo, hiyo gesi hapo azam mwandege imewekwa lini?hadi jana 4.5.2021, cjaiona?kwa mbagala kiwanda walichounganishiwa gesi kilikuwa ni kile cha KTM, pale misheni tu.hapo mwandege hadi jana kiwanda kinatumia umeme tu, tena ameunganishiwa line kubwa yake tu.
 
Nilisikia kwenye hotuba gesi huwa inasafirishwa kwa njia ya barabara kwenda kenya hivyo gharama inakuwa kubwa ndio maana wameomba bomba.
Kumbe biashara ilianza muda mrefu, kitakachobadirika ni jinsi ya kuisafirisha
Nawaomba mkaisikilize tena ile summury ya hotuba .
Tukumbuke Kenya imetuzidi uchumi kwa 80% .
Elfu 10000 ya Kenya more than100000 ya Tz.
Urusi huuza gesi ulaya na china ila hawana viwanda kama ulaya, Iran huuza gesi China ila hawana viwanda kama China.
Japan ilikuwa inatumia resource za mataifa mengine kuzakisha bidhaa na kuzirudisha bidhaa kuwauzia hao wenye material, Japan iliongoza viwanda bara Asia.
Makaa ya mawe ya Njombe yanasafirishwa hadi Nairobi lakini Njombe hakuna kiwanda chochote kinachotumia makaa ya mawe.
 
Hili suala la kuweka restriction za corona na kujipendekeza kwa watu sijajua mshauri ni nani, inatuletea picha ya udhaifu! Akimaliza hii ya Magufuli, itakuwa ngumu sana mimi kumpigia kura, niwe mkweli, nachukia udhaifu dhaifu kwenye uongozi! Tunarudi tena enzi za msoga sasa..
Heri Mama kuliko Mwendazake hamtwambiii kitu kabisa ushamba na ulimbukeni tupa kuleeeee shimoni
 
Back
Top Bottom