Profesa Mutembei amesema, ziara hiyo ya siku tatu kuanzia tarehe 2 hadi 4 itatoa fursa zaidi kwa maendeleo ya uhusiano wa nchi hizo mbili, na kupanua ushirikiano wa kibiashara kati ya China na Tanzania.
Profesa Mutembei amesema, China ni rafiki mkubwa wa Tanzania, na nchi hizo mbili zina fursa isiyo na mwisho katika kukuza ushirikiano wa utamaduni, uchumi na diplomasia.
Amesema maingiliano ya elimu yamekuwa na nafasi muhimu katika ushirikiano kati ya Tanzania na China, na hivi sasa, Kiswahili kinatumika katika taasisi za kitaaluma za China, hali ambayo imehimiza ushirikiano wa kina wa kiuchumi kati ya nchi hizo mbili na uwekezaji wa China nchini Tanzania.
Ameongeza kuwa nchini Tanzania, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na Taasisi ya Confucius, pia vimekuza ipasavyo ushirikiano wa Tanzania na China katika nyanja za uchumi, utamaduni na kilimo.