Ziara ya ujumbe wa viongozi wa Afrika nchini Ukraine na Urusi yaonesha kuwa na Mafanikio

Ziara ya ujumbe wa viongozi wa Afrika nchini Ukraine na Urusi yaonesha kuwa na Mafanikio

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111441657192.jpg



Ujumbe wa nchi za Afrika ulioongozwa na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ulifanya ziara nchini Ukraine na Russia, na kukutana na viongozi wa pande hizo mbili ukitafuta njia za kutatua mgogoro huo ambao umekuwa na madhara kwa nchi mbalimbali za Afrika. Ujumbe huo ni moja ya juhudi za jumuiya ya kimataifa kujaribu kutafuta suluhisho la kidiplomasia la mgogoro kati ya Russia na Ukraine.

Rais Ramaphosa aliongoza ujumbe unaowakilisha sauti ya Afrika, ukiwa na maofisa waandamizi kutoka Misri, Senegal, Jamhuri ya Kongo, Comoro, Zambia na Uganda. Rais Ramaphosa alisema ziara ya ujumbe huo ilikuwa na malengo mawili. Lengo la kwanza ni kuzisikiliza pande zote mbili, na lengo la pili ni kuzifahamisha pande hizo kuhusu madhara ya vita hiyo kwa nchi za Afrika (na kwa uchumi wa dunia kwa ujumla), na hata kutoa pendekezo lenye hatua kumi la kukomesha mgogoro huo.

Nchi za magharibi zimekuwa zikitumia vyombo vya habari na majukwaa ya kidiplomasia kujenga sura mbaya ya Russia kuwa ni nchi korofi na inatakiwa kulaaniwa na dunia nzima. Lakini ukweli umeonesha kuwa mgogoro wa Ukraine na Russia ni suala lenye utatanishi mkubwa, na sio suala la kutupia lawama upande mmoja bila kujua mzizi wa mgogoro huo. Wakati dunia inaaminishwa kuwa ni mapambano kati ya Russia na Ukraine, lakini undani wake ni kuwa nyuma ya Ukraine kuna nguvu kubwa ambayo huenda ni chanzo cha mgogoro. Kwa hiyo uamuzi wa ujumbe wa Afrika kutaka kusikiliza pande zote mbili, kwanza ni jambo la kuonesha kuziheshimu pande zinazopambana, lakini pili linaonesha nchi za Afrika hazitaki kufanya maamuzi kwa kuambiwa au kulazimishwa, kama ilivyoonekana mwanzoni mwa mgogoro huu.

Pamoja na kuwa bara la Afrika si mhusika wa moja kwa moja kwenye mgogoro wa Russia na Ukraine, matokeo ya mgogoro huo kwa nchi za Afrika yamekuwa wazi kabisa makubwa na yameigusa karibu kila nchi ya Afrika. Rais Ramaphosa amewaambia marais wa Russia na Ukraine kuwa karibu kila nchi imeshuhudia kupanda kwa bei ya nafaka zinazoagizwa kutoka Russia na Ukraine, hasa ngano, lakini pia zimeshuhudia ongezeko kubwa la bei ya mbolea na kuathiri sana uwezo wa wakulima, na hata uchumi kwa ujumla.

Pamoja na ukweli kwamba ni mapema sana kuzungumzia matokeo ya ziara ya ujumbe huo, ni jambo la faraja kuona kuwa Afrika imetoa sauti yake na imetoa maoni yake. Rais Ramaphosa amewaambia wenyeji wake kuwa mgogoro huu una madhara makubwa kwa uchumi wa dunia na hauwezi kuendelea bila ukomo. Sauti ya Afrika kuhusu kutaka mgogoro huo ukomeshwe kwa njia ya amani, umekuja baada ya China, Uturuki na Vatican, kutoa mwisho na mapendekezo ya kutatua mgogoro huo.

Ni wazi kuwa kuna baadhi ya nchi zenye nguvu zinafurahia mgogoro huu, na inaonekana wazi kuwa zinapenda uendelee kuwepo. Tumesikia kuwa nchi hizo zinatoa silaha na kutaka mapambano yaendelee kwa kuwa sio wao wanaoumia au sio wao wanaathiriwa sana na mgogoro huo. Wanachukulia vita hii kama ni fursa ya kuonesha umwamba na kutanua eneo lao ushawishi. Upande wenye busara umekuwa ukitoa mwito wa kutafuta suluhisho la kidiplomasia la mgogoro huu, kwani ni wazi kuwa madhara ya mgogoro huu yataendelea kuwepo muda mrefu hata baada ya mgogoro kwisha. Ni kama alivyosema Rais Ramaphosa kila mgogoro una mwisho, ni bora mgogoro huu uishi mapema ili kupunguza madhara yake.
 
Wapiganapo mafahari, ziumiazo ni nyasi. Bahati mbaya waAfrika tunaangukia kwenye kila kibaya!

Cha kusikitisha, hatuoni kuwa ni alama ya kututaka tuamke, tujielewe, tujitegemee, bali tunawafuata waache kupigana ili waendelee kunufaika kwa uhitaji wetu! Hiyo ziara kama kawaida ya wanasiasa wa kutoka Afrika, wameenda kupiga pesa tu, hawana lolote!
 
Wangeanza na Sudan, Somalia, Ethiopia, Sahel nk za ndani ya Afrika ndio wajitanue kwenda bara ulaya tungeona kweli wanedhamiria amani.

Wameonekana hamna lolote "...concerned with their stomach infrustructure...."
 
View attachment 2664876


Ujumbe wa nchi za Afrika ulioongozwa na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ulifanya ziara nchini Ukraine na Russia, na kukutana na viongozi wa pande hizo mbili ukitafuta njia za kutatua mgogoro huo ambao umekuwa na madhara kwa nchi
Lakini Ukraine haikuanzisha vita Ukraine imevamiwa Urusi na shindwa kuelewa mwathiriwa wa Uvamizi anapelekewa lawama kwa kujitetea na wanaomsaidia silaha kujitetea ndio wanaoonekana wanachochea vita hivi huu ni unafiki wa aina gani?

Mlitaka Ukraine asijitete ili ardhi zake zichukuliwe kiulaini na na Zelesky aliyechaguliwa kidemocrasia angeshapinduliwa haraka mwanzo wa vita Zelesky aliomba mazungumzo ya amani na Putin lakini Putin alionekana hataki mazungumzo na anatoa masharti ya kuumiza na kuendelea kuvurumisha makombora yake Ukraine ili vita viishe ilitakiwa Urusi aanze kuondoa majeshi yake UKRAINE na kuacha kuishambulia Ukraine kwa sababu Urusi ndio mwanzilishi wa hii vita vya kichokozi
 
View attachment 2664876


Ujumbe wa nchi za Afrika ulioongozwa na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ulifanya ziara nchini Ukraine na Russia, na kukutana na viongozi wa pande hizo mbili ukitafuta njia za kutatua mgogoro huo ambao umekuwa na madhara kwa nchi
Putin aliingilia hotuba za viongozi wa Africa akionesha kutokubaliana na matakwa yao. Afrika imefanya politics just for politics sake na wametimiza tu hilo ili wasiambiwe kwanini hamkufanya lolote.

Putin kamwe hawezi kubadili msimamo wake kwa ushawishi wa waafrika! Vita ya Urusi na Ukraine itakwisha kwa intervention ya mataifa makubwa na ni pale Urusi itakapoishiwa nguvu au Putin kuondolewa kwa kifo au upinzani kutoka nchini mwake.
 
Back
Top Bottom