Ziara ya wanadiplomasia wa Afrika mkoani Hunan, China, kufungua fursa nyingi zaidi za kibiashara na kiuchumi

Ziara ya wanadiplomasia wa Afrika mkoani Hunan, China, kufungua fursa nyingi zaidi za kibiashara na kiuchumi

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
fbfc8cb57946428f8b4cee0a16c253b0.jpg


ffd455e7fa734dd48733fc6cf349003b.jpg


Na Pili Mwinyi

China na Afrika ni ndugu ambao wanafaana wakati wa dhiki na faraja, na uhusiano uliopo kati yao tunaweza kusema kwamba ni uhusiano wa kihistoria duniani.

Uhusiano huu mashuhuri ambao unajulikana vizuri na kwa mapana zaidi duniani, kutokana na umuhimu wake katika kuchangia mabadiliko ya pande mbili, umekuwa ukileta tija kubwa zaidi.

Na ndio maana wasomi, waandishi wa habari, wanadiplomasia, washauri, na hata watu wa kawaida pia wanaunga mkono ushirikiano kati ya China na Afrika.

Ili kuhakikisha ushirikiano huu unazidi kuwa imara hasa katika masuala ya uchumi na biashara, hivi karibuni, Julai 27 hadi 29, wanadiplomasia 25 kutoka nchi 15 za Afrika walitembelea eneo la majaribio la Mpango wa Kina wa Ushirikiano wa Kiuchumi na Kibiashara kati ya China na Afrika lililopo mkoani Hunan hapa nchini China.

Wakiwa huko, wanadiplomasia hao wameeleza imani yao kwa uchumi wa China na kusema wanatarajia kwamba utakuwepo uhusiano wa karibu zaidi wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi zao na China.

Ingawa tunafahamu kuwa dunia inakabiliwa na changamoto za aina mbalimbali likiwemo janga la UVIKO-19, lakini kilichowapa matumaini zaidi wanadiplomasia hao ni kwamba uchumi wa China bado unaendelea kuwa imara na soko la China linazidi kutoa fursa nyingi mbalimbali.

Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki, ambaye naye ni miongoni wa wanadiplomasia waliotembelea eneo hilo la kibiashara na kiuchumi, kwa upande wake alisema ushirikiano wa kibiashara na kiuchumi kati ya China na Afrika umekuwa ukiongezeka katika kipindi cha miaka 20 iliyopita, hivyo soko la China lenye wanunuzi bilioni 1.4 lina fursa nyingi kwa nchi zote za Afrika, na kwamba ana imani kutakuwa na fursa nyingi zaidi kwa Tanzania kusafirisha bidhaa nchini China, hasa bidhaa zenye thamani ya juu.

Hivi sasa Tanzania kupitia Wizara yake ya Kilimo imekuwa ikiweka kipaumbele katika kutafuta fursa mbalimbali za kuweza kusafirisha bidhaa zake za kilimo kwenye soko la China, hasa maparachichi, kwani soko hili linanunua bidhaa hii kwa fedha za Kimarekani zaidi ya dola milioni 108 kwa mwaka, hali ambayo inaonesha kuwa China ni soko la uhakika kwa wakulima wa Tanzania.

Kwa mujibu wa balozi Kairuki, eneo walilokwenda kutembelea la majaribio mkoani Hunan linaunganisha pamoja faida za bidhaa bora za kilimo za Afrika na uwezo wa usindikaji na usambazaji wa China, na kusaidia bidhaa za Afrika kuweza kuongeza thamani yake kulingana na mahitaji ya soko la China.

Eneo la majaribio ni mpango muhimu ulio chini ya “Miradi tisa” iliyotangazwa Novemba mwaka jana katika Mkutano wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika.

Maeneo haya mapya ya ushirikiano wa kibiashara, uwekezaji na ushirikiano wa mambo ya fedha kati ya China na Afrika hivi sasa yanaendelea kukuzwa ili kusaidia mageuzi na kuboresha zaidi ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizi mbili.

Kwa muda mrefu tumeshuhudia biashara na uwekezaji vikileta tija kubwa sio tu kwa watu wa China bali hata wa nchi nyingine zinazoendelea, kwa kutoa ajira na maisha mazuri.

Kwa mujibu wa Idara Kuu ya Forodha ya China, mwaka jana wa 2021, thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilipanda na kuwa dola bilioni 254.3 za Marekani, ikiongezeka kwa asilimia 35.3 kuliko mwaka wa nyuma yake, huku Afrika ikisafirisha bidhaa nchini China zenye thamani ya dola bilioni 105.9 ikiwa juu kwa asilimia 43.7.

Vilevile kuanzia Aprili hadi Mei 12, tamasha la manunuzi ya bidhaa za Afrika lililofanyika kwa mafanikio kwenye mtandao wa intenet, lilivutiwa na nchi 23 za Afrika, ambapo kupitia majukwaa na matangazo ya moja kwa moja kwenye mtandao, wanunuzi wa China waliweza kununua kwa urahisi zaidi bidhaa za Afrika kama vile kahawa ya Kenya na mvinyo wa Afrika Kusini.

Katika ziara yao hiyo ya siku tatu, mabalozi wa Afrika walitembelea maeneo muhimu na ya msingi ya eneo hilo la majaribio, pamoja na makampuni mbalimbali ambayo ni muhimu.
 
Siyo ya maharagwe soya now ni ziara ya fulsa, asee!.
 
Back
Top Bottom