ArD67
JF-Expert Member
- Nov 14, 2016
- 2,817
- 2,044
Hatupo tupo tu mkuu, kupanga ni kuchagua mkuu. Tulipanga kuanza hivi... hii ni vision yetu. Isome vyema historia ya hii nchi kwanza kabla hujaijaji kwa lolote lile.Wewe inafaa ikuingie kwamba humu hatupo ili tukusifie, ukiingia kwenye mitandao ya kijamii lazima uwe tayari kuambiwa chochote, kuwa tayari kuupokea ukweli japo mchungu. Binafsi kuna wakati Kenya huwa inapondwa humu, japo inaniuma lakini unakuta mengi hayo ni ya ukweli mtupu, inabidi kuyameza kimya kimya na kuendelea na maisha.
Uzalendo sio kutetea kila uchafu na udhaifu, bali kuyakubali hata kama kimya kimya na pia kusifia mazuri.
Bongo nimekatiza mikoa mingi sana hata zaidi ya wengi wenu, nimekula bata huko na pia kufanya shughuli za kibiashara. Kuna mengi mazuri, lakini pia kuna mapungufu mengi sana, hiyo nchi yenu ina kila sababu za kuwa kiongozi Afrika kiuchumi, kiviwanda na karibia kila kitu, lakini nyie mpo mpo tu kazi kutetea mapungufu na kuwapuuza wataalam wenu.
Watu wake, mila,tamaduni na desturi zao. Tawala zao kabla na baada ya ukoloni, jiografia yao, mazingira yao nk. Mngetujua msingetushangaa kwanini tukiwa wachanga tulijitoa ktk ukombozi wa wengine, kwanini tunasema "naomba" dukani huku tunalipa, asante huku tumetoa hela. Ujamaa hatukuuiga kutoka kwa Marx, tumezaliwa nao hata kabla ya ukoloni wa waarabu.
Hili ndilo taifa la Tanzania..... Hata hivyo umenena vyema sana mkuu. Mapungufu yapo, kila mahali, na kuyakubali ni hatua mojawapo ya kujisawazisha. Ila si kila nilionalo kuwa ni pungufu kwa Kenya lazima liwe kweli ni pungufu kwao,mila zao inaweza likawa si tatizo ktk hilo, vivyohivyo kwa Tanzania pia.
Wakenya walio wengi ni wafugaji, wala nyama kwa asili, tena si kama wasukuma, hawa ni kama wamasai, hata damu mbichi huliwa kwao. Tanzania ni kinyume cha hapo, ukitumia ubongo kidogo utaweza pata tofauti kati ya nchi hizi 2 ktk idara nyingi sana.
Anzia tu hapo, ktk ulaji wa nyama na damu. Ufanye utafiti kiutabibu, kibaiolojia, kiimani, kifizikia, kimazingiria, kihistoria, kinadharia nk. Kuna kitu utakibaini.
Umesema ulishalizunguka hili taifa, haya yote umeyashudia kwa macho yako. Utaifa wetu umo ndani ya misingi hiyo tuliyozaliwa nayo. Mungu ibariki Africa.