Ziara ya waziri wa China East Africa yaipa Tanzania viwanda 200

Hatupo tupo tu mkuu, kupanga ni kuchagua mkuu. Tulipanga kuanza hivi... hii ni vision yetu. Isome vyema historia ya hii nchi kwanza kabla hujaijaji kwa lolote lile.

Watu wake, mila,tamaduni na desturi zao. Tawala zao kabla na baada ya ukoloni, jiografia yao, mazingira yao nk. Mngetujua msingetushangaa kwanini tukiwa wachanga tulijitoa ktk ukombozi wa wengine, kwanini tunasema "naomba" dukani huku tunalipa, asante huku tumetoa hela. Ujamaa hatukuuiga kutoka kwa Marx, tumezaliwa nao hata kabla ya ukoloni wa waarabu.

Hili ndilo taifa la Tanzania..... Hata hivyo umenena vyema sana mkuu. Mapungufu yapo, kila mahali, na kuyakubali ni hatua mojawapo ya kujisawazisha. Ila si kila nilionalo kuwa ni pungufu kwa Kenya lazima liwe kweli ni pungufu kwao,mila zao inaweza likawa si tatizo ktk hilo, vivyohivyo kwa Tanzania pia.

Wakenya walio wengi ni wafugaji, wala nyama kwa asili, tena si kama wasukuma, hawa ni kama wamasai, hata damu mbichi huliwa kwao. Tanzania ni kinyume cha hapo, ukitumia ubongo kidogo utaweza pata tofauti kati ya nchi hizi 2 ktk idara nyingi sana.

Anzia tu hapo, ktk ulaji wa nyama na damu. Ufanye utafiti kiutabibu, kibaiolojia, kiimani, kifizikia, kimazingiria, kihistoria, kinadharia nk. Kuna kitu utakibaini.

Umesema ulishalizunguka hili taifa, haya yote umeyashudia kwa macho yako. Utaifa wetu umo ndani ya misingi hiyo tuliyozaliwa nayo. Mungu ibariki Africa.
 
China?
Viwanda vya kuzalisha nini?
Tuwe waangalifu hapa. We know Chinese.
Mpaka sasa wachina ndio wanaongoza hapa Dar kwa kuwa na utitiri wa viwanda bubu mitaani. Wanazalisha mpaka gongo na kuziweka kwenye pakiti za Viroba.
kweli mkuu viwanda 200? itawezeknaje kwa capital gani toka bajeti gani ya china
 
kweli mkuu viwanda 200? itawezeknaje kwa capital gani toka bajeti gani ya china
Wawekezaji 200 tu wakichina wenye mitaji yao, kila mmoja anaweza akajenga kimoja na tukawa tumevipata hivyo 200 vyote na kwa wakati. Nia na maamuzi tu ndo shida, ikiwepo vitapatina.
 
The high priest wa vijembe leo hii anakuwa askofu wa kutuambia ukweli mchungu. Ngoja nikuambie, watanzania hatuna shida na ukweli mchungu, rais Magufuli anatupa dose ya ukweli mchungu mpaka tunasahau njia ya kurudi nyumbani. Na siku hizi tumeshaanza kumuelewa elewa, tumejifunza jinsi ya kuumeza ukweli wake mchungu. Wakenya wengi wa humu JF hata huko uraiani hakuna wa kuwaabia watanzania ukweli mchungu, wote ni vijembe kashfa na mitusi. Na ukiangalia ndani utakuta hakuna kingine zaidi ya uwoga, hakuna kitu kinamuuzi mkenya kama akisikia Tanzania inafanya hiki kizuri kushinda Kenya. Mkenya yuko radhi apitwe hata na Burundi au South Sudan, lakini sio Tanzania. Kwanini, yote hiyo ni uwoga, na kutokuwa tayari kisaikolojia kwamba kuna siku Tanzania itakuwa mbele ya Kenya. Mfano mzuri ni wakati wa digital change over, tv za Kenya waligoma kubadili mitambo, serikali ya Kenyatta ikawalazimisha laki wapi, mpaka tv zikaenda mahakamani kupinga agizo la serikali, serikali ikatumia karata yake ya mwisho, ikawaambia mbona mnapitwa hata na Tanzania? Baada ya hapo, hata public opinion ikabadilika, wananchi wakapiga kelele mpaka tv zika salimu amri na kukubali yaishe. Halafu watanzania wengi wala hawana ushindani na Kenya, kila mmoja na speed zake.

Nikupe ujumbe uwafikie wakenya maana ukija huku unakula bata unasahahu kuondoka na sanduku la upendo. Waambie wale wanao kaa kwenye flats za Umoja, Tanzania ni nchi ya amani, na hatujali kama Kenya watajenga chombo cha kuwapeleka sayari nyingine, sisi tunachotaka ni kupiga biashara na Kenya, zaidi ya hapo tuanza kushikiana uchawi. "Umeniroga ...Hapa, wewe ndio umeniroga" haya hatuyataki
 

Aisei nitakuja kusoma hii riwaya yako nikipunguza kazi, lakini kidogo nilichokisoma kinaongea kuhusu yale yale ya kufikiria Wakenya wamekaa wakiwaza Tanzania. Yaani muulize Mkenya yeyote barabarani kuhusu kinachoendelea Tanzania utashangaa sana, nyie ndio kila siku mnaimba Kenya hiki Kenya kile.
 

Uje tuu tukubariki, maana hii 2017 unahitaji baraka zote.
 
Ni kweli kabisa pia habari zinasema wataihuisha TAZARA na Kujenga reli ya kati. Ni jambo la kihistoria na wala China hajawahi kufanya hivi katika taifa lolote.

[Udumu udugu wetu kati ya Tanzania na China.]
Hii ndio faida ya ujamaa
 
Vimefika vingapi? Au yaleyale ya vyerehani vitatu-kiwanda?
 
Hapa umeonge point,, hili jambo tuliwaachia sana hadi na nyie mkatuzoea vibaya, hadi hapa tulipoamua kuanza kuwawekea vikwazo vya kiuchumi
 
Hapa umeonge point,, hili jambo tuliwaachia sana hadi na nyie mkatuzoea vibaya, hadi hapa tulipoamua kuanza kuwawekea vikwazo vya kiuchumi

Nyie bado ni wale wale, labda baada ya vizazi vipite kama sita hivi ndio tutegemee kautofauti, vikwazo vya kiuchumi dhidi yetu hamjaanza leo, hata enzi za Nyerere tulifungiana mipaka na kuvunja EAC.
Sema sisi ni mabepari, hivyo tuna uvumilivu maana tunatanguliza maslahi yetu, hivyo tunawakuna mnakenua na kuachia na kuendelea kuliwa, Mchina naye anakuja anawaita ndugu mnakenua na kumuachia, mtaendelea hivyo kwa muda mrefu sana mpaka siku ujamaa wa Nyerere utawatoka na kila Mtanzania awe mchakarikaji na wa kujituma na asiyepumbazwa na hayo ya kuitana ndugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…