Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Kila mwanzoni mwa mwaka, diplomasia ya China ina “makubaliano yasiyobadilika” — ziara ya kwanza ya waziri wa mambo ya nje lazima iwe Afrika, na mwaka huu hauna tofauti. Kuanzia tarehe 5 hadi 11 Januari, Wang Yi, Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC na Waziri wa Mambo ya Nje wa China, ametembelea Namibia, Jamhuri ya Congo, Chad, na Nigeria.
Huu ni mwaka wa 35 mfululizo kwa waziri wa mambo ya nje wa China kufanya ziara yake ya kwanza barani Afrika mwanzoni mwa mwaka, jambo ambalo lina maana kubwa katika kuendeleza uhusiano wa kina kati ya China na Afrika.
Kwanza, kwa kuzingatia mkakati wa kidiplomasia, kushikilia desturi hii kwa miaka 35 mfululizo kunaonyesha jinsi China inavyothamini urafiki wa jadi kati yake na Afrika na kudumisha uhusiano huu. Uhakika huu ni wa thamani sana kwa uhusiano wa China na Afrika na kwa jumuiya ya kimataifa kwa ujumla, hasa wakati huu ambapo dunia ipo katika kipindi cha mabadiliko na msukosuko mpya.
Tangu mwaka jana, ambapo uhusiano kati ya China na Afrika ulipandishwa hadhi na kuwa “jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa hali zote katika enzi mpya,” umuhimu wa ziara hii umeongezwa uzito wa kimkakati.
Pili, mwaka huu unaanzwa kutekelezwa “Mpango wa utekelezaji wa Beijing wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (2025-2027).” Katika mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC uliofanyika Beijing mwaka jana, pande zote mbili zilikubaliana kuhusu nyaraka mbili muhimu — “Azimio la Beijing” na “Mpango wa Utekelezaji.”
Nyaraka hizi zinajumuisha maudhui kama vile kuimarisha uhusiano mpya, kushirikiana katika kufanikisha “maendeleo ya kisasa katika pande sita,” na kutekeleza “hatua kumi za wenzi wa kimkakati.” Ziara ya Wang Yi barani Afrika mwaka huu inalenga kuimarisha mawasiliano na uratibu na nchi za Afrika juu ya jinsi ya kutekeleza matokeo ya mkutano wa kilele, hasa juu ya jinsi ya kuanzisha vizuri mpango wa utekelezaji wa miaka mitatu.
Tatu, kama nguvu mpya katika dunia, kuibuka kwa kasi kwa nguvu ya Afrika katika miaka ya hivi karibuni kunabeba matarajio ya pamoja ya China na nchi nyingine nyingi zinazoendelea. Katika muktadha huu, ziara ya Wang Yi inalenga kuimarisha mshikamano wa Dunia ya Kusini, kuimarisha maafikiano ya maendeleo, na kuongeza nafasi ya Dunia ya Kusini katika nyanja ya usimamizi wa kimataifa. Mwaka huu, Dunia ya Kusini inatarajiwa kufanya shughuli mbalimbali:
China itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai, Afrika Kusini itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Kundi la G20, na Brazil itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa Nchi za BRICS. China, ikiwa ni moja ya nchi za Dunia ya Kusini, inahitaji kushirikiana kwa karibu na nchi za Afrika, ambazo ni sehemu muhimu ya Dunia ya Kusini, na kufanya mjadala na mashauriano kuhusu maendeleo ya Dunia ya Kusini mwanzoni mwa mwaka mpya.
Tukitazama mbele, mwaka huu unaleta fursa nyingi kwa maendeleo ya ushirikiano wa kiuchumi kati ya China na Afrika pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Afrika. Kwanza, tangu Desemba 1 mwaka jana, China imezipatia nchi 33 za Afrika msamaha wa ushuru wa bidhaa zinazoingia China, na mwaka huu China itaendelea kuwa mwenyeji wa Maonesho ya Kimataifa ya Uagizaji wa Bidhaa ya China na Maonesho ya Uchumi na Biashara kati ya China na Afrika, ambayo yatazileta pamoja nchi nyingi za Afrika na makampuni kushiriki. Faida hizi zinatarajiwa kuendelea kuleta manufaa makubwa kwa Afrika. Pili, Mpango wa Beijing, ambao umeanza kutekelezwa mwaka huu, unalenga maeneo kumi ya ushirikiano muhimu, na hivyo kutoa nguvu kwa maendeleo ya kisasa ya Afrika. Tatu, mwaka jana, Rais Xi Jinping wa China alitangaza katika Mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika kuwa “Pendekezo la Usalama wa Dunia” litaanza kutekelezwa barani Afrika. Kwa sasa, China na Afrika zinashirikiana katika nyanja ya amani na usalama, ikiwa ni pamoja na kuteua Mjumbe Maalum wa China kwa Masuala ya Pembe ya Afrika na kuandaa “Mkutano wa Amani wa Pembe ya Afrika,” ili kusaidia amani na utulivu barani Afrika.
Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, pamoja na miaka 70 tangu kufanyika kwa Mkutano wa Asia na Afrika mjini Bandung. Aidha, baada ya Misri na Ethiopia kujiunga na “familia kubwa” ya BRICS mwaka jana, kuna matumaini makubwa kuwa China na Afrika zitakuwa na majukwaa mengi zaidi ya pande mbili na ya kimataifa ya kuimarisha mawasiliano na ushirikiano. Hatua hizi zitachangia zaidi katika kuimarisha Jumuiya ya Mustakabali wa pamoja wa Hali zote kati ya China na Afrika, huku pia zikiongeza mshikamano wa ndani na ushawishi wa kimataifa wa Dunia ya Kusini.