Ziara yangu ofisi za JamiiForums

Ziara yangu ofisi za JamiiForums

Screenshot_20240713-181559_Chrome.jpg

Nipenda hii picha imekaa kama vile simba ana pembe
 
Hakika ni jambo jema sana kuwa karibu na viongozi wetu humu kwenye social network ila tambueni siyo watanzania wote wanamiliki simu janja, hivyo basi waheshimiwa msibase humu kwenye social network, humu habari nyingi ni za burudani, social network nikimbilio la wengi walio na stress, mf ndg yangu Ushimen hapo juu masiala ni mengi sana.
 
Ofisi kali sana JF. I am longing for day nitakapo fikia hatua kama hiyo.
Hongereni sana ,sio kazi rahis.

Nb.
Mamods achen ukuda, kumbe ndio maana mnajisahau na kunogewa kupiga ban tu na kufuta nyuzi bila utaratibu
 

Wasalaam Wanajukwaa wenzangu.

Mapema tarehe 12 Julai, 2024 nimetembelea Ofisi za Jamii Forums kama mojawapo ya taasisi inayojihusisha na habari za kijamii. Lengo la ziara ni kuweza kufahamu shughuli za taasisi hii na kuona namna ya kushirikiana Ili kupanua wigo wa kuifikia jamii kidigitali.

Kama Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, tumejadiliana kuhusu umuhimu wa kushirikiana kwenye mada za kuifikia jamii katika masuala mbalimbali ya maendeleo na ustawi wa jamii kwa ujumla na hususan, kupambana kutokomeza ukatili wa kijinsia na kwa watoto.

Kama mwanachama hai wa JF na aliyethibitishwa, niko tayari kuendelea kupokea mawazo na changamoto kutoka kwa wananchi kupitia mitandao ya kidigitali ambayo kimsingi inarahisisha sana mawasiliano na wananchi.

Hivyo, nawakaribisha nyote kunitumia mawazo mbalimbali na changamoto kwani, ushirikiano wa jamii ni muhimu kwa maendeleo.

Ahsante sana Mkurugenzi wa JamiiForums Maxence Melo (ninayesalimiana naye) na timu yako yote🤝

Mungu awabariki 🤝🇹🇿 na awabariki wanajukwaa wote🤝

Msaidieni huyu mtu 👇👇

View: https://www.instagram.com/reel/C_FtxmrCmAx/?igsh=MTJtMXVvOWp0MHZ5aA==
 
Back
Top Bottom