Zidane ni kocha wa kawaida sana, kimbinu anapitwa hata na Arteta

Sahihi ila bahati
 

Tunaanza hapa Kwanza,
Hivi ni vikosi viwili tofauti vya real Madrid
kimoja ni cha Zidane kilichochukua uefa dhidi ya juve
kingine ni cha Carlo Ancelotti kinachotarajiwa Kucheza final jumamosi, Je huoni Kama lineups zilivyopangwa zinanana?

Peter msechu anaweza kupanga kikosi kifanane na cha Ancelotti?
 

Attachments

  • IMG_20240530_001958.jpg
    178.4 KB · Views: 2
  • IMG_20240530_001939.jpg
    185 KB · Views: 1
Mfumo na falsafa ni tofauti mfano gadiora na klopp mfumo wanaopanga wachezaji wao unalingana ila falsafa zao ni tofauti. Mifumo ipo 442, 352, 433 n.k ukija kwenye falsafa kuna counter attack, low block, pressing, ball possesion n.k.. bado haujanijibu swali langu Zidane akiwa kocha real madrid alikua anatumia falsafa gani.
 
Nimekujibu Falsafa ya Madrid.

Utamaduni wa Madrid ni kutafuta kutumia wachezaji wake kama nguzo badala ya mbinu pekee.

Juzi Kati Carlo Ancelotti alifanyiwa interview na kuzungumzia ufundishaji wake na makocha wengine akasema wao wanatoa Maelekezo mengi Kwa Wachezaji Hii inafanya kuwabsna Ila yeye hua anawaachia Uhuru Wachezaji wacheze Kwa vipaji vyao.

Huo ndio utamaduni wa Carlo Tangu akiwa juve, AC Milan, Parma na kadharika huoni umefanana na wa Madrid?

Sababu ya kukuletea vikosi ni kuanza kukuonesha mfanano kuanzia hapo ili uijue Falsafa ya Madrid, Ancelotti na Zidane ni kitu kimoja.

Angalia Madrid wanavyocheza sasa haitofautiani na madrid Ile ya Zidane.

pia haitofautiani na madrid ya 2014.

kwahyo hiyo Falsafa Ipe jina we mwenyewe si unajua majina ya Falsafa bhana.

Unashangaza ujue mkuu.
Kwani hujui Carlo Ancelotti anatumia Falsafa gani? Au Hujui kwamba Zidane kapita mikono ya Ancelotti?

Ikiwa Arteta kuwa Chini ya pep kapewa Arsenal hajachukua hata kombe la maana ulaya tayari ushasema ana Falsafa.

Imekuaje Zidane aliekua Chini ya Ancelotti kapewa Madrid kabeba uefa 3 na la Liga juu et Hana Falsafa.!!!

Au na Carlo Ancelotti Hana Falsafa?

Hivi mnatufanya Wengine tunaangaliziaga mpira Kwa visogo sio?
 
Kipindi zidane anafundisha real madrid alikua anatumia falsafa gani? Kama haujui kuna ugumu gani wa kusema haujui? sasa falsafa ya real madrid ndio kitu gani hicho.
 
Umenikumbusha kuna game moja ya El classico ilipigwa Bernabeu, real madrid walifungwa goli la kona na Carles Puyol, baada ya mechi kuisha Morinho alimlaumu sana Ramos kwamba alishindwa kutekeleza wajibu wake.... maana kabla ya mechi Morinho alikuwa amewaambia kwenye mipiraya set pieces Ramos ndio atamfanyia man-marking Puyol halafu Pepe atakuwa ana mmark Gerald Pique, sasa kwenye lile goli ilikuwa ni vice verse, Ramos alienda kummark mtu mwingine kabisa tofauti na Puyol.... baasi baadae ya hapo Morinho alimmind sana Ramos, Ramos nae kwa kiburi akamwambia "wewe unanilaumu mimi kwa sababu hujacheza mpira na hivyo kuna vitu vingi huvijui vinavyondelea uwanjani, light kama ungekuw umewahi kucheza kwenye professional level usingenilaumu, ungejua kwamba sio lazima muda wote wachezaji wafuate maelekezo ya kocha, kuna muda itabidi mchezaji nifanye maamuzi tofauti na maelekezo ya kocha kulingana na movement ya mchezo"

Basi baada ya Ramos kutoa hayo maneno Morinho aliumia sana, na ukawa ndio mwanzo wa bifu lao mpaka anaondoka pale real madrid.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…