Zielewe kazi za Usalama wa Taifa (TISS) na mipaka yake

Tofautisha usalama tiss na psu mwajiri wao nani, kiongozi wao nani ambaye wanawajibika kwake

Nikipata haya majibu labda utaelewa nataka kujua nini
 
TISS wa miaka hii wamekuwa ni watu wa kujikweza kiasi wananchi tumewazoea na kuona hawana jipya ile heshima yote imetoweka hawana weledi wowote ule, kutoa silaha hadharani pasipo sababu za msingi ni kitu kingine kinachofanya waonekane kama mahayawani tu na hela zenyewe hawana kiivyo
 
Hongera kwa andiko bora kabisa.Mkuu sijakuelewa ulipoandika kuna wengine wameajiriwa kama wasaidizi lakin wala hawafahamu kama wanafanya kazi hiyo.Usalama huwa hawana ID card?Huwa nasikia pia hao watu huwa hawajuani japo wanafanya kazi moja.Na je kila mtu wa usalama ni lazima ajue kutumia bunduki?
 
Kwamba hata mko wote PSU mfn msijuane ? ..yaani wakae makumbusho mule na familia zao wasijuane ?
 
Shukran sana comred
 

Wameingia watu wengine kule ndani ambao hawana faida yoyote ile na wala hawajui hata nini kinaendelea duniani 😂 😂 😂 😂 😂
 
sijakuelewa kitu kimoja, unaposema mtu wa usalama hatakiwi kujitangaza au kujulikana isipokuwa kwa familia yake tu. Mbona ofisi zao tunazijua? kila mkoa kuna jengo la tiss, na hata akienda kufanya kazi popote wanajua katoka jengo fulani? pili, haujamaliza, ongelea pia hatari walizo nazo ukijumuisha na zile za kupotezwa na tiss wenzao wakitoa siri au kufanya jambo la kiusaliti. pia, hao wanaojitangaza, mbona tukifuatilia huwa tunaona ni tiss kweli. na mbona siku hizi wale wale wanaofanya kazi toka ofisi ya tiss kabisa mfano DSO au RSO huwa wanaorganize arrest kwa watu, arrest kwenye magari yetu ya biashara n.k? unafikiri sisi ni wageni na tiss? as if kwa biashara tumefanya miaka yote hii hatuwajui? hawajawahi kuomba au kupokea rushwa? hatuwajui? pia, ongelea nyoka, yaani wale bablish wanaotumiwa na kubwagwa.
 
Mkuu hujanielewa au umechagua usinielewe. Kwani nikisema mwanafunzi hatakiwi kuwa mtoro ndio hakuna watoro mashuleni? Tukisema mawaziri hawataki kuomba na kupokea rushwa ndio hakuna wanaofanya kinyume? Kwani mahakama na magereza zipo kwa ajili gani kama sio kuwaadhibu wanaokwenda kinyume na sheria?

Tunaposoma mada tuelewe malengo ya mtoa mada. Mada yangu ni kuelezea kazi na mipaka ya TISS sio vinginevyo. Kama kuna watu wa TISS wanaokwenda kinyume na kazi na maadili yao hilo linastahili uzi mwingine na anayejua afungue uzi huo. Niseme tu kwamba TISS wala sio ofisi takatifu, kama ilivyo kwenye ofisi nyingine za serikali wapo waajiriwa wanaofanya kinyume na matarajio. Lakini mada yangu haijakusudia kuchambua utendaji kazi wao au ufanisi wao.
 
Watu wanatumia hii kazi kututishia tishia yani hata raia wa kawaida nao wanatutishia ni tiss ilimradi tu tuishi kinyonge.....
Ni kwa vile tu hamjui, usalama wa Taifa hawana power of arrest.

Akiingia kwenye 18 zako mletee defender anawekwa ndani na hawezi kujitambulisha Polisi kama yeye ni usalama atatumia network yake kujichomowa ndani ya nondo.

Kuna dereva mmoja wa usalama alikuwa anafanya deal za kubeba wahamiaji haram siku yake akaingia kwenye 18 za Polisi akawekwa ndani Moshi, RSO alivyokwenda akaitwa chemba akachukuwa kitambulisho chao akamuacha apambane na hali yake na kibarua kiliishia hapo.

Usalama ni tofauti na wengi mnavyowachukulia, hao wanaowababaisha mitaani ni Uvccm wanashona vikaunda suti vyao nyeusi na kujifanya usalama wakati ni green guard wa maccm tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…