Zifahamu adhabu za kikatili zilizotolewa na wafalme wa zamani

Zifahamu adhabu za kikatili zilizotolewa na wafalme wa zamani

Uweeeeeeeeee...!! ukibaki shule kwamba usiende, wanaita majina huko huko afu usionekane..!! Kesho yake utangóa visiki ukome
😂😂😂😂 mkitoka hapo mnaambiwa mrudi shule 😂😂😂
 
Kwani jiwe alikuwa wa zamani?
Tofautisha. Zamani hizo adhabu(licha ya kwamba zilikuwa ni za kikatili) zilitolewa baada ya Mtuhumiwa kupatikana na Hatia na Hukumu ikatolewa kwa mujibu wa Taratibu zilizokuwepo.
 
Mada nzuri sana iweke na huku pia
Kweli kabisa.
 
Salaam wakuu, Leo katika historia nimeamua niwafahamishe baadhi ya adhabu za kikatili zilizotolewa na wafalme wa enzi hizo.

Brazen bull; hii ni adhabu ambayo ilivumbuliwa na bwana mmoja aliyeitwa perilaus kutoka katika nchi ya wagirikiView attachment 2471472adhabu hii ilihusisha kifaa kilichokuwa kimetengenezwa mithili ya ng'ombe, kwa kutumia malighafi aina ya shaba.

Ambapo sehemu moja ya kifaa hicho kuliwekwa mlango kwa ajili ya kuingizia waharifu, lakini pia iliwekewa tundu mbili kwa ajili ya kutolea sauti.

ambapo moto mkubwa ungewashwa chin ya ng'ombe huyo na kisha mtuhumiwa angeingizwa ndani yake na kisha angeachwa afie humo.

Choke pear; adhabu hii ilihusisha kifaa kilichotengenezwa mithili ya puto, yaani puto la chuma.
huku mbele kikiwa kimewekewa viwembe vya chuma vilivyokunjwa na nyuma kikishikiliwa na chuma kilichokuwa Kama funguo
View attachment 2471480
adhabu hii walipewa watu wote waliozungumza maneno yenye hatia mfano kuitukana serikali au raisi wake.
Lakini pia wazinzi au mashoga adhabu hii walipata, ambapo kifaa hiki kingechukuliwa na kuwekwa ndani ya sehemu za Siri za mwanamke mzinzi au dume lililolaaniwa.

molten gold torture; hii ilihusisha kumuadhibu mtu kwa kumnywesha uji wa dhahabu ya moto uliochemshwa.

View attachment 2471484
Ambapo mtu angefungwa kwa nguvu ili asifurukute na kisha mdomo wake unafunguliwa kwa kifaa maalumu na kuuacha mdomo wake ukiwa wazi kwa upana mkubwa.
Kisha uji wa moto wa dhahabu ungemiminwa ndani ya mdomo wake na kumuua.
Hii ilivumbuliwa ndani ya nchi ya Spain.

Iron chair of spikes; adhabu hii ilihusisha kiti kilichokuwa kimetengenezwa kwa chuma, kisha kuwekewa vimishale au mikuki midogo sehemu ya kukalia, kuweka mikono pamoja na miguu.

View attachment 2471510

Ambapo mtuhumiwa angekamatwa na kufungwa katika kiti hicho, hii ingepelekea kuanza kubanwa au kutobolewa na vimishale hivyo.
Mtuhumiwa hupoteza damu nyingi na kupelekea kifo chake.

Till next time guys💪🙏
Watu bana, kutesa wengine.
 
Kwan ulikuwa unalazimishwa kwenda?au ilikuwaje? Najua zaman mpo shule mnaambiwa kwenda barabaran na matawi ya miti 😂😂😂
Mhhh! Bibie, Kuna kipindi Mheshimiwa akiwa uwanjani, huko mitaani wapo mgambo wakali kama pilipili kichaa wanapita nyumba kwa nyumba. Ole wako wakukute na sio mgonjwa. Vilabu vyote vya "manywaa" hufungwa hadi mkubwa aondoke.
 
Mhhh! Bibie, Kuna kipindi Mheshimiwa akiwa uwanjani, huko mitaani wapo mgambo wakali kama pilipili kichaa wanapita nyumba kwa nyumba. Ole wako wakukute na sio mgonjwa. Vilabu vyote vya "manywaa" hufungwa hadi mkubwa aondoke.
😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom