Zifahamu changamoto za kwenye kilimo zilizo kubwa

Uko sahihi ila kwenye kutengeneza title Bora na yakuvutia kila lika usitumie formular uliyo kalilishwa darasani tengeneza kichwa chenye kushawishi watu wengi wahitaji kulipitia andiko.kasome magazeti ya mwana sport na yale ya udaku utani elewa logic yangu kwenye title ya kitu kilicho ndani kama unataka kila mtu avutiwe kusoma.

Kingine huenda kichwa Cha habari kama hicho nimesha tumia huko nyuma ndo mana sikupenda kikae Kwa mfumo huo nilio kwisha andika baadhi ya maandiko Kwa kichwa Cha habari kama hicho.

Karibu tena
Nimekumbuka kipindi kile tukitakiwa kusoma insha isiyo na title kisha kutakiwa ku-propose title yake.

Hii ingesomeka something like "CHANGAMOTO KUBWA KWENYE KILIMO" ingekuwa poa sana.
O
 
Please nipeni
sumu nzuri za maharage
Dawa nzuri ya ukungu.
Pia kiwango cha matumizi kwa acre tano.
Niko mwese-,mpanda.
 
Mkuu nina mpango nilime heka 100 za ufuta nina mpango niende naliendele nikapate elimu sahihi
 
Huku nilipo maafisa ugani wapo na wanasaidia sana wakulima na wao wanalima mashamba yao. Leta hoja nyingine
 
Naunga Mkono hoja.Kilimo ni kipana Sana ingawa wengi wamejikita kwene Kuzalisha Mazao (crop production).Kwenye value chain ya Kilimo Kuna Shughuli nyingi.Wauzaji/Wasambazaji wa Pembejeo nao wapo,wenye magodown ya Kuhifadhi mazao nao wapo,wasafirishaji wa Mazao pia wapo,Madalali pia wapo.Wachakataji (processing)wa Mazao pia wapo.Wote Hao Wanaunda Mnyororo wa Thamani ya Kilimo.Chagua Upande sahihi unaweza kuumudu.Upande wa Kuzalisha Mazao kuna changamoto ya Mvua kutokuwa za Uhakika,Msimu kuyumba, miundombinu dhaifu (ya Barabara,Nishati za Umeme,umwagiliaji NK),Masoko yasiyotabirika,Wizi na utapeli wa Madalali,Huduma mbovu za ugani, wataalam wa Kilimo kutokidhi viwango,wahudumu wa Maduka ya Pembejeo wasio na Ujuzi wa bidhaa wanazouza,taasisi dhaifu za Serikali kusimamia ubora wa bidhaa za Kilimo (Pembejeo,Mbegu,Mbolea, Viuatrifu NK).Kwa ufupi ukienda kununua Dawa Madukani huna Uhakika kama ina Kiwango na ubora sahihi.Ni kama unapiga ramli.Mwaka 2020 kuna Wilaya walipewa Mbegu na Mbolea za bei nafuu.Ilikuja kugundulika baada ya Kulima Mbegu zilikuwa reject na Mbolea ziliokotwa kama makapi kisha kufungashwa.Walilia machozi,Nami nilipewa Mifuko 2 bado sijasahau Maumivu yake.Mwisho hizi Mbegu za ASA kaa nazo kwa tahadhari Ubora wake uko chini Sana.
 
Mimi tafsiri yangu.....kilimo ni kamari.
 
Hivi kuna Bima ya kilimo?
 
T
Tanzania yangu yaan wakala wa mbegu naye haaminiki .Daaah sijui ni lini nas tutakuwa proud
 
Mwaka huu wakulima wa mbaazi wamelia newala baada ya kuletewa mbegu ya mbaazi ambayo hairefuki na inazaa mbaazi chache sana na hizo chache zenyewe ukimenya ni kama vigololi
 
Andiko limeandikwa kwa kuongozwa na hisia za mtu binafsi pasipo kuhusishwa ujuzi na uzoefu wa Kilimo
 
Andiko limeandikwa kwa kuongozwa na hisia za mtu binafsi pasipo kuhusishwa ujuzi na uzoefu wa Kilimo.
Acha niheshim mtazamo wako ila hisia sijui kama zinaweza kuandika vitu kama hivyo kama mtu haupo kwenye kilimo na hukijui kilimo kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…