Zifahamu Engine oil

ebu weka picha ya hiyo stika na sehemu ya boneti inapokaa,na sisi tujirizishe kuwa ni km 15000 ndo tubadili engine oil.
 
Yes technology ya oil imeadvance.. Ila km 15,000 kwa oil ni nyingi..
 
Nini tofauti kati ya oil ya diesel engine na ile ya petrol?
 
Nini tofauti kati ya oil ya diesel engine na ile ya petrol?
Zinapishana additives zinazowekwa..!
Mazingira ya kazi kwenye diesel engine ni tofauti na kwenye petrol engine..!
 
Oil ya gear box inatakiwa kubadilishwa baada ya mda gan wakuu...?
Inategemea na condition ya gari , kuanzia 30,000km mpaka 60,000km, na kama ni ATF itathmini kwa kuangalia rangi yake ikianza kuwa nyeusi , badilisha , weka oil ya brand nzuri , TOTAL, SHELL, CASTROL then unasahau miaka 4..

Sent from my Phantom6-Plus using JamiiForums mobile app
 

Oky ist nlinunua na elfu 33km sasa 46km na mwaka nayo sasa sijawah kupadilisha kumbe bado Nipo muda...[emoji1545]
 
Gear Box ya Rav 4 new Model ( Miss TZ ) inayotumis oil CVT TC inaingia lita ngapi??
 
Toyota fielder mwaka 2007, cc 1450 natumia oil SAE 5w40, ni sawa?? Naomba kujua Gear box oil yake pls
 
Mkuu habari, Uzi mzuri sana, naomba Ushauri Gari Engine 1NZ - FE T.Spacio Km 50,000 naomba kufahamu kupitia Manual book yake kuna Maelezo hapo kwenye hiyo Picha je nibadilishe kwa aina IPI ya oil kama inavyosomeka, nipo Dar. Asante.
 

Attachments

  • IMG_20220728_175825_4.jpg
    307.6 KB · Views: 108
Mkuu habari, Uzi mzuri sana, naomba Ushauri Gari Engine 1NZ - FE T.Spacio Km 50,000 naomba kufahamu kupitia Manual book yake kuna Maelezo hapo kwenye hiyo Picha je nibadilishe kwa aina IPI ya oil kama inavyosomeka, nipo Dar. Asante.
Engine bado mbichi kabisa..
Tumia 5w30..!
 
Odo za kibongo zimechezewa mkuu. Jamaa kanunua gari yard ina 45k km
Fraud kamaa hizi ni rahisi kuzingundua... Ukitaka kununua gari yard za bongo... Mwambie muuzaji akupe file lenye auction details kutoka huko gari liliko toka.. utaona auction rating, utaona odo zake wakati inauzwa, utaona service history na kama imewahi pata accident au lah
 
Kuhusu oil.. jamaa wadau wameelezea vizuri, nami niweke kamchango kangu kidogo.

Mineral oil ambazo ni non synthetic oil zina changamoto ya kutengeneza carbon kwenye injini kama zisipo badilishwa kwa wakati

Synthetic oil kwakua zina additives zinazofanya ziweze kumantain viscosity yake hata zikiwa exposed to high temperature for extended time... Lakini si kusubiri mpaka gari ifikishe km 10,000 ndo ubadili oil.. utaua injini yako.

Ubora wa oil.. ubora wa oil una angalia urahisi wa oil ku flow wakati wa low temperature na uwezo wa ku-maintain thickness ya oil wakati wa high temperature, carbon formation kwenye engine, evaporation rate ya oil.

Matumizi ya oil kwenye Gari.. oil ufanya kazi ya lubrication kwenye moving parts, sasa hizi moving parts ndan ya injini huwa zinakua na certain clearance kwa ajili ya oil kukaa ili kuzuia physical contact between moving parts.. hapa sasa ndo bongo kuna shida. Unakuta manufacturer kaandika gari yake inatumia oil 5w-30.. hapa mzungu kaisha jua kwamba kwa clearance iliyopo kwenye components za injini basi oil ya viscosity fulan itafaa, sasa mbongo anaenda chukua oil nzito Kama sae 40 au 20w-50 anatia ndani ya gari.. sasa kumbe hapa anatengeneza tatizo. Hizi oil ni zito sana zinaongeza pressure kwenye moving parts kwakua clearance inakua ni ndogo ulinganisha na thickness ya oil hasa during cold start.. mpaka baadae oil ikisha pungua thickness because of temperature. Sasa gari nyingi hapa Tanzania hufa kwasababu ya oil hizi nzito hasa wakati wa asubuh ambapo kwakua hizi oil ni nzito, ukiwasha Gari for the first time oil inachelewa kupanda juu kwenye cam shafts, vvti system na kufika kwenye cylinder wall kwakua oil ni nene na hai flow kwa wakati.. sasa unakuta hadi injini inatoa sauti za ajabu wakati inapowaka for the first time, then zile sauti zinapotea baada ya oil kufika kwenye yale maeneo kwakua tayari injini imechemka na oil imelainika.. na situation huwa mbaya zaidi kama umetoa thermostat kwakua injini inachelewa ku attain required temperature so na oil inashidwa yeyuka kwa wakati, na kama kukiwa na extended usage ya hizi thick oil wakati mwingine huua (destroy) rings za oil kwenye piston kwakua oil inashindwa kupita kwenye vitundu vya piston kurudisha oil kwenye sump.. nakuleta tatizo gari kula oil.. lakini pia kuua piston rings because of excessive compression inayosababishwa na thick oil na kuleta shida pia ya injini kula oil in long run.

Kuhusu interval ya ku change oil.. watu wengi sisi tuna angalia kilometers tu peke yake Gari imetembea ili kubadili oil, ila tuna sahau kuna muda Gari ina unguruma hata saa nzima bila kwenda popote ila oil inaungua.. sasa hapa kama una angalia tu km shauri yako utaua injini mapema.. ni vizuri kuangalia oil ipo kwenye hali gani hasa kama gari ina kaa sana kwenye folen injini ikiwa on.

Pia kama ni mtu unatembea short distance unazima gari mara unawasha zima kila wakati.. hii pia hufanya oil iwe contaminated na gasoline.. kumbuka gari inapowaka injekta (fuel injectors) humwaga mafuta mengi ila kufanya gari iwake, so sio mafuta yote huungua, mengine hupenya na kwenda kwenye sump ya oil, so haya yanayopenya huenda ku contaminate oil na kuifanya oil ipungue ubora wake with time.

Pia kama unasafiri zaid ya miezi sita na gar ikakaa 6months bila kuwaka hata kama uliondoka umeweka oil mpya ukija toa hiyo oil weka nyingine.

Interval ya oil changing.. kama watumia mineral oil kwa mazingira yetu ya kitropic na hizi folen za mjini change oil from 2500km to 3000km.. na hakikisha watumia quality oil zisizokua na rate kubwa ya utengenezaji wa carbon au rate kubwa ya oxidation.

Kwa wa synthetic oil change after every 5000km na sio kwenda mpaka km7000-10,000 hata kama watumia liquimo oil. (Na hapa lazima uwe na uhakika gari yako haina tatizo la kula oil. Kama inakula oil utakuta unaweka hizi kwakua ni nyepesi mpaka unafika km 5000 unakuta umebakiwa na oil lita moja)


Kuhusiana na quality ya oil, tafuta oil zenye API rating nzuri hasa ukiwa na gari zenye GDI fuel system au pia ukiwa na Gari ya Turbo.

Kuhusiana na oil za gearbox (transmission fluid) weka recommended transmission fluid ambazo manufacturer wako ame recommend.. kama ni ATF-TYPE 4, CVT-TC, or CVT-FE, WS, NS-2 or3, Matic J, DSG nk.. ili mradi ni recommended.. and avoid universal transmission fluids.. na transmission hubadilishwa after at least every 30,000km but you can go more than that depending na mazingira gari inatumika..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…