Zifahamu Engine oil

Zifahamu Engine oil

Kuna stika kwenye bonnet kwa ndani , gari ni Toyota imeandikwa kijapani , ukiiscan na Google translator , inasema badilisha engine oil every 15,000km. sijakosea , ni kilomita elfu 15.
Nafkiri oil za kizamani sana ndio unabadilisha hizo 5,000km , au 3,000km , siku hizi ziko improved mno kuokoa gharama kwa mtumiaji.
ebu weka picha ya hiyo stika na sehemu ya boneti inapokaa,na sisi tujirizishe kuwa ni km 15000 ndo tubadili engine oil.
 
Kuna stika kwenye bonnet kwa ndani , gari ni Toyota imeandikwa kijapani , ukiiscan na Google translator , inasema badilisha engine oil every 15,000km. sijakosea , ni kilomita elfu 15.
Nafkiri oil za kizamani sana ndio unabadilisha hizo 5,000km , au 3,000km , siku hizi ziko improved mno kuokoa gharama kwa mtumiaji.
Yes technology ya oil imeadvance.. Ila km 15,000 kwa oil ni nyingi..
 
Tabia yake
Oil inakuwa nyepesi jinsi inayopata joto na kuwa nzito jinsi inavyopoa.. Kwahiyo kufahamu viscosity sahihi kwenye cold start na operating temperature ni muhimu..!
Viscosity ni resistance ya oil kuflow.. Kwahiyo oil yenye viscosity kubwa ni ngumu kuflow hence nzito zaidi..!

Kazi yake
Kulainisha msuguano wa vyuma ndani ya engine..!
Oil pump inaizungusha oil kwenye sehemu za engine kama damu inavyozungushwa kwenye mishipa..
Wakati inarudi kwenye sump inakutana na oil filter ambayo inachuja uchafu na kuhakikisha oil inavyozungushwa ipo vizuri..!
Sump huwa inakuwa chini kabisa ya gari, as gari inatembea cold air inapooza oil kwenye sump na kusaidia kutoa joto kwenye engine..!

Aina zake
Mineral oil - hii inatokana na kuchujwa kwa crude oil..haina mambo mengi kwenye uzalishaji wake..molecules zake hazipo uniform.. Kwahiyo flow sio nzuri..bei ipo chini.. Interval ya service nayo ni karibu karibu..!

Semi Synthetic na Synthetic oil - hizi zipo very refined.. Hasa hasa synthetic.. Ni oil zinazotengenezwa LAB kwa formula.. Kwahiyo molecules zake zipo uniform.. Flow inakuwa nzuri..!
Interval yake unaenda kilometers nyingi..
Hapa panahitaji umakini.. Oil inaweza kuwa nzuri kwa kilometers nyingi ila oil filter isiwe na uwezo wa kwenda kilometers nyingi..!

Grading ya Oil
Oil imekuwa graded na hawa SAE kwenye makundi 2..Monograde na Multigrade..!
Mono kama jina lake.. Ina viscosity moja throughout..! Wakati Multi ni zaidi ya moja..

MFANO wa Monograde SAE40.. Hii inakuwa na viscosity ya 40 kuanzia cold start mpaka operating temperature.. Kwahiyo ukiwasha gari inabidi uipe muda kidogo ili oil ipande vizuri kwenye engine.. Unaweza ukawasha gari then ukaenda kuoga.. Mpaka ukitoka mambo yamekaa sawa..!
Hizi zinafaa kwa mazingira ambayo hakuna temperature change kubwa kwenye seasons kama hapa TZ..!

Mfano wa Multigrade 5W40.. Hii inabehave kama oil ya 5 viscosity kwenye cold start na 40 viscosity kwenye operating temperature..!
Kwahiyo ukiwasha tuu gari.. Oil itapanda chap kwenye engine haihitaji kusubiri muda..! Hizi zinafaa kwenye mazingira yenye mabadiliko makubwa ya temperature ndani ya mwaka..!
Hii inapunguza usumbufu wa kubadilisha oil wakati wa winter na summer..!

0W40 ni nyepesi zaidi ya 5W30 kwenye winter(cold start) .. Ila ni nzito zaidi kwenye summer(operating temperature).!
Nini tofauti kati ya oil ya diesel engine na ile ya petrol?
 
Nini tofauti kati ya oil ya diesel engine na ile ya petrol?
Zinapishana additives zinazowekwa..!
Mazingira ya kazi kwenye diesel engine ni tofauti na kwenye petrol engine..!
 
Oil ya gear box inatakiwa kubadilishwa baada ya mda gan wakuu...?
Inategemea na condition ya gari , kuanzia 30,000km mpaka 60,000km, na kama ni ATF itathmini kwa kuangalia rangi yake ikianza kuwa nyeusi , badilisha , weka oil ya brand nzuri , TOTAL, SHELL, CASTROL then unasahau miaka 4..

Sent from my Phantom6-Plus using JamiiForums mobile app
 
Inategemea na condition ya gari , kuanzia 30,000km mpaka 60,000km, na kama ni ATF itathmini kwa kuangalia rangi yake ikianza kuwa nyeusi , badilisha , weka oil ya brand nzuri , TOTAL, SHELL, CASTROL then unasahau miaka 4..

Sent from my Phantom6-Plus using JamiiForums mobile app

Oky ist nlinunua na elfu 33km sasa 46km na mwaka nayo sasa sijawah kupadilisha kumbe bado Nipo muda...[emoji1545]
 
Toyota fielder mwaka 2007, cc 1450 natumia oil SAE 5w40, ni sawa?? Naomba kujua Gear box oil yake pls
 
Tabia yake
Oil inakuwa nyepesi jinsi inayopata joto na kuwa nzito jinsi inavyopoa. Kwahiyo kufahamu viscosity sahihi kwenye cold start na operating temperature ni muhimu!

Viscosity ni resistance ya oil kuflow.. Kwahiyo oil yenye viscosity kubwa ni ngumu kuflow hence nzito zaidi..!

Kazi yake
Kulainisha msuguano wa vyuma ndani ya engine!

Oil pump inaizungusha oil kwenye sehemu za engine kama damu inavyozungushwa kwenye mishipa..
Wakati inarudi kwenye sump inakutana na oil filter ambayo inachuja uchafu na kuhakikisha oil inavyozungushwa ipo vizuri.

Sump huwa inakuwa chini kabisa ya gari, as gari inatembea cold air inapooza oil kwenye sump na kusaidia kutoa joto kwenye engine.

Aina zake
Mineral oil - hii inatokana na kuchujwa kwa crude oil..haina mambo mengi kwenye uzalishaji wake..molecules zake hazipo uniform.. Kwahiyo flow sio nzuri..bei ipo chini.. Interval ya service nayo ni karibu karibu..!

Semi Synthetic na Synthetic oil - hizi zipo very refined.. Hasa hasa synthetic.. Ni oil zinazotengenezwa LAB kwa formula.. Kwahiyo molecules zake zipo uniform.. Flow inakuwa nzuri. Interval yake unaenda kilometers nyingi..
Hapa panahitaji umakini.. Oil inaweza kuwa nzuri kwa kilometers nyingi ila oil filter isiwe na uwezo wa kwenda kilometers nyingi.

Grading ya Oil
Oil imekuwa graded na hawa SAE kwenye makundi 2. Monograde na Multigrade.
Mono kama jina lake.. Ina viscosity moja throughout. Wakati Multi ni zaidi ya moja.

MFANO wa Monograde SAE40.. Hii inakuwa na viscosity ya 40 kuanzia cold start mpaka operating temperature.. Kwahiyo ukiwasha gari inabidi uipe muda kidogo ili oil ipande vizuri kwenye engine.. Unaweza ukawasha gari then ukaenda kuoga.. Mpaka ukitoka mambo yamekaa sawa.

Hizi zinafaa kwa mazingira ambayo hakuna temperature change kubwa kwenye seasons kama hapa TZ..!

Mfano wa Multigrade 5W40.. Hii inabehave kama oil ya 5 viscosity kwenye cold start na 40 viscosity kwenye operating temperature.

Kwahiyo ukiwasha tuu gari. Oil itapanda chap kwenye engine haihitaji kusubiri muda. Hizi zinafaa kwenye mazingira yenye mabadiliko makubwa ya temperature ndani ya mwaka.

Hii inapunguza usumbufu wa kubadilisha oil wakati wa winter na summer.

0W40 ni nyepesi zaidi ya 5W30 kwenye winter(cold start) ila ni nzito zaidi kwenye summer(operating temperature).!
Mkuu habari, Uzi mzuri sana, naomba Ushauri Gari Engine 1NZ - FE T.Spacio Km 50,000 naomba kufahamu kupitia Manual book yake kuna Maelezo hapo kwenye hiyo Picha je nibadilishe kwa aina IPI ya oil kama inavyosomeka, nipo Dar. Asante.
 

Attachments

  • IMG_20220728_175825_4.jpg
    IMG_20220728_175825_4.jpg
    307.6 KB · Views: 108
Odo za kibongo zimechezewa mkuu. Jamaa kanunua gari yard ina 45k km
Fraud kamaa hizi ni rahisi kuzingundua... Ukitaka kununua gari yard za bongo... Mwambie muuzaji akupe file lenye auction details kutoka huko gari liliko toka.. utaona auction rating, utaona odo zake wakati inauzwa, utaona service history na kama imewahi pata accident au lah
 
Kuhusu oil.. jamaa wadau wameelezea vizuri, nami niweke kamchango kangu kidogo.

Mineral oil ambazo ni non synthetic oil zina changamoto ya kutengeneza carbon kwenye injini kama zisipo badilishwa kwa wakati

Synthetic oil kwakua zina additives zinazofanya ziweze kumantain viscosity yake hata zikiwa exposed to high temperature for extended time... Lakini si kusubiri mpaka gari ifikishe km 10,000 ndo ubadili oil.. utaua injini yako.

Ubora wa oil.. ubora wa oil una angalia urahisi wa oil ku flow wakati wa low temperature na uwezo wa ku-maintain thickness ya oil wakati wa high temperature, carbon formation kwenye engine, evaporation rate ya oil.

Matumizi ya oil kwenye Gari.. oil ufanya kazi ya lubrication kwenye moving parts, sasa hizi moving parts ndan ya injini huwa zinakua na certain clearance kwa ajili ya oil kukaa ili kuzuia physical contact between moving parts.. hapa sasa ndo bongo kuna shida. Unakuta manufacturer kaandika gari yake inatumia oil 5w-30.. hapa mzungu kaisha jua kwamba kwa clearance iliyopo kwenye components za injini basi oil ya viscosity fulan itafaa, sasa mbongo anaenda chukua oil nzito Kama sae 40 au 20w-50 anatia ndani ya gari.. sasa kumbe hapa anatengeneza tatizo. Hizi oil ni zito sana zinaongeza pressure kwenye moving parts kwakua clearance inakua ni ndogo ulinganisha na thickness ya oil hasa during cold start.. mpaka baadae oil ikisha pungua thickness because of temperature. Sasa gari nyingi hapa Tanzania hufa kwasababu ya oil hizi nzito hasa wakati wa asubuh ambapo kwakua hizi oil ni nzito, ukiwasha Gari for the first time oil inachelewa kupanda juu kwenye cam shafts, vvti system na kufika kwenye cylinder wall kwakua oil ni nene na hai flow kwa wakati.. sasa unakuta hadi injini inatoa sauti za ajabu wakati inapowaka for the first time, then zile sauti zinapotea baada ya oil kufika kwenye yale maeneo kwakua tayari injini imechemka na oil imelainika.. na situation huwa mbaya zaidi kama umetoa thermostat kwakua injini inachelewa ku attain required temperature so na oil inashidwa yeyuka kwa wakati, na kama kukiwa na extended usage ya hizi thick oil wakati mwingine huua (destroy) rings za oil kwenye piston kwakua oil inashindwa kupita kwenye vitundu vya piston kurudisha oil kwenye sump.. nakuleta tatizo gari kula oil.. lakini pia kuua piston rings because of excessive compression inayosababishwa na thick oil na kuleta shida pia ya injini kula oil in long run.

Kuhusu interval ya ku change oil.. watu wengi sisi tuna angalia kilometers tu peke yake Gari imetembea ili kubadili oil, ila tuna sahau kuna muda Gari ina unguruma hata saa nzima bila kwenda popote ila oil inaungua.. sasa hapa kama una angalia tu km shauri yako utaua injini mapema.. ni vizuri kuangalia oil ipo kwenye hali gani hasa kama gari ina kaa sana kwenye folen injini ikiwa on.

Pia kama ni mtu unatembea short distance unazima gari mara unawasha zima kila wakati.. hii pia hufanya oil iwe contaminated na gasoline.. kumbuka gari inapowaka injekta (fuel injectors) humwaga mafuta mengi ila kufanya gari iwake, so sio mafuta yote huungua, mengine hupenya na kwenda kwenye sump ya oil, so haya yanayopenya huenda ku contaminate oil na kuifanya oil ipungue ubora wake with time.

Pia kama unasafiri zaid ya miezi sita na gar ikakaa 6months bila kuwaka hata kama uliondoka umeweka oil mpya ukija toa hiyo oil weka nyingine.

Interval ya oil changing.. kama watumia mineral oil kwa mazingira yetu ya kitropic na hizi folen za mjini change oil from 2500km to 3000km.. na hakikisha watumia quality oil zisizokua na rate kubwa ya utengenezaji wa carbon au rate kubwa ya oxidation.

Kwa wa synthetic oil change after every 5000km na sio kwenda mpaka km7000-10,000 hata kama watumia liquimo oil. (Na hapa lazima uwe na uhakika gari yako haina tatizo la kula oil. Kama inakula oil utakuta unaweka hizi kwakua ni nyepesi mpaka unafika km 5000 unakuta umebakiwa na oil lita moja)


Kuhusiana na quality ya oil, tafuta oil zenye API rating nzuri hasa ukiwa na gari zenye GDI fuel system au pia ukiwa na Gari ya Turbo.

Kuhusiana na oil za gearbox (transmission fluid) weka recommended transmission fluid ambazo manufacturer wako ame recommend.. kama ni ATF-TYPE 4, CVT-TC, or CVT-FE, WS, NS-2 or3, Matic J, DSG nk.. ili mradi ni recommended.. and avoid universal transmission fluids.. na transmission hubadilishwa after at least every 30,000km but you can go more than that depending na mazingira gari inatumika..
 
Back
Top Bottom