Zifahamu Engine oil

Siyo kweli. Ingie kwenye mitandao ya magari Japani angalia gari nyingi ni zipi kati ya zilizotembea below 50k kms,100k km, na above 100k kms
 
Umeelezea vema sana aiseee.
 
Kwa nini kitaalamu.
Engine ikifisha 100K milage inakuwa imeshachoka kwahiyo engine itahitaji namba ya juu kidogo ya kuweza kuendana na friction.
5W -30 inafaa zaidi Kwa engine zenye milage ndogo(ni kama mafuta ya watoto ya kulainisha ngozi kutumiwa na MTU mzima aliyefikisha milage 100,000)
5W- 40 inafaa zaidi kwasababu ni nzito kidogo ambayo ni rahisi kulainisha Kwenye chuma chakavu
 
Habari mkuu,
Rumion ODO 90k inafaa oil number ngapi?
 
Sasa mbona hawa mafundi wetu mitaani wanaweka 20W-50 kwenye hivi vigari vyetu? Kuna fundi hapa yeye premio, IST, spacio, Rav 4 nk zote anaweka 20W-50 tu
 
Sasa mbona hawa mafundi wetu mitaani wanaweka 20W-50 kwenye hivi vigari vyetu? Kuna fundi hapa yeye premio, IST, spacio, Rav 4 nk zote anaweka 20W-50 tu
Ndiyo maana gari nyingi zinapoteza performance yake hata mlio wa engine unapotea ikiwemo ulaji wa mafuta hii yote inasababishwa na utumiaji wa oil isiyo sahihi..
Magari ya ulaya huwezi kufanya hivyo na likatembea ndani ya siku kadhaa mbele linakufa Tu, Sisi wabongo tupo nyuma Sana kwenye ufahamu juu ya magari tofauti na wenzetu kenya
 

Je wakati wa ku change oil ni lazima ku change na filter? Kuna mahala nimesoma kuwa sio lazima

Naomba kuelekezwa hapa

Hasa kwa gari za mjerumani
 
Wenyewe wanakwambia 5W-30 inafaa kwenye nchi za baridi kama huko ulaya, huku bongo kwa kuwa kuna joto kali na gari zenyewe zina millage zaidi ya 100,000km basi oil sahihi ni 20W-50. Hatari sana hawa local fundi.
 
Km 100,000 ni ndogo sana kwa injini mkuu..yaan kama wabadili oil kila baada ya km 3000 injini itakaa muda mrefu mno...kinacho chosha injini haswa hapa bongo ni matumizi ya oil substandard (hizi oil za madukan nyingi fake) nunua oil kwenye Petrol station..

Kingine kinacho chosha injini ni matumizi ya wrong oil viscosity...mfano mtu kanunua gari anatia oil SAE 40, or 20w-50. These are too thick oils... clearance ya moving parts ndani ya injini ni ndogo sana hivo inajitaji oil film ndogo sana na ndio essence ya 5w-30, or 5w-40 or 10w-40 not bad..so ukiweka thick oil inaongeza excessive pressure kwenye cylinder walls na rings za pistons then baada ya muda unakuta shida ina anza.

Kingine kinachoua injini ni kuto badili oil kwa wakati..( kama gari latumika mara kwa mara-yaan daily driven bila kupark kwa muda mrefu, bas change oil after every 3000 to 3500km bila kujali unatumia oil brand gan. kumbuka oil uchoka because of temperature na contamination.. sasa oil ikitumika muda mrefu bila kutolewa huanza kuganda..sasa ikiganda huwa ina ng'ang'ania piston ring-ile ring inayo kupangusa na kuzuia oil isije juu kwenye combustion chamber(nb hizi rings za gari za kisasa zina tension ndogo tofauti na zaman) sasa ring ikisha ng'ang'ania basi oil inakua haina kitu kinacho izuia isipande kwenye combustion chamber. Lakini pia kwakua ring ikisha ng'ang'ania sehemu moja basi unakuta ile sehemu ili ng'ang'ania inakua inakwangua cylinder wall kwa muda mrefu, matokeo yake cylinder bore ina tanuka sasa tatizo lingine lina jitokeza la cylinder bore kutanuka, sasa cylinder bore ikisha tanuka ndo utaanza ona kila aina ya tatizo la injini mara injini kutoa Moshi wa blue,mara miss zisizo isha, hizi miss ni kwakua compression imeshuka kwenye cylinder (miss inayo husiana na compression kushuka huwa aiishi mpaka utatue issue ya compression--unaweza badili kila aina ya makitu Kama plugs,coil,pump, nozzles ila Kama compression ni ndogo nothing gona work) lakini pia tatizo ligine compression ikisha shuka ni injini kutumia mafuta mengi sana, na kula oil.

Kwa watu wanao fanya short trips frequent (mfano katoka sinza kaenda mcity kazima gari, mara kawasha kaenda mwenge kazima, kawasha kaenda itv kazima..sasa short distance trip uharibu oil pia... what is happening ni kwamba every time you crank engine ,(kila unapowasha injini), basi mafuta mengi sana humwagwa kwenye combustion chamber ili kuwezesha gari kuwaka, sasa katika hali hii sio mafuta yote uhungua, mengine upenya kwenye cylinder walls kwenda kwenye sump ya oil..sasa haya mafuta yakisha ingia huko kwenye sump, contamination hutokea na kufanya oil iwe broken down..sasa hapa oil hupoteza properties zake za kua resistant to heat lakini pia ku provide required lubrication sasa baada ya muda mfupi oil huwa maji na kuua injini yako in long run..so ukiwa unafanya root fup muda mwingi basi badili oil kwa wakati.

Kuna Wale wenzangu anatembea km 5000 ndani ya mwaka mzima...ni hivi ikisha fika miezi 6 oil ipo ndan ya injini hata kama hautembei km 5000 ndan ya mwaka mzima basi oil isizidi miezi 6 bila kubadilishwa.


So in short gari nyingi hapa bongo tunaziua prematurely because of very simple reason oil.

Kwa kesi ya European cars zenyewe apart from issue za oil change, zenyewe zipo na inherent problem za durability kwenye upande wa drivetrain hasa kuanzia km100,000.

Change oil every 3000 to 3500km kwa watu wa DSM, kwa watu wa mikoani waweza enda mpaka km 4000 kwakua mikoani hakuna foleni.. lakini pia monitor oil consumption ya injini yako.maana kuna gari unaweka 4lts za oil baada ya km 1000 oil imebaki 2lts hii si mchezo

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Je wakati wa ku change oil ni lazima ku change na filter? Kuna mahala nimesoma kuwa sio lazima

Naomba kuelekezwa hapa

Hasa kwa gari za mjerumani
Toa filter weka nYingine...filter unafanya filtration ya debris zinazikua ndani ya engine na kuchuja contaminants nyingime zinazoweza athili injini. Ina chuja metal shavings sometimes incase ikitokea excessive wear. So usipo change inafika mahala inaziba....pia hizi filter watu inabidi watu wawe nazo makini maana nazo zaweza leta majanga hasa pale outlet zake zinapikua either ndogo sana or haziruhusu kiwango cha ktosha cha oil ili ikazunguke kwenye injini for adequate lubrication.hii ni topic ya siku nYingine.but oil filters nazo ni shida.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Pamoja Saanaa
 
90% ya oil filter ni fake hasa za Toyota
 
90% ya oil filter ni fake hasa za Toyota
Huwa sifundi oil filters za Toyota ..mara nyingi huwa natumia filter za GUD from South Africa...oil natumia total from total energy zinazo uzwa kwenye petrol station na si madukani. Natumia 5w-40 or 10w-30.. and I always change after 3000km.

Speaking of issue ya oil kwenye injini, fungu kile kifuniko cha kuingizia oil kwenye injini ya gari yako tizama chuma ndani ya injini through hicho kitundu rangi utayo iona inatakiwa iwe kama gold na kama patakua na black basi ujue shida imeasha anza ndani ya injini.. au tizama kifuniko cha oil, kama kina ukoko mwingi ndani basi hicho kifuniko kina represent uhalisia wa behavior yako ya kuchange oil.

Issue nyingine ya oil ni ujazaji wa oil bila kuacha nafasi ya expansion ya oil pindi inapokua ya moto...oil ikiwa under high temperature u expand sasa kama oil itakua imejazwa sana na expansion ikatokea ina maana oil ita overflow ...sasa kwakua over flow ya oil ipo very limited, basi ile excess oil either itapanda kwenye combustion chamber kuchomwa au itapasua internal seals na kuanza ku leak.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Synthentic Castrol unachange mpaka kms 10,000 ukipunguza 7,000. Siyo hizo za kms 3000, 3500.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…