Km 100,000 ni ndogo sana kwa injini mkuu..yaan kama wabadili oil kila baada ya km 3000 injini itakaa muda mrefu mno...kinacho chosha injini haswa hapa bongo ni matumizi ya oil substandard (hizi oil za madukan nyingi fake) nunua oil kwenye Petrol station..
Kingine kinacho chosha injini ni matumizi ya wrong oil viscosity...mfano mtu kanunua gari anatia oil SAE 40, or 20w-50. These are too thick oils... clearance ya moving parts ndani ya injini ni ndogo sana hivo inajitaji oil film ndogo sana na ndio essence ya 5w-30, or 5w-40 or 10w-40 not bad..so ukiweka thick oil inaongeza excessive pressure kwenye cylinder walls na rings za pistons then baada ya muda unakuta shida ina anza.
Kingine kinachoua injini ni kuto badili oil kwa wakati..( kama gari latumika mara kwa mara-yaan daily driven bila kupark kwa muda mrefu, bas change oil after every 3000 to 3500km bila kujali unatumia oil brand gan. kumbuka oil uchoka because of temperature na contamination.. sasa oil ikitumika muda mrefu bila kutolewa huanza kuganda..sasa ikiganda huwa ina ng'ang'ania piston ring-ile ring inayo kupangusa na kuzuia oil isije juu kwenye combustion chamber(nb hizi rings za gari za kisasa zina tension ndogo tofauti na zaman) sasa ring ikisha ng'ang'ania basi oil inakua haina kitu kinacho izuia isipande kwenye combustion chamber. Lakini pia kwakua ring ikisha ng'ang'ania sehemu moja basi unakuta ile sehemu ili ng'ang'ania inakua inakwangua cylinder wall kwa muda mrefu, matokeo yake cylinder bore ina tanuka sasa tatizo lingine lina jitokeza la cylinder bore kutanuka, sasa cylinder bore ikisha tanuka ndo utaanza ona kila aina ya tatizo la injini mara injini kutoa Moshi wa blue,mara miss zisizo isha, hizi miss ni kwakua compression imeshuka kwenye cylinder (miss inayo husiana na compression kushuka huwa aiishi mpaka utatue issue ya compression--unaweza badili kila aina ya makitu Kama plugs,coil,pump, nozzles ila Kama compression ni ndogo nothing gona work) lakini pia tatizo ligine compression ikisha shuka ni injini kutumia mafuta mengi sana, na kula oil.
Kwa watu wanao fanya short trips frequent (mfano katoka sinza kaenda mcity kazima gari, mara kawasha kaenda mwenge kazima, kawasha kaenda itv kazima..sasa short distance trip uharibu oil pia... what is happening ni kwamba every time you crank engine ,(kila unapowasha injini), basi mafuta mengi sana humwagwa kwenye combustion chamber ili kuwezesha gari kuwaka, sasa katika hali hii sio mafuta yote uhungua, mengine upenya kwenye cylinder walls kwenda kwenye sump ya oil..sasa haya mafuta yakisha ingia huko kwenye sump, contamination hutokea na kufanya oil iwe broken down..sasa hapa oil hupoteza properties zake za kua resistant to heat lakini pia ku provide required lubrication sasa baada ya muda mfupi oil huwa maji na kuua injini yako in long run..so ukiwa unafanya root fup muda mwingi basi badili oil kwa wakati.
Kuna Wale wenzangu anatembea km 5000 ndani ya mwaka mzima...ni hivi ikisha fika miezi 6 oil ipo ndan ya injini hata kama hautembei km 5000 ndan ya mwaka mzima basi oil isizidi miezi 6 bila kubadilishwa.
So in short gari nyingi hapa bongo tunaziua prematurely because of very simple reason oil.
Kwa kesi ya European cars zenyewe apart from issue za oil change, zenyewe zipo na inherent problem za durability kwenye upande wa drivetrain hasa kuanzia km100,000.
Change oil every 3000 to 3500km kwa watu wa DSM, kwa watu wa mikoani waweza enda mpaka km 4000 kwakua mikoani hakuna foleni.. lakini pia monitor oil consumption ya injini yako.maana kuna gari unaweka 4lts za oil baada ya km 1000 oil imebaki 2lts hii si mchezo
Sent from my TECNO KC8 using
JamiiForums mobile app