Zifahamu mbinu za kuondoa umasikini katika familia πŸ‘¨β€πŸ‘©β€πŸ‘§β€πŸ‘¦

Zifahamu mbinu za kuondoa umasikini katika familia πŸ‘¨β€πŸ‘©β€πŸ‘§β€πŸ‘¦

Joined
May 16, 2022
Posts
22
Reaction score
57
Umasikini ni tatizo kubwa hususani ktk mataifa yanayoendelea kama Tanzania. Sababu za umasikini ni ujinga,maradhi , uzalishaji hafifu ktk shughuli za kiuchumi kama kilimo, viwanda na biashara. Vilevile umasikini husababishwa na mfumo mbovu wa elimu.

Hoja zifuatazo zitaeleza kuhusu mbinu za kuondoa umasikini katika familia.

1. Umasikini unaweza kuondolewa Kwa kujifunza elimu ya fedha na elimu ya kujiendeleza ( self development ) ; mifumo ya Dunia inayotawaliwa na mzungu ilianzisha aina kuu mbili za elimu ambazo ni scholarstic education pamoja na formal education. Ukisikia scholarstic education ni elimu inayomtaka mwanafunzi kujua kusoma ,kuandika na kuhesabu na hiyo formal ni Ile Inayomtaka mwanafunzi asome na kuhitimu kiwango Fulani Cha elimu yaani kama ni degree au masters nk. Sasa wataaalamu, life coaches, public speakers na watafiti wamegundua aina nyingine za elimu ,lkn Kwa Leo nitagusia aina mbili tu ambazo ni self development pamoja na financial education ( elimu ya fedha). Kulingana na mafundisho ya @ Joel Nanauka anasema elimu ya fedha ni elimu ambayo Ina umuhimu mkubwa hususani Kwa Sasa ktk ulimwengu huu.Familia zetu za kiafrika # watz twapaswa kujifunza kuhusu financial education ili kuondoa umasikini katika familia kwasababu husaidia katika kujenga thamani ya fedha pamoja na kukuza thamani ya fedha inayopatikana. Elimu ya kategoria ya pili ni elimu ya kujiendeleza ( self development education) ambapo familia nyingi hamna elimu hii inayojikita katika kumjengea mtu personal and interpersonal skills . Elimu hii hupatikan Kwa kusoma vitabu,kusoma makala mbalimbali nk.

2. Kuanzisha miradi mbalimbali; ss suala hili linawahusu zaidi wazazi, walezi na ndugu ambao wanaendesha familia ." My fellow Tanzanians" umasikini hauwezi ondoka Kwa kulaumu serikali Bali ni Kwa kuanzisha miradi mbalimbali katika familia itakayokuwa ni chanzo Cha ajira Kwa watoto.kuliko kuwa na maisha ya kifahari na kula bata anzisha investment ambazo zitasaidia watoto na wajukuu wako.

3. Umasikini unaweza kuondolewa Kwa kufanya savings ; Sasa hapa ndio Kuna tatizo kubwa hususani ktk familia nyingi za tz Kwa sababu kuweka savings ( akiba ) siyo utamaduni wetu hata kidogo lakini ni vizuri sana kuweka akiba. Kuna namna mbalimbali za kuweka akiba kama kupitia kibubu( wengi tumezoea ) ,kuweka fedha bank,kuweka fedha kupitia saccos na vikoba. Mathalani inashauriwa kutunza akiba Kwa ajili ya watoto wako,ili kuondoa utegemezi uliopitiliza .Sasa tatizo lingine ni kuwa wazazi wengi wanashindwa kutofautisha kati ya kuwekeza na kuwajibika Kwa mtoto wako. Unaposomesha mtoto unawajibika lakini unapomuwekea akiba unainvest ss.

4. Kugundua na kuibua vipaji ktk familia; Leo hii watu wanamfahamu Lionel Messi kutokana na uwezo wake wa kucheza soka na pesa nyingi anazolipwa lakini wanasahau kuwa katika familia ya Messi ,bibi yake ndiye aliyegundua kipaji hicho na kufanya wao kuwa familia tajiri na yenye mafanikio. Ndugu wazaz njia moja wapo ya kuondoa umasikini katika familia ni kugundua na kuibua vipaji vilivyopo maana huwezi jua kipaji hicho kitasaidia vp Dunia . Leo hii katika Dunia hii tunamfahamu sharuk Khan lakini watu wanasahau kuwa mama yake ndiye aliyeibua kipaji Hiko. Hivyo tusipuuzie talents πŸ˜ƒπŸ˜ƒ

5. Kuhimiza ufanyaji wa kazi za mikono; hili lipo katika malezi Sasa umasikini ni tabia kama ilivyo Kwa utajiri . Na utajiri huletwa Kwa kufanya kazi . Pongezi Kwa wazazi wote strict wanaohimiza watoto wao kufanya kazi Kwa bidii na kutokuwa mzigo. Kuajiri mayaya kumekithiri na kufanya watoto washindwe kufanya shughuli hapo nyumbani na kuinfluence uvivu. Faida za kufanya kazi ni kwamba husaidia kukuza ubunifu, uwajibikaji na kuandaa kizazi Cha wafanya kazi.

Thanks for reading πŸ€—πŸ€—πŸ€—πŸ€—
 
Inshaallah nitajitahidi kuzingatia hizo points hapo juu, umasikini mbaya sana
 
1. Kutonunua vitu ambavyo hamuviitaji
2. Kutokua na mahusiano ya kingono nje ya familia
3. Kutoruhusu kabisa uvivu katika familia
4. Kuhakikisha dira ya familia kwa uwazi kabisa inafamika na wana familia wote kuanzia mkubwa mpaka mdogo ili kila mmoja ajue mchango wake kwenye kutimiza malengo ya familia
5. Kuchagua mumtegemee Mungu mwenye nguvu au shetani mwenye nguvu kamwe hamuwezi kutoboa kama ni vugu vugu hamjulikani mpo team gani
( Huu ni ukweli mchungu sana hila ndio hatuna jinsi kama huna Mungu ndugu yangu unashetani utake usitake )
 
Umesahau uchawi katika familia na Koo mbali mbali ni chanzo Cha umaskini pia, kuroga wasomi, kuwazuia katika shughuli mbali mb

1. Kutonunua vitu ambavyo hamuviitaji
2. Kutokua na mahusiano ya kingono nje ya familia
3. Kutoruhusu kabisa uvivu katika familia
4. Kuhakikisha dira ya familia kwa uwazi kabisa inafamika na wana familia wote kuanzia mkubwa mpaka mdogo ili kila mmoja ajue mchango wake kwenye kutimiza malengo ya familia
5. Kuchagua mumtegemee Mungu mwenye nguvu au shetani mwenye nguvu kamwe hamuwezi kutoboa kama ni vugu vugu hamjulikani mpo team gani
( Huu ni ukweli mchungu sana hila ndio hatuna jinsi kama huna Mungu ndugu yangu unashetani utake usitake )
Asante boss Kwa mchango wako
 
Umeandika vizuri sana nakazaia. .

UMASKINI NI ROHO na hata mwingine akipata mabilioni bado anakuwa maskini. Utajiri au Umaskini unaishi ndani ya mtu. .
 
Pont zote ni sawa ila ya namba tano sio kweli huko ulaya , marekani na asia Kuna watu hawana dini kabisa na Wana pesa chafu..
Ila wanafanya kazi kwa bidii hasa..
 
Umeandika vizuri sana nakazaia. .

UMASKINI NI ROHO na hata mwingine akipata mabilioni bado anakuwa maskini. Utajiri au Umaskini unaishi ndani ya mtu. .
Ni roho kivip? Na utajiri ni roho pia?

Ayo mabilion yanakua yamepotea au anakua nayo afu bado ni maskini?
 
Umasikini ni laana, umasikini ni tabia, umasikini unaondoka kwa kukataa tabia za kimasikini na kukata connection au muunganiko wowote na mizimu
 
Ni roho kivip? Na utajiri ni roho pia?

Ayo mabilion yanakua yamepotea au anakua nayo afu bado ni maskini?
Roho ni nguvu isiyoonekana iliyo nyuma ya mtu ambayo ndio uamua mstakabari wa maisha ya mtu kimwili.
Matendo ya mtu, mafanikio ya mtu ,tabia ya mtu ni matokeo ya roho iliyomo ndani mwake.Roho utoka sehemu mbili kwa Mungu au Shetani.
Hizi ni roho zitokazo kwa shetani
Uongo, uvivu, hasira, umasikini, ulevi, uzinzi, wizi, ushoga, ubinafsi na zifananazo na hayo.
Roho toka kwa Mungu
Uadilifu, Kazi, bidii, utoaji, usafi, hekima, busara, na yafananayo na hayo.
 
Ardhi pasipo kujari Ina rutuba au ubora wake ndio msingi pekee au mtaji wa kumkwamua mtu yeyeto au ukoo dhidi ya umasikini. Ardhi ni basic starting point ya kumkwamua mtu dhidi ya umasikini.
 
Kila Familia ina njia yake ya pekee inayoweza kujikwamua ktk Umaskini,Hizo ulizotaja ni njia ambazo mtu Alizigundua kutokana na Kusoma Changamoto za kwenye Familia yake,huenda kweli zikanisaidia au zikafeli zote na kuniletea matatizo zaidi...Aliyegundua hizo njia sidhani km anajua km huku kwetu kuna Utamaduni wa Kurogana unapoanza kufanikiwa!!!
Afrika tushtuke,Hakuna mzungu atagundua kitu kwa kuzingatia kuna Waafrika Duniani.

images.jpg
 
Ni roho kivip? Na utajiri ni roho pia?

Ayo mabilion yanakua yamepotea au anakua nayo afu bado ni maskini?
Kwangu mimi utajiri ni nadharia tu. Kwani kipimbo cha utajiri ni kipi? mabilioni?
1. Kuna mwingine kuwa na watoto tu ni utajiri tosha.
2. Mwingine hajawahi kupungukiwa na kitu ana kila anachokihitaji pia na utajiri tosha.
3. Wamasai wana ngo'ombe wengi pia ni utajiri tosha.
4. Hata kuwa na afya njema husumbuliwi na magonjwa ni utajiri tosha.
5. Ukiwa na moyo wa kujitoa kwa wengine huo ji utajiri mkubwa,
Mimi binafsi mtu ambae ana kila anachokihitaji na karidhika ni utajiri tosha. .

Kwa nini nimesema umaskini ni roho?
Unakuta mtu ana hela nyingi lakini hata
1.Usingizi halali,
2. Anatamani hata vya wengine na kuwanyang'amnya wale wasio nacho,
3 Hana amani ndani yake,
4. Hata akila kitu nafsi yake haiburudiki
5. Kikubwa hata utajiri wake haumpi furaha, kwangu huyu ni masikini mkubwa. .
 
Umesahau uchawi katika familia na Koo mbali mbali ni chanzo Cha umaskini pia, kuroga wasomi, kuwazuia katika shughuli mbali mbali,
Uchawi unakudhuru kama uzijui mbinu na codes zao,ukivijua vizuia uchawi utawaona ni wapumbavu tu.
Uchawi hauna nguvu kubwa Sana zaidi ya kubebwa na propaganda zaidi.
 
Kila Familia ina njia yake ya pekee inayoweza kujikwamua ktk Umaskini,Hizo ulizotaja ni njia ambazo mtu Alizigundua kutokana na Kusoma Changamoto za kwenye Familia yake,huenda kweli zikanisaidia au zikafeli zote na kuniletea matatizo zaidi...Aliyegundua hizo njia sidhani km anajua km huku kwetu kuna Utamaduni wa Kurogana unapoanza kufanikiwa!!!
Afrika tushtuke,Hakuna mzungu atagundua kitu kwa kuzingatia kuna Waafrika Duniani.
Kurogwa kunazuilika
 
Back
Top Bottom