Zifahamu mbinu za kuondoa umasikini katika familia 👨‍👩‍👧‍👦

Zifahamu mbinu za kuondoa umasikini katika familia 👨‍👩‍👧‍👦

Umasikini ni tatizo kubwa hususani ktk mataifa yanayoendelea kama Tanzania. Sababu za umasikini ni ujinga,maradhi , uzalishaji hafifu ktk shughuli za kiuchumi kama kilimo, viwanda na biashara. Vilevile umasikini husababishwa na mfumo mbovu wa elimu.

Hoja zifuatazo zitaeleza kuhusu mbinu za kuondoa umasikini katika familia.

1. Umasikini unaweza kuondolewa Kwa kujifunza elimu ya fedha na elimu ya kujiendeleza ( self development ) ; mifumo ya Dunia inayotawaliwa na mzungu ilianzisha aina kuu mbili za elimu ambazo ni scholarstic education pamoja na formal education. Ukisikia scholarstic education ni elimu inayomtaka mwanafunzi kujua kusoma ,kuandika na kuhesabu na hiyo formal ni Ile Inayomtaka mwanafunzi asome na kuhitimu kiwango Fulani Cha elimu yaani kama ni degree au masters nk. Sasa wataaalamu, life coaches, public speakers na watafiti wamegundua aina nyingine za elimu ,lkn Kwa Leo nitagusia aina mbili tu ambazo ni self development pamoja na financial education ( elimu ya fedha). Kulingana na mafundisho ya @ Joel Nanauka anasema elimu ya fedha ni elimu ambayo Ina umuhimu mkubwa hususani Kwa Sasa ktk ulimwengu huu.Familia zetu za kiafrika # watz twapaswa kujifunza kuhusu financial education ili kuondoa umasikini katika familia kwasababu husaidia katika kujenga thamani ya fedha pamoja na kukuza thamani ya fedha inayopatikana. Elimu ya kategoria ya pili ni elimu ya kujiendeleza ( self development education) ambapo familia nyingi hamna elimu hii inayojikita katika kumjengea mtu personal and interpersonal skills . Elimu hii hupatikan Kwa kusoma vitabu,kusoma makala mbalimbali nk.

2. Kuanzisha miradi mbalimbali; ss suala hili linawahusu zaidi wazazi, walezi na ndugu ambao wanaendesha familia ." My fellow Tanzanians" umasikini hauwezi ondoka Kwa kulaumu serikali Bali ni Kwa kuanzisha miradi mbalimbali katika familia itakayokuwa ni chanzo Cha ajira Kwa watoto.kuliko kuwa na maisha ya kifahari na kula bata anzisha investment ambazo zitasaidia watoto na wajukuu wako.

3. Umasikini unaweza kuondolewa Kwa kufanya savings ; Sasa hapa ndio Kuna tatizo kubwa hususani ktk familia nyingi za tz Kwa sababu kuweka savings ( akiba ) siyo utamaduni wetu hata kidogo lakini ni vizuri sana kuweka akiba. Kuna namna mbalimbali za kuweka akiba kama kupitia kibubu( wengi tumezoea ) ,kuweka fedha bank,kuweka fedha kupitia saccos na vikoba. Mathalani inashauriwa kutunza akiba Kwa ajili ya watoto wako,ili kuondoa utegemezi uliopitiliza .Sasa tatizo lingine ni kuwa wazazi wengi wanashindwa kutofautisha kati ya kuwekeza na kuwajibika Kwa mtoto wako. Unaposomesha mtoto unawajibika lakini unapomuwekea akiba unainvest ss.

4. Kugundua na kuibua vipaji ktk familia; Leo hii watu wanamfahamu Lionel Messi kutokana na uwezo wake wa kucheza soka na pesa nyingi anazolipwa lakini wanasahau kuwa katika familia ya Messi ,bibi yake ndiye aliyegundua kipaji hicho na kufanya wao kuwa familia tajiri na yenye mafanikio. Ndugu wazaz njia moja wapo ya kuondoa umasikini katika familia ni kugundua na kuibua vipaji vilivyopo maana huwezi jua kipaji hicho kitasaidia vp Dunia . Leo hii katika Dunia hii tunamfahamu sharuk Khan lakini watu wanasahau kuwa mama yake ndiye aliyeibua kipaji Hiko. Hivyo tusipuuzie talents [emoji2][emoji2]

5. Kuhimiza ufanyaji wa kazi za mikono; hili lipo katika malezi Sasa umasikini ni tabia kama ilivyo Kwa utajiri . Na utajiri huletwa Kwa kufanya kazi . Pongezi Kwa wazazi wote strict wanaohimiza watoto wao kufanya kazi Kwa bidii na kutokuwa mzigo. Kuajiri mayaya kumekithiri na kufanya watoto washindwe kufanya shughuli hapo nyumbani na kuinfluence uvivu. Faida za kufanya kazi ni kwamba husaidia kukuza ubunifu, uwajibikaji na kuandaa kizazi Cha wafanya kazi.

Thanks for reading [emoji847][emoji847][emoji847][emoji847]
Unaweza ukafanya yote hayo lakini tatizo kuna kulogana na hauchomoi kirahisi
 
Uchawi unakudhuru kama uzijui mbinu na codes zao,ukivijua vizuia uchawi utawaona ni wapumbavu tu.
Uchawi hauna nguvu kubwa Sana zaidi ya kubebwa na propaganda zaidi.
Code zipi?, unaweza kuelezea
 
1. Kutonunua vitu ambavyo hamuviitaji
2. Kutokua na mahusiano ya kingono nje ya familia
3. Kutoruhusu kabisa uvivu katika familia
4. Kuhakikisha dira ya familia kwa uwazi kabisa inafamika na wana familia wote kuanzia mkubwa mpaka mdogo ili kila mmoja ajue mchango wake kwenye kutimiza malengo ya familia
5. Kuchagua mumtegemee Mungu mwenye nguvu au shetani mwenye nguvu kamwe hamuwezi kutoboa kama ni vugu vugu hamjulikani mpo team gani
( Huu ni ukweli mchungu sana hila ndio hatuna jinsi kama huna Mungu ndugu yangu unashetani utake usitake )
Ufafanuzi wa pointi namba mbili tafadhali.
 
Ufafanuzi wa pointi namba mbili tafadhali.
1. Kijamii
Unapokua na mahusiano ya kingono nje ya familia yanaweza kupunguza ufanisi wa kazi , kukuharibia kazi au biashara , kukutesa kisaikolojia muda mwengine kiasi cha kushindwa kuhusiana vyema na jamii ila kubwa kabisa mwisho wake ni kupotesa imani ya jamii juu yako ninapo sema jamii na maanisha professional wise & non professional one [ me / ke ]
2. Kiuchumi
Ni lazima uchumi hugawanywe hakuna jinsi hilo linategemea demand over supply ya wahusika wanaotakiwa kupewa keki hili linawamaliza sana wanaume
Wanawake ni kupuuzia mahitaji ya familia na kuwekeza pesa ili wawavutie wanaowapa penzi
Hili husababisha familia kukosa dira moja ya maendeleo kupelekea umasikini
3. kiimani
Uzinzi ni zambi na mshahara wa zambi ni mauti , bro uchumi wenu lazima ufe kibudu
 
Unawezaje:
1. Kufanya saving kama wewe ni maskini?
2. Kuanzisha miradi kama wewe ni maskini?
Ilo la pili bado sijawai fanya mkuu personal ila kushiriki miradi ya wengine nishawai kidogo.
Ila savings mkuu ni kutengeneza mfumo tu na nidhamu kama umeajiriwa au umejiajiri
% mahitaji binafisi
% mahitaji ya familia [ mahusiano]
% kula maisha
% sadaka [ zaka nk]
% emergency
% savings

Iyo ni kwamimi nilie peke yangu bado sijaoa .....mimi nafanya hivyo
 
Pont zote ni sawa ila ya namba tano sio kweli huko ulaya , marekani na asia Kuna watu hawana dini kabisa na Wana pesa chafu..
Ila wanafanya kazi kwa bidii hasa..
Sasa wewe unaekaa huku bongo, unataka kufuata formula ya Ulaya, jaribu uone kama utatoboa.
IMG-20220508-WA0002.jpg
 
Hii njia nayo inaondoa umasikini haraka.
Njia rahisi ya kuondokana na umasikini kwa mtu asiye na kipato.
Ardhi still bado ndio mtaji rahisi wa kutokea kimaisha.
Nje ya mji mapori tele yamejaa hata bure au kukodi unaweza pata safisha angalau si chini ya heka 10,panda mazao yasiyo na changamoto mfano kunde, alizeti, mtama, nk.
Chukua zao moja hili ni uhakika.
Baada ya kusafisha heka 10 au zaidi panda mmea wa nyonyo castro oil huu unavuna baada ya miezi 3 na utaendelea kuvuna kwa mda wa miaka 2.
Heka moja ya nyonyo utapata gunia 15 ukizikamua utapata lita 500 za mafuta, so heka 10 ni lita elf 5.
Jifunze kutengeneza sabuni za mche za mawingu
Lita moja ya mafuta utapata miche 2 mara lita elf 5 utapata miche elf 10.
Uza mche kwa sh 1500 mara elf 10 utapata milioni 15.
Jinsi ya kutengeneza mashine ya kukamua mbegu za mafuta tafuta bomba inchi nne tafuta Nondo mm 12 ikunje mfano wa spring ingiza ndani ya bomba mbele ya bomba ziba acha tundu dogo.Toboa toboa Bomba vitundu vidogo Ili mafuta yamwagike chini, weka mshikio wa kunyongea Ili ukamue mafuta.
Ukipata pesa kodi nyumba nenda viwandani kafunge bidhaa ambazo ni daily use kisha jaza kwenye nyumba uliyokodi kisha uwe tengeneza network na wauzaji wa dogo uwe unawasambazia bidhaa wanazoishiwa.
Kwa kufanya hivi ndani ya mwaka utakua mbali sana utaoa, utajenga, nk.
 
Aina za marafiki pia wanaweza kukufanya uwe maskini.
True maana kuna watu wengine Wana laana ya umasikini so ukishirikiano nao kutoka ni ngumu, ukiona unafanya jambo KILA mara na the Same rafiki na halifanikiwi, badili ushirika ,
 
Back
Top Bottom