Zifahamu mbinu za kuondoa umasikini katika familia πŸ‘¨β€πŸ‘©β€πŸ‘§β€πŸ‘¦

Yote ni ubatili tu na kujilisha upepo.
 
Unaweza ukafanya yote hayo lakini tatizo kuna kulogana na hauchomoi kirahisi
 
Uchawi unakudhuru kama uzijui mbinu na codes zao,ukivijua vizuia uchawi utawaona ni wapumbavu tu.
Uchawi hauna nguvu kubwa Sana zaidi ya kubebwa na propaganda zaidi.
Code zipi?, unaweza kuelezea
 
Ufafanuzi wa pointi namba mbili tafadhali.
 
Ufafanuzi wa pointi namba mbili tafadhali.
1. Kijamii
Unapokua na mahusiano ya kingono nje ya familia yanaweza kupunguza ufanisi wa kazi , kukuharibia kazi au biashara , kukutesa kisaikolojia muda mwengine kiasi cha kushindwa kuhusiana vyema na jamii ila kubwa kabisa mwisho wake ni kupotesa imani ya jamii juu yako ninapo sema jamii na maanisha professional wise & non professional one [ me / ke ]
2. Kiuchumi
Ni lazima uchumi hugawanywe hakuna jinsi hilo linategemea demand over supply ya wahusika wanaotakiwa kupewa keki hili linawamaliza sana wanaume
Wanawake ni kupuuzia mahitaji ya familia na kuwekeza pesa ili wawavutie wanaowapa penzi
Hili husababisha familia kukosa dira moja ya maendeleo kupelekea umasikini
3. kiimani
Uzinzi ni zambi na mshahara wa zambi ni mauti , bro uchumi wenu lazima ufe kibudu
 
Unawezaje:
1. Kufanya saving kama wewe ni maskini?
2. Kuanzisha miradi kama wewe ni maskini?
Ilo la pili bado sijawai fanya mkuu personal ila kushiriki miradi ya wengine nishawai kidogo.
Ila savings mkuu ni kutengeneza mfumo tu na nidhamu kama umeajiriwa au umejiajiri
% mahitaji binafisi
% mahitaji ya familia [ mahusiano]
% kula maisha
% sadaka [ zaka nk]
% emergency
% savings

Iyo ni kwamimi nilie peke yangu bado sijaoa .....mimi nafanya hivyo
 
Pont zote ni sawa ila ya namba tano sio kweli huko ulaya , marekani na asia Kuna watu hawana dini kabisa na Wana pesa chafu..
Ila wanafanya kazi kwa bidii hasa..
Sasa wewe unaekaa huku bongo, unataka kufuata formula ya Ulaya, jaribu uone kama utatoboa.
 
Hii njia nayo inaondoa umasikini haraka.
Njia rahisi ya kuondokana na umasikini kwa mtu asiye na kipato.
Ardhi still bado ndio mtaji rahisi wa kutokea kimaisha.
Nje ya mji mapori tele yamejaa hata bure au kukodi unaweza pata safisha angalau si chini ya heka 10,panda mazao yasiyo na changamoto mfano kunde, alizeti, mtama, nk.
Chukua zao moja hili ni uhakika.
Baada ya kusafisha heka 10 au zaidi panda mmea wa nyonyo castro oil huu unavuna baada ya miezi 3 na utaendelea kuvuna kwa mda wa miaka 2.
Heka moja ya nyonyo utapata gunia 15 ukizikamua utapata lita 500 za mafuta, so heka 10 ni lita elf 5.
Jifunze kutengeneza sabuni za mche za mawingu
Lita moja ya mafuta utapata miche 2 mara lita elf 5 utapata miche elf 10.
Uza mche kwa sh 1500 mara elf 10 utapata milioni 15.
Jinsi ya kutengeneza mashine ya kukamua mbegu za mafuta tafuta bomba inchi nne tafuta Nondo mm 12 ikunje mfano wa spring ingiza ndani ya bomba mbele ya bomba ziba acha tundu dogo.Toboa toboa Bomba vitundu vidogo Ili mafuta yamwagike chini, weka mshikio wa kunyongea Ili ukamue mafuta.
Ukipata pesa kodi nyumba nenda viwandani kafunge bidhaa ambazo ni daily use kisha jaza kwenye nyumba uliyokodi kisha uwe tengeneza network na wauzaji wa dogo uwe unawasambazia bidhaa wanazoishiwa.
Kwa kufanya hivi ndani ya mwaka utakua mbali sana utaoa, utajenga, nk.
 
Aina za marafiki pia wanaweza kukufanya uwe maskini.
True maana kuna watu wengine Wana laana ya umasikini so ukishirikiano nao kutoka ni ngumu, ukiona unafanya jambo KILA mara na the Same rafiki na halifanikiwi, badili ushirika ,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…