Faida za kutumia email ya kampuni
Uaminifu: Siku zote wateja hupenda kufanya biashara na watu wanao waamiini. Kwa kutumia emails za kampuni kutakusaidia kujenga uaminifu kwa wateja na kuondoa maswali maswali.
Inakufanya uwe kikazi zaidi: Wazo la haraka ambalo huwajia watu pindi wanapopokea email yako toka gmail au Yahoo ni kuwa, huyu hayupo makini na kazi yake. Hata email hana bado anatumia Gmail kikazi. Hivyo epuka kupoteza thamani na kuonekana haupo makini.
Inaongeza upatikanaji wako online: Email za kampuni hubeba jina la kampuni, kwa mfano, unatumia info@yourbusiness. com, hii inamaanisha mtu akienda yourbusiness. com ataonana na website yako. Hata kama hauna Website, unaweza kuweka kurasa ya matengenezo ya website (Under Construction page) na taarifa kadhaa zinazotoa ujumbe wa biashara yako.
Msaada wa haraka: Kwa kutumia email za kampuni, inakuwezesha kupata msaada wa haraka pale unapokutana na tatizo lolote, mfano kuvamiwa na hackers nk kwakuwa unakuwa umejiunga na huduma ya malipo toka kwa kamouni husika.