Zijue faida za mafanikio ya Yanga kubezwa

Zijue faida za mafanikio ya Yanga kubezwa

KAGAMEE

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2013
Posts
4,457
Reaction score
5,454
Nimemsikia Ahmed Ally akibeza mafanikio ya Yanga kwamba imekutana na vibonge kwa hatua zote alizopita,swali ambalo semaji la CAF hawezi kujibu ni kwamba je Yanga imebeba ubingwa wa NBC Simba akiwa wapi?(Ambayo ni timu imara na giant zaidi ya Yanga?) Achana na hilo swali utapigwa makofi.

Wapo wanasimba wachache wanaokubali Yanga imeimprove sana na imeizidi mbali mno timu yao kimataifa lakini lipo kundi lingine ambalo binafsi nalipenda na nataman waendelee kubeza mafanikio ya Yanga ili iwafanye viongozi wangu waone safari bado.

Zifuatazo ni faida za kubezwa kwa mafanikio ya Yanga.

1. Itafanya viongozi kusajili MAWINGER mawili matata sana kwa ajili ya klabu Bingwa.Itatufanya mashabiki tuendelee kuvimba mtaani.

2. Itafanya wachezaji wasibweteke na waone hayo mafanikio ni ya kawaida sana na watakuwa na spirit ya kuleta kombe la Klabu bingwa Afrika. Huku mashabiki tukiendelea kuvimba mtaani.

3. Tunabezwa hatuna uwanja. Hii itapelekea viongozi kupambana na kujenga uwanja.Hilo nalo litatufanya tuzidi kuvimba kitaa.

NB: Simba wako vizuri sana wamecheza na giants Africa na kufika ROBO FAINAL kwa miaka 5 sasa hivyo mashabiki hawawadai wachezaji😊.

Natamani sana Yanga iendelee kubezwa ili izidi kujiimarisha zaidi.

Mwanafainali ongeza faida zingine.
 
Kama kubezwa kunawaletea faida sa iweje wabezaji tubezwe tena?

Mnatubeza kutukata moyo tushindwe kuwabeza mshindwe kufanya makubwa, huoni hapo adui wa nyie ni nyie wenyewe?

Kwanini msitupe pongezi wabezaji kwa namna tulivyohusika kwenye mafanikio yenu na badala yake mnatusimanga mpaka tunakosa raha wakati hii nchi yetu wote? (jana baada ya mechi yenu sijatoka nje)

Kwanini tunatungiwa majina ya maudhi wakati nyuma ya mafanikio yenu tupo sisi? (wabezaji)
 
Kama kubezwa kunawaletea faida sa iweje wabezaji tubezwe tena?

Mnatubeza kutukata moyo tushindwe kuwabeza mshindwe kufanya makubwa, huoni hapo adui wa nyie ni nyie wenyewe...
Hongera mkuu
 
Naomba Yanga ishinde kombe la shirikisho na baadaye msimu unaokuja tujipange kuchukua klabu bingwa. Klabu bingwa ndio iwe lengo la Yanga bila kuacha makombe ya ndani.
Mmekutana na tuvibonde tu leo mnaota CAFCL Mnadhani kule wako vibonde [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Nawahakikishia msimu ujao safari mtaishia round ya kwanza tu
 
Mmekutana na tuvibonde tu leo mnaota CAFCL Mnadhani kule wako vibonde [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Nawahakikishia msimu ujao safari mtaishia round ya kwanza tu
Namshangaa anapopiga hesabu za Club Bingwa wakati huko ndiko walipoanzaia.

Yani anapoitaja Club Bingwa ni kama vile alianzia shirikisho moja kwa moja
 
Kama kubezwa kunawaletea faida sa iweje wabezaji tubezwe tena?

Mnatubeza kutukata moyo tushindwe kuwabeza mshindwe kufanya makubwa, huoni hapo adui wa nyie ni nyie wenyewe...
Kwa hiyo mna sehemu yenu kwenye mafanikio ya Yanga?
 
Ahmed Ally ni kichaa anayevaa suti.

2020/21 kulikuwa na COVD 19 Nchi nyingi ligi ilisimama.TZ haijasimama.

Simba ilifika wapi?
 
Kama kubezwa kunawaletea faida sa iweje wabezaji tubezwe tena?

Mnatubeza kutukata moyo tushindwe kuwabeza mshindwe kufanya makubwa, huoni hapo adui wa nyie ni nyie wenyewe?

Kwanini msitupe pongezi wabezaji kwa namna tulivyohusika kwenye mafanikio yenu na badala yake mnatusimanga mpaka tunakosa raha wakati hii nchi yetu wote? (jana baada ya mechi yenu sijatoka nje)

Kwanini tunatungiwa majina ya maudhi wakati nyuma ya mafanikio yenu tupo sisi? (wabezaji)
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣Pole mkuu
 
Back
Top Bottom