Zijue fursa zilizopo kwa Kila mkoa ili uamue vyema sehemu sahihi ya kuishi na kuwekeza kwa muda mrefu

Zijue fursa zilizopo kwa Kila mkoa ili uamue vyema sehemu sahihi ya kuishi na kuwekeza kwa muda mrefu

PAZIA 3

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
1,102
Reaction score
1,919
ramani-ya-tanzania-mikoa-na-wilaya.jpg


Hii ni makala maalumu kwa ajili ya kuweka fursa adhimu zilizopo kwenye mikoa yote iliyopo Tanzania. Zipo fursa ambazo zinajulikana na kila mtu, ila hapa napendekeza tuorodheshe fursa mbalimbali ambazo tuna uhakika wageni katika eneo hilo hawazijui.

Zipo fursa zilizojificha ndani ya fursa zingine, mfano, ukizungumzia kilimo, ndani ya kilimo kuna fursa adhimu kwa baadhi ya mikoa.

Mfano, kwenye kilimo Cha kahawa mkoa wa kagera, wapo wafanyabiashara wananufaika sana kwa kununua kahawa na wanatajirika kuliko wakulima wenyewe, ni hivyo hivyo hata kwenye biashara, kuna mikoa ukiwekeza kwenye duka la Vyakula hutoboi kulingana na namna ya maisha ya jamii husika.

Niwakaribishe sasa kuchangia fursa adhimu ili iwe msaada kwa watafutaji kuchagua ni wapi wakaishi kwasababu maalumu.
 
Huu uzi unalipa wakuu, njooni tupeane fursa za mikoa mliyopo au mliyowahi kuona fursa huko.
 
Simiyu pia maana pamba imeshindwa kutupa utajiri
 
Back
Top Bottom