Zijue Hasara 30 za Matusi(Kutukana)

Relaxation
Kujiamini
Relaxation? Matusi may feel like a release, but they escalate tension and lead to regret. True relaxation comes from resolving conflicts peacefully.

Kujiamini? Matusi hayajengi true confidence; they often mask insecurity. Genuine confidence is shown through respect and understanding, not tearing others down.
 
Wanaotukana ndo wanafeel hivo but in reality ndo kama ulivoelezea
 
Ajabu ni kwamba anayetukana hapendi kutukanwa. Biblia imasema jambo usilopenda kutendewa usimtendee mwrnzako
 
Andiko zuri sana lakini kwa faida ya wanaojua YESU ni nabii umeharibu sana Usiwe unaonyesha udini.
 
Andiko zuri sana lakini kwa faida ya wanaojua YESU ni nabii umeharibu sana Usiwe unaonyesha udini.
Ninapomtaja Yesu sina lengo la kuonyesha udini. Naeleza uzoefu nilio nao. Fuatilia nyuzi zangu utagundua nimetukanwa sana humu, lakini kamwe sirudishi matusi. Uwezo huo wa kuuzuia ulimi usitamke matusi ni Yesu amenipa. Kabla sijampokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wangu, sikuweza kuuzuia ulimi. Mtu akinitukana na mimi namrudishia tusi zito zaidi. Sasa hivi nooooo, Yesu ananipa uwezo wa kushinda dhambi hiyo na nyingine nyingi, ndio maana nasema kwa ujasiri: Yesu ni zaidi ya Nabii.
 
Kutukana ni kuzuri kwa afya ya akili lakini sio vizuri kutukana hadharani hususan kwa kiongozi wa umma.

Ukiwa faragha na mweza wako pia sio jambo baya sana..
Duh, ukiwa faragha ruksa kutukana? Mungu anaona na anasikia hata maneno tunayoongea faraghani. Maisha ya dunia hii yana mwisho; tujitakase tusiyakose maisha yajayo
 
Duh, ukiwa faragha ruksa kutukana? Mungu anaona na anasikia hata maneno tunayoongea faraghani. Maisha ya dunia hii yana mwisho; tujitakase tusiyakose maisha yajayo
Tutukane ili kuondoa hasira..
 
Si lazima kila jambo liwe na faida. Kuua, au kudhuru mwili kuna faida gani
Faida ya kuua ni kupunguza idadi ya watu na kuongezea fursa ya ajira. Mfano kuuza majeneza, mfanyakazi wa TCRA akifa, fursa za ajira zinatangazwa.

Faidha ya kumdhuru mwili ni kwamba, dispensary na pharmacy zinauza dawa na serikali inapata Kodi..
 
Matusi huzuia uzembe kazini, Wafanyakazi wa Tanesco wanasema wasipotukana umeme hautapita kwenye laini mpya wanayojenga!
Wakipandisha zile nguzo huwa wanaporomosha sana matusi wale majamaa aisee. Tena ya nguoni..
 
Faida ya kuua ni kupunguza idadi ya watu na kuongezea fursa ya ajira. Mfano kuuza majeneza, mfanyakazi wa TCRA akifa, fursa za ajira zinatangazwa.

Faidha ya kumdhuru mwili ni kwamba, dispensary na pharmacy zinauza dawa na serikali inapata Kodi..
Mungu alisema "zaeni mkaongezeke, mkaijaze dunia," dunia haijajaa, wewe unapunguza tena watu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…