Zijue Injini 5 za Japan zilizopendwa sana na zenye nguvu sana

Zijue Injini 5 za Japan zilizopendwa sana na zenye nguvu sana

Boeing 747

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
3,515
Reaction score
9,415
Japan ikiwa ni miongoni mwa nchi zenye kutengeneza magari kwa wingi duniani, na ikiwa inamiliki kampuni kubwa tatu za magari ambazo zipo kwenye top 10 ya makampuni makubwa ya magari dunian ambazo ni maarufu kama BIG THREE (TOYOTA, NISSAN na HONDA). Kampuni hizi pamoja na kampuni nyingine ndogo ndogo zimekuwa zikiunda magari yenye injini za technology tofauti tofauti.

Pamoja na hayo, inasemekana injini zifuatazo ndiyo injini bora kabisa na zenye nguvu sana zilizowahi kuundwa nchini Japan. Wale fans wa Mbio watazimis sana injini hizi..

1. 2JZ-GTE (TOYOTA)
Hii ni injini bora kabisa yenye nguvu kutoka kampuni ya Toyota.
Injini hii ina inline six cylinders, twin turbocharged na inauwezo wa kutoa 276hp (206kw)
Ilianza kuzalishwa mwaka 1991 mpaka 2002.

2.RB26DETT (NISSAN)
Hii ni miongoni mwa injini bora kabisa kutoka Nissan ni inline six cylinder, twin turbo charged. Ina uwezo wa 276hp (206kw)

Imetumika sana kwenye Nissan skyline na GTR

3.EJ20k. (SUBARU)
Hii ni injini kutoka kampuni ya Subaru. Ina four cylinders, boxer engine yenye turbo moja. Ina uwezo wa 295hp (219kw). Imetumika sana kwenye subaru impreza WRX na Impreza WRX STI.

4. 13B-REW (MAZDA)
Injini hii imetoka kampuni ya Mazda...Ni Wankel engine au maarufu kama Rotary engine. Ukubwa wake ni Lita 1.3 tu lakini ina uwezo wa 276hp (206kw)

Imekuwa ikitumika kutoka 1972 mpaka 2002 kutokana na ubora wake, imetumika takribani miaka 30. Weka mbali kabisa na watoto

5. K20A. (HONDA)
Hii ni injini kutoka kampuni ya Honda..Ilianza kuzalishwa mwka 2001 mpaka 2011.
Ina 212 hp(158kw)..Imetumika katika model tofauti tofauti za Honda ikiwemo Honda Civic

Nadhani wale fans wa mbio na sauti za kibabe za injini, watazimis sana hizi injini...[emoji39][emoji39][emoji39]..kwa sababu kwa sasa magari yanafungwa majenereta na si injini..







Sent using Jamii Forums mobile app
 
Y
Mdau kaongelea za petrol na zilizotumika katika sport car.

Kwa injini za diesel kwenye kampuni ya Toyota 1hz ndio amempatia sifa kubwa duniani na kumsaidia kuwa na mauzo makubwa miaka ya nyuma.

List ya engine bora za Toyota za Diesel
1. 1HZ
2. 2L/5L
3.14B
4. 1KZ
5. 2H
Shukrani mkuu. Kwangu the best ni 1HZ, then 2L/5L then 1KZ. Hiyo 14B inatumika hasa kwenye gari gani za Toyota
 
The best engine kwa muungurumo ni Engine iliyofungwa kwenye Nissan Civilian.
The best small engine inaenda kwenye engine ya Suzuki Carry!
Nissan TD42 ile ndio hatari zaidi, toka kwa Patrol mpaka Civilian.

Huku Toyota ana 1HZ na 1HD zinazokaa kwenye Landcruisers na Coaster. Kwangu hizi ni hatari zaidi bila kuisahau ile ilioko kwenye Land Cruiser 60 series kitu kama ni 12HT.
 
Back
Top Bottom